Zari, Daimond Kimeeleweka, Babu Tale Afanya Kweli Sauzi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Zari, Daimond Kimeeleweka, Babu Tale Afanya Kweli Sauzi

Zari, Daimond Kimeeleweka.... Babu Tale Afanya Kweli SA
KIMEELEWEKA asilimia 90! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya meneja wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ kutua pande za Afrika Kusini kwa lengo la kusaka suluhu ya msanii wake huyo na mama watoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

KWA NINI ASILIMIA 90?

Kwa wafuatiliaji wa magazeti Pendwa, hakuna asiyejua kuwa familia inayomzunguka Diamond inavyomkubali Zari kuliko mwanamke mwingine yeyote hivyo kilichokuwa kimebaki ni mtu tu anayeheshimika na Zari kwenda kumuombea radhi Diamond.

“Sisi wote tulikuwa tunaomba tu mtu kama Babu Tale (Hamis Taletale) aamue kujitoa kwenda maana Zari licha ya kuwa na msimamo, anamheshimu sana Tale na ndiyo maana alivyoamua tu kwenda, tuna uhakika asilimia 90, Zari anarudi Madale,” mmoja wa wanafamilia ya Diamond aliling’ata sikio Ijumaa Wikienda.

AZIDI KUSHUSHA UBUYU

Mwanafamilia huyo alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa kitendo cha Tale kutua Sauz ni kwenda kumaliza biashara kwani, kama familia, wote walikuwa wanamhitaji Zari na walikuwa wakimchombeza kila uchwao.

“Wewe angalia mama Diamond kila siku anawasiliana na Zari, Zari anamtumia picha za watoto kila wakati. Anamuweka karibu kiasi kwamba Diamond mwenyewe na ubishi wake anakuwa mpole,” alisema mwanafamilia huyo.

IYENA IMECHOCHEA MOTO ‘Fujo’ za kumrejesha Zari Madale zilichochewa zaidi na picha mpya za Zari na Diamond zilizovuja Ijumaa iliyopita mara baada ya msanii huyo kuachia wimbo wake mpya uitwao Iyena.


Katika picha hizo za ‘behind the scene’ ya wimbo huo, Zari alionekana alishaini kwa raha zake katika mavazi yanayoashiria si tu kwamba ni mzazi mwenzake bali ni mke halali wa ndoa wa Diamond.

FAMILIA YAZIDI KUVUTIWA Mara baada ya picha hizo kusambaa, mwanafamilia ya Diamond aliyezungumza na Ijumaa Wikienda, alisema picha hizo ziliongeza kasi ya kampeni ya kumrudisha Zari katika familia yao kwa kuvutiwa na muonekano wao.

“Kila mtu akasema yes, huyu ndiye mke halali wa Diamond na si mwingine yeyote,” alisema mwanafamilia huyo na kuongeza: “Yaani kwa sasa mama Diamond, Esma na sisi wote tunamsubiri kwa hamu maana Tale kwenda kule tunajua ni uhakika.”

MITANDAO YASHADADIA

Mbali na familia, baada ya kuvuja kwa picha hizo, mitandaoni kulichafuka ambapo watu mbalimbali walitupia maneno wakiiunga mkono kurudi kwa penzi la Diamond na Zari huku wakimrushia madongo makali Hamisa Mobeto, mrembo aliyechepuka na Diamond kisha kuzalishwa mtoto mmoja.

MSIKIE MAMA D

Katika harakati za kukushibisha ubuyu huu wa motomoto, Ijumaa Wikienda lilimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambapo yeye alijikita zaidi kumsifia Zari kuwa ndiye mama Madale, na kitu kinachomvutia kwake ni mwanamke ambaye anajua jinsi gani anaweza kumjali mumewe kwa kila kitu na mambo mengi ya usafi wa ndani.

“Ninachojua mpaka sasa Zari ndiye mama mjengo, anajua jinsi gani ya kumfanya mume akajisikia yuko na mke na kwa upande wa kuweka nyumba poa huyu mwanamke ni hatari halafu kingine ananikosha kuhusu wajukuu zangu,” alisema mama huyo.

ESMA SASA…

Kwa upande wa dada wa mwanamuziki huyo Esma Khan ‘Esma Platnumz’, alisema kuwa Madale iko wazi na wanamkaribisha Zari, kwani kwa kipindi ambacho alikuwa hayupo, wametambua umuhimu wake.

“Jamani Zari ni mwanamke sijui hata nisemeje kwa sababu kwanza anajua kuweka nyumba safi mpaka ukiingia ndani unakubali kila kitu, kingine tunamkumbuka sana na umuhimu wake sasa unaonekana yeye aje tu Madale inamsubiri,” alisema Esma.


TUJIUNGE NA TALE

Tale alipotafutwa na Ijumaa Wikienda ili aweze kuweka bayana mafanikio ya safari yake hiyo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita, alisema kama mtu ambaye Zari anamheshimu, hakuna kitakachoshindikana.

“Kwangu ni kazi ndogo sana kuyarudisha mapenzi ya Zari na Diamond na kwa vile mashabiki wote walikuwa wakinilaumu mimi nimeshindwa kuweka mambo sawa lakini naamini kabisa familia hiyo itarudi kama zamani,” alisema Tale.

MOBETO KAMA ULIVYOSIKIA

Baada ya kusikia familia ya Diamond imeweka msimamo wake kuhusu kumhitaji Zari arudi Madale, Mobeto alitupia ujumbe mzito kwenye ukurasa wa Diamond Instagram alipoweka picha na kuhoji mahojiano (ya kumponda Mobeto kuwa ni mchafu), aliyoyafanya dada yake Esma alikuwa mzima au alikunywa ndipo Mobeto alipolipuka na kumtaka mwanamuziki huyo aoe mke anayehitajika na familia hiyo.

“Inabidi umuoe mwanamke ambaye anatakiwa na ndugu zako…na mameneja zako bila kusahau mashabiki… siyo kutwa miye mtoto wa watu naandamwa na kukaliwa miye kooni.

Sijakuita wala kukufunga kamba…kila siku maneno kwani alishindwa kukufata kukushauri mpaka akimbilie kwenye Matv na mitandao? Unapokaa hapajui? Namba ya simu pia hana? Kwani miye hayo Matv hayaombi kunihoji mbona nakaa kimya? Tena saa ingine (nyingine) nakaa kimya kuwasitiri kwa mengi na pia @ deedaylan (mwanaye) akikua asione hii migogoro lakini ndugu zako hawabebeki its too much, talk to your familia maana wewe ni mwanaume na una uwezo wa kuyamaliza…na pia uwaambie unahitaji mke na siyo house girl wa nyumba…” alitoa povu Mobeto.

TUMEFIKAJE HAPA?

Februari 14, mwaka huu, Zari alitangaza kumpiga chini Diamond kwa kile alichosema kuwa staa huyo amezidi ‘mambo mengi’ hivyo ameamua kujiweka pembeni kuepusha msongamano kama si maradhi.

Licha ya Diamond kuonesha kukubaliana na matokeo, familia yake imekuwa ikijitahidi kurudisha uhusiano huo kwa nguvu huku ikielezwa kuwa Diamond amekuwa akijishusha na kuomba radhi lakini alipozungumza na gazeti hili wiki iliyopita, alikanusha taarifa hizo. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.