TID: Tangu Mangwea Amefariki Sijawahi Kupata Rafiki Wa Kweli - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

TID: Tangu Mangwea Amefariki Sijawahi Kupata Rafiki Wa Kweli

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kama TID amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi kupata rafiki kama aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’.

TID amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv ambapo alisema mwaka huu hakufanya Tamasha la kumkumbuka kwa sababu imekuwa katika mwezi Mtukufu wa ramadhani.

Ni kweli kila mwaka huwa tunafanya tamasha hilo kwa sababu tunakuwa na sababu na pia na uwezo lakini mwaka huu kitu kilichotufanya mpaka hatufanya tamasha letu ni Ramadhani ambayo imetubana na kusema kweli tupo kwenye swaumu.

Lakini pia TID aliwatolea povu watu ambao amewaita Masnich ambao walijitokeza wakati Mangwea alipofariki:

Mangwea alipofariki watu kibao walijitokeza na wengine kabisa wapo frontline wanachangisha wakati Ngwea yupo hai hawakumpa tamasha hata siku moja haya leo hii Ngwea hayupo hakuna hata mtu mmoja aliyesema tumuenzi Ngwea watu wana roho mbaya na masnich .

Wasanii kibao unaowaona leo ni masnitch tu nawaangalia sana ndio maana siwezi hata kuwa na ukaribu nao sina marafiki sahivi wala sitakuja kupata rafiki kama Ngwea”.

Mangwea alifariki dunia miaka mitano iliyopita na alikuwa rafiki wa karibu sana wa TID.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.