Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 28) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 28)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 28

Alisalimiana na vijana wawili waliokuwemo ndani ya gari hilo, kisha wakaanza kumuongoza kwenda katika jengo la kampuni......

bado usingizi ulikuwa unamuuma licha ya kulala muda mrefu, kitanda alichokilalia kwa mara ya kwanza alikuwa hakuwai kukilalia tokea azaliwe, hakuisi kama amelalia godoro kwa namna lilivyokuwa limejazia na kufungasha, moyo wote ulikuwa unacheka, kila alivyoangalia jinsi alivyopendeza, aliachia tabasam, na kujiona kama amezaliwa upya duniani.
"haya ndo maisha ambayo mwandam anatakiwa aishi ,, gari zuri, suti nzuri, na vingine vizuri vinakuja huko, mbona watanikoma mimi!.

aliongea peke yake ndani ya gari, huku akiangalia makini kwa mbele, ili gari linalomuongoza lisije likampotea, pia alikaa makini kusoma mazingira, aijue bara bara ikiwezekana wakati wa kurudi arudi peke yake kama itawezekana.
kila kona aliyopinda aliiangalia vizuri, baada ya dakika kadhaa wakawa wanaingia posta katika geti la jengo la kampuni, aliserebua gari mpaka katika paking, akapaki gari lake.
" Dah, kwa namna hii, hata Mungu unaweza kujikuta unamsahau maana hizi ni zaidi ya raha dadeq, kuendesha gari raha nyie acheni bhana ,,
bado aliongea peke yake akiwa anaangalia gari lilivyo zuri, imani za kuamini kama ndo yeye huyo aliekuwa akilalia viazi usiku zilimuingia na kujikuta anacheka peke yake, alitikisa kichwa akafungua mlango, alipokuwa tayari ameshuka alifunga akasimama kuanza kuliangalia jengo kwa mara nyingine, ,, muda huo huo alimuona mr mtikira anakuja akitokea ndani, alianza kutembea kumfata huku akiwa na furaha, walikutana katikati ya jengo la kampuni na sehemu lilipokuwa gari lake, wakasalimiana, wakajuliana hali kisha wakatembea kuelekea ndani huku mtikira akimwambia wafanyakazi wote washafika na wamekaa kumsubiri yeye.

walifika katika ukumbi wa kufanyia vikao vya mjumuiko wa wafanyakazi wote, wakakaa kwenye viti, wafanyakazi wote wakimtolea macho seid, hasa watoto wa kike waliowengi walihadaika na uzuri wa sura alionao seid, mapozi yake yaliwafanya watoto wakike wawe na coment nyingi sana mioyoni mwao, seid yeye akiwa hana habari, wala hakuitaji kumwangalia mtu yoyote usoni.

" Habari zenu wapendwa? ,, Sasha nae alikuwa amechelewa kidogo, muda huo ndo alikuwa anaingia, wote waliitikia ,, " nzuri ",,, kisha akakaa kwenye kiti chake kilichokuwa pembeni ya kiti alichokaa mr mtikira, kiu kilikuwa kimembana, kwa kutembea mbio mbio, alifungua maji akanywa kisha akasimama kufungua kikao yeye mwenyewe.

" Jamani nimecheleweni nisameeni mambo ya folen za ilala, ,, Nimesimama mbele yenu, kama kiongozi wa wafanyakazi idara zote hapa katika kampuni yetu ,,, aliongea sasha baada ya kusimama, akafungua makaratasi ambayo yalikuwa yamechapichwa, macho yake yakiwa yanaangaza kwa baadhi ya wafanyakazi  ,, kikao hiki ni tofauti kidogo na vikao vyengine ambavyo tumevizoea vinavyokuwa kiofisi, ,, tunajua kuwa kampuni yetu imekaa muda mrefu kidogo bila kuwa na mkurugenzi ambae husimama kama bosi wa kampuni, na hatimae kukaa katika mikono ya menega mr mtikira hapa kipindi cha miaka mitatu, ,, Wamiliki wa kampuni yetu itambulikanayo kama G.A.R.T Company ikiunganisha majina manne ya wamiliki, iliyosajiliwa na kutambulika serikalini na katika anga zote za makampuni mwaka 2010, hatimae wamemchagua Seid mtoto wa Sharif mzawa wa Zanzibar kuwa mkurugenzi wa kampuni hii, na uongozi wote uliokuwa hapa kuwa chini yake, hivyo nisingependa kuongea sana, naomba nimkaribishe, ili muweze kumuona, na kutoa hoja zake za uwezo wa kuiongoza kampuni ya G.A. R.T company kuhakikisha haitetereki... Mr Seid! ,, unakaribishwa katika kikao hiki adhimu, uweze kuongea na wafanyakazi wako, lakini kabla ya hapo, tunakukaribisha sana katika kampuni hii, tunakukaribisha pia katika jiji letu la dar es salam, tulikuona kabla hujafika kupitia email zetu na website ya kampuni,, , hivyo Karibu sana.

alipomaliza kuongea alikaa chini, seid kidogo moyo ulikuwa unaenda mbio, majukumu makubwa sana alishajua yanataka kutua mikononi mwake, aliuangalia umati wote wa watu waliokuwa wamefurika ukumbini bila kupata majibu ya aanze vipi kuongea nao, wazee wenye mvi zao walikuwa wamejazana pale, alijiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu, alisimama akiwa bado anajiuliza aanzie wapi ,,, " Leo seid nimeisha, nkiongea ujinga tu hapa natimliwa leo leo ,,, alisema moyoni  huku akiwa anasimama, kijasho kilianza kumvusha usoni na mgongoni, woga bado ulikuwa umemkaa, hasa kila alipoangalia mbele na kuona watu walivyomtolea macho ndivyo alivyozidi kudata....

Mbali na mawazo yake kwenda mbali sana, kila mtu hakuangalia sehemu nyingine isipokuwa kwake, Namna alivyokuwa ametokelezea aliwachanganya wengi hasa watoto wa kike, huku wazee wakubwa wakikaa sawa kusikia kijana ataongea point gani.

" Ndugu zangu ,, baba zangu ,, Wazee wangu.. nshatambulishwa vya kutosha, ,, nadhani sina la kujiongezea kwa sababu hata sifa zangu zilishaorodheshwa kwenye website ya kampuni ambazo kila mmoja alizisoma, ,, waswahili wanasema ,, kuku mgeni, hakosi kamba mguuni, na mimi ni mgeni siwezi kukosa aibu au hata kigugumizi cha kuongea jambo la maana mbele ya umati wa watu kama huu ,,, kikubwa ni kuwa, sitotumia ujinga nlionao kuiongoza kampuni, bali ntaitumia elim nliyonayo kuleta ubora mkubwa katika kampuni ,,, Elim yangu ni ya mastaz nimesoma chuo kikuu cha uingereza, nlipofaulu mr andri komen aliniita akiwa pamoja na Raferisty, wakanambia kila kitu kuhusu kampuni, tuliongea sana wakanipatia mikataba tukitumia njia ya mitandao kumaliza kila kitu ,, ,, Katika maisha ya mwanadam wa kawaida, unaweza kuwa na Elim ya chuo ukaonekana kama una elim ya darasa la kwanza kutokana na vile utavyoitumia, pia unaweza kuwa na elim ya form fo lakini ukaonekana una ya chuo kutokana na utavyoitumia pia, huwa napenda kwenda kwa mifano kwa sababu mifano ndo imepelekea mimi kufika hapa nlipo, hata watu wakubwa wote walipendelea kutumia mifano.

Seid aliwafurahisha wazee kwa maneno yake ya hekma, aliweka baadhi ya mafumbo pamoja na methali mbali mbali kwa ajili ya kumfurahisha kila mmoja, aliongea muda mrefu, baada ya saa moja kikao kilimalizika, wote waliokuwa kikaoni walirizika na point zake, hakuna ambae alikuwa na neno zaid ya huyu kijana kweli msomi, alitaja namba zake za cm kuweka online mawasiliano yake kama kiongozi wa kampuni, kila mtoto wa kike aliichukua namba akiwemo sasha, ilitoka ofa siku hiyo ya kila mmoja kurudi kwake mapema, baada ya kikao hakukuwa na kazi nyingine, seid nae alipanga mambo yake vizuri ofisini kwake akiongea ongea na baadhi ya wafanyakazi, ili kesho aanze kazi rasmi..

Baada ya kuweka mambo vizuri, wafanyakazi wengi muda huo walishaondoka, alitoka nje akiwa peke yake mara tu alipokaa ndani ya ofisi zaid ya nusu saa akiweka vitu sawa, aliangalia muda akakuta ni saa nne na nusu, kabla ya kufungua gari yake ilisikika sauti ya kike ikimuita kwa nyuma, aligeuka haraka akamuona sasha anakuja sehemu aliyopo.

" Ushamaliza! ,, aliuliza sasha alipofika sehemu aliyoko seid kama amemaliza kazi zake za kiofisi alizokuwa nazo.
" Yah nimemaliza muda huu.
" Ok poa,  wapi sasa hivi.
" hapa sina pa kwenda zaid ya home nkasome mazingira basi, si unajua niko katika hali ya ugeni.
" Yah i know that ,, but mimi pia leo sina mipango yoyote, itakuwa mbaya kama tukienda sehemu moja nzuri tukatulia mpaka mida ya lunch hivi, then, nadhani tutakuwa tushapeana kampani kubwa sana mpaka muda huo. ,, sasha aliongea akimwangalia seid ndani ya kiwani mikubwa aliyokuwa ameivaa, 
" ammmmmm! ni wazo zuri sana, ,, alifikiria kisha akajibu ,, ilaaa maeneo gani, usije ukaniuza naogopa sana dar hii.
" Hahahaaaa! ,, hapana bhana, maeneo ya sehemu nnayokaa Ilala.
" Na itakuwaje kuhusu usafiri coz nadhani na wewe una wako.
" Hilo sii tatizo, unaweza kuacha gari lako ,, tukenda na langu......
" Ok sawa.

Walikubaliana, alifunga gari lake wakaongozana mpaka katika gari la sasha, wakaingia ndani na kuanza safari huku seid akiwa na Mawazo ya bora azunguke sehemu tofauti ili alijue jiji kwanza, kuliko kurudi nyumbani kukaa peke yake.
" Zanzibar wanasemaje huko seid ,, aliuliza sasha akiwa yuko bara barani anakanyaga mafuta.
" Huko Z,bar salama tu.
" Nasikia wala urojo nyie huko ,, aliuliza kama kumtania, kabla ya kujibu wote waliachia kicheko, walizoeana ndani ya Muda mfupi, Sasha alikuwa anapenda sana kuongea, baada ya nusu saa walikuwa maeneo ya Ilala, muda wote seid alikuwa anaangalia mazingira namna dar ilivyojengwa, huku akiisifia, walifika sehemu aliyokuwa akiishi sasha, akamuomba waingie ndani ili abadili nguo, baada ya kupaki gari, wapumzike kidogo kisha ndo watoke.....

"Karibu sana kwangu mr seid ,, alimkaribisha walipokuwa tayari wameingia ndani.
" Asante sana, yani mwanamke uko full, ,, unaishi peke yako hapa? samahani lakini, au mzee yumo ndani.
" Noo naishi peke yangu, ni nyumba yangu, so rilax.
" na mzee yuko wapi sasa.
" Ah potezea bhana seid, kwa sasa naweza kusema niko single.
" Una weza,, ina maana huna uhakika.
" Bwana seid nini jamani Ah,, ngoja tutaongea vizuri niingie ndani nibadili nguo coz joto kisha nakuja tuongee vizuri.

Sasha alimuacha seid sebleni, akaingia chumbani kwake, alijitupa kitandani akiwa ameachia tabasam, mawazo mazito yalimchukua ghafla akiwa anajigeuza huku na kule, ni miongoni mwa madada wa kwenye kampuni ambao walishamzimia mchizi, alijisikia furaha kubwa sana alipofanikiwa kumteka seid mpaka nyumbani kwake, aliamini lengo lake aliloitaji linaweza kukamilika.....
" Seid nimetokea kukupenda kiukweli, kijana mzuri, unavutia, pia bosi wangu, una vigezo vyote vya kuwa mpenzi wangu, nami ni msichana mzuri najiamini, nimewaringia wengi ila nahisi wewe ndo mbuyu wangu nimenasa...

Aliwaza akiwa anashusha na kupandisha pumzi yake taratibu, aliinuka kitandani akafungua kwenye kabati akaangalia nguo zote zilizokuwemo, alitoa nguo moja ya pink iliyokuwa inambana kwa kumuachia akiivaa na kufanya maungo yake yatamanishe kwa mtu, alivua nguo alizokuwa amevaa za kiofisi, akaenda kuoga alipomaliza akavaa nguo yake, akajipiga piga mapoda na mamekapu kisha akarudi sebleni.....

Seid macho yalimtoka kidogo baada ya kumuona sasha, hakuamini kama ameumbika vile, mavazi ya kiofisi aliyokuwa ameyavaa yalimficha maumbile yake ,,, " Waaaaaaao beutfull Garl ,,, maneno yalimtoka moyoni...

" nimekuja sasa now niko okey, tunaweza kustori mpaka mida flan tukaenda lunch ,, aliongea sasha baada ya kukaa kwenye sofa lililokuwa mbele ya alilokaa Seid, alimkalia mikao ya kihasara hasara wenyewe wanaita Take away ili seid aingie mtegoni, macho ya kijana yalipelekea moyo wake kuwa mbali sana kimawazo, zile ashk za mapenzi zote zilishamtawala muda huo, ukizingatia kitu kilichomfanya kipindi anasoma aweke nadhiri ya kurudi dar ni wingi wa wanawake wazuri waliomchanganya, mipango yake ilienda sawa akachaguliwa kufanya kazi dar hiyo hiyo, kitu ambacho mbali na cheo alicho pewa alifurahi.
" umependeza sana mwanamke ,, alisema seid akiwa bado haamini namna sasha alivyo mzuri, wakati alipovaa kiofisi alionekana wakawaida sana.
" asante mr ,,, aliitikia kwa pozi, sauti iliyoivaa....

Ni sasha ambae tayari alikuwa amemuitaji seid kimapenzi, mtoto wa kike alikaa mikao ya hasara hasara mbele ya macho ya Seid, kuhakikisha anaingia mtegoni....
" Nadhani yoyote alioko katika dunia yako ya mapenzi anainjoy sana.
" Kwa nini mr!.
" Coz so beutfull garl.
" Kawaida bhana Seid but niko alone sasa hivi mbona ,, alisema akiwa anampiga jicho legevu seid.
" acha uongo bhana sasha.
" Serious tena.
" Ina maana wanaume hawakuoni au!? ,, alisema huku akiegamia kwenye sofa baada ya kutumia muda mrefu kumwangalia.
" Kujitunza tu bosi, kwa sababu si kila mwanaume anaekuitaji anakupenda kimaendeleo ,, nnapojua kitu kama hicho sitomkubalia kila ataenitaka, na ingekuwa hivyo, Um! ,,, ningejaza nyumba nzima hii.... 
" Ok ila vizuri mtoto wa kike kujitunza.

Mpaka mazungumzo yalipofikia tamati, Seid alikuwa hajiwezi, alitamani chochote kitokee kwa namna alivyokuwa, sasha aliomba waende lunch baada ya kutumia muda mwingi kuongea, walinyanyuka wakaingia katika gari la sasha wakaanza safari ya kuelekea restaurant ambayo haikuwa mbali sana na nyumbani kwake.

Wengi sana katika restaurant hiyo walikuwa wamemzoea sasha, ulikuwa ni mgahawa wake wa kupata chakula kila siku anapokuwa nyumbani, wanaume wengi walijikuta wakibabaika nae kwa jinsi alivyo mzuri, wapo waliojaribu kumfatilia kumfata kimapenzi, lakini wote aliwatolea nje. walipofika eneo la mgahawa na kupaki gari, walianza kutembea huku sasha akiwa amemshika seid mkono tabasam nje nje, kila aliekuwepo eneo hilo alishangaa kumuona sasha akiingia na men wakati si kawaida yake, tena wameshikana mikono kuashiria wana uhusiano wa karibu, wapo madada pia waliemuona rafiki yao huyo akiwa na Seid, hawakutumia muda mwingi kumwangalia Sasha bali na wao walimuangalia Seid namna alivyotokelezea mfano wa chotara wa kiarabu, mwili uliotanuka akionekana mbavu kidogo...

Walikaa moja ya viti vya ndani vya restaurant, walipiga stori mbili tatu kabla ya mhudumu kuja kuwaudumia, Seid alitumia muda mwingi kumwangalia Sasha akimpa hundred %z za uzuri aliokuwa nao ndani ya moyo wake.
" Nadhani huu mji umeumbiwa wazuri tu wabaya wote wanaishia mikoani, sikuwai kutembea z,bar masaa mawili nkashindwa kuona kimwanamke kimekunjiana sura, lakini huku kila nnae muona ana uzuri wa aina yake. au kuna chombo maalum kinawachuja?, ukiitaji kuingia dar bila kuwa mzuri rudi kwenu!!? Oooh Seid mbona huku panakufaa? ,,, aliwaza moyoni wakati huo mhudumu alikuwa anawaletea kile walichoagiza, alikiangalia chakula ambacho ameletewa akajikuta anashiba ghafla kwa kilivyo kuwa kimeandaliwa.

" Welcome mr seid, hapa chikken, soseji, juis, Ndizi, baga, matunda, ,,, ni wewe tu ujisikiavyo kuanza, ,,, Sasha alimkaribisha seid, akamtambulisha vyakula vilivyoko mezani pozi kwa pozi,.

" Um! Chiken, Ndizi, Soseji, baga na hivi vizaga zaga vingine, mbona naingia kwenye dunia isiyo yangu hii? ,, alijiuliza moyoni akiegamia kwenye kiti kama mtu aliechoka huku akishusha pumzi.
" Nini ? ,, Sasha alimuangalia akamuuliza.
" Harufu ya chakula tu imenifanya nishibe ghafla, ngoja nikivutie kasi ili nianze kutia vitu upya.

Alicheka sana sasha kwa maneno ya seid, watu waliokuwa eneo hilo waliowengi bado waliendelea kumwangalia Sasha, huku baadhi ya masistar duh nao wakijigonga kivyao kumwangalia kijana aliekaa na sasha namna alivyo katika muonekano wa kisasa.

" Rita yule kaka mzuri! ,, alisikika dada mmoja aliejulikana kwa jina la batuli akimshtua mwenzake.
" Yuko wapi!? ,, aliuliza rita.
" Yuule pale amekaa na yule mdada.
Rita aligeuka pembeni yake akawa amemuona,  ,,, " hhmm hand some wa ukweli si kitoto. ,, alisema baada ya kuwa amemwangalia.
" alafu atakuwa mzanzibar au kachanganyika na uarabuni.
" um shost yangu weeee, ebu tuongee ya kwetu achana nayo hayo.
" Rita kweli mi pozi zote zishaisha hapa, ujue kuna mwanaume unae muona ukajikuta unapagawa ee! ,, si kuwa ni mzuri saana but yani muonekano wake ni mwanaume wa ukweli unamuona kabisa amekamilika.
" kwa iyo unamtaka hapo ulipo.
" Ah! tuachane nayo mtu mwenyewe naona uko kivyengine.
" Bwana ako anakutoa mashavu hayo ukimsaliti mtu mwenyewe mjeda yule.
" aaaaaagh yeye mwenyewe anachepuka, bongo hii pesa mbele kiuno peleka twanga, wangapi anawatamani huko na yeye?

Walipokuwa wanaendelea kumdisi seid bila yeye mwenyewe kujua, Sasha alimuomba aende kujisaidia mara moja, aliinuka kwa ajili ya kwenda chooni, akamuacha seid peke yake.. Batuli hilo aliliona, alimuangalia sasha mpaka alipoingia bafuni, alitoa chek card yake kwenye mkoba akamuomba rita amuangalizie, aliinuka akatembea mpaka alipokuwa seid.
" Hi
Seid alinyanyua uso wake akangalia mbele aliposikia anapewa hi, pumzi zilikata ghafla alipoona amesimamiwa na msichana ambae ni beutfull mbele yake, akiwa ndani ya kipensi jinzi kifupi kilichoishia mapajani, kikiwa kimejichana kwa duara ya kopa.
" Hi too.
" Ok, sorry mr, this's my chak card, pliz naomba unicheki en time utapokuwa free.

Alipewa kadi akaipokea, batuli aligeuka akaondoka huku kiuno chake kikichanja mbuga, seid alibaki ameduwaa, kama kungekuwa na nzi karibu yake angeingia mdomoni kwa jinsi alivyokuwa ameuacha mdomo wazi.

" wewe batuli mbona una balaa hivyo ,, rita alimuuliza baada ya kufika na kukaa.
" best we niache tu, najijua nlivyo nafsi yangu huwa ikiitaji kitu sipendi nikikose, masiara mbali tokea nianze kula kwenye hii restaurant mwaka sasa, wameingia wanaume wengi wazuri lakini sijamwona hata mmoja nkasema huyu yuko gud kama huyu men.
" um! Shauri yako lakini.....

Sasha alirudi akakaa kwenye kiti akomba seid amsamehe kwa kumuweka peke yake, chek card aliyopewa alishaiweka mfukoni tayari, walimalizia kula wakajifuta futa midomo, wakafanya malipo na kuondoka..

" kumbe nna Uhb wa namna hii hadi nawatoa udenda watoto wa kike! ,, yule dada mzuri ila, yani nguo alizovaa na yeye vyote vinaendana na inaonekana wale ndo wahuni wa jiji wale maana dah!!!,, kipindi yuko kwenye gari ukimya baina yake na sasha ulitanda kidogo kumpelekea kuwa na mawazo juu ya batuli dada aliempatia chek card iliyokuwa na maelezo kuhusu yeye.
"mbona unaonekana uko mbali kimawazo bosi, sasha aliiona hali ya seid.
"hapana, ni vijimambo tu ambavyo naviona ndani ya jiji ndo vinanifanya niwaze hivi.
" Kitu gani sasa umekiona kikubwa seid, mimi naona hujaona chochote, ngoja siku moja ntakuja kukutembeza sehemu tofauti meridian, ambians huko, sansiro vetnal uone jiji, yani huku ni kama ulaya tu wangu.
" Haa!!! ,, aliitikia kwa kushangaa akigeuza uso kumwangalia aliposikia ni kama ulaya tu, walifika nyumbani kwa sasha wakapaki gari na kuingia ndani.

Walikaa sebleni dakika tano wote wakionekana kushiba, walipokuwa wanaendelea na mazungumzo ya hapa na pale, ghafla sasha alishusha pumzi ya aina yake, akakaa mkao wa kubinua kiuno kwa nyuma akiwa ameegamisha mikono pembeni mwa sofa, alimwangalia seid akamwambia waende chumbani kwake, eneo la sebleni anaona si zuri kwa muda ule wa joto wakati chumbani kuna kiyoyozi kinapuliza vikali huku akionekana kuwa na jicho la mitego.

Tukutane sehemu ya 29 kesho sehemu hii.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.