Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 25) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 25)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 25

Hamad alichanganyikiwa baada ya kusikia maneno hayo upande wa pili wa cm, Mama yake alipomaliza kuongea hivyo alikata cm, moyo ulianza kumuenda mbio kijana, alijaribu kuipiga huku Sulaiha akiuliza kuna nini, cm haikuita, alijaribu tena na tena majibu yakawa haipatikani, kijasho kilianza kumtoka, aliongeza mwendo wa gari ili afike nyumbani haraka kuangalia baba yake kapatwa na nini.

Seid kipindi ametulia nyumbani, anapiga stori za hapa na pale na mama yake, alipokea message kupitia email iliyokuwa inatoka kwa Christina, aliifungua kuiangalia inasemaje akiwa anatabasam,,, " Nimekumiss Seid, ,,Nadhani ushabadilisha line kwa sasa, naomba unitumie namba yako nikuskype tuongee..

( Repley > Ok Mchumba 07 12******* nlikuwa na mawazo hayo ila niko naongea na mama, ntakutumia message badae ili unipigie nisikie Sauti yako mrembo ,, aliandika maneno hayo ambayo yalikuwa kwa kingereza akayatuma ,, aliweka cm pembeni akaendelea kuongea na mama yake.

" Naona unachart na wazungu tu sasa hivi. Bi najma alimuuliza mwanae.
" Hahahaaa Hapana mama, rafiki yangu tu huyu ,,, ,, Itabidi niende kwa bibi leo nkiwa bado nanukia Paundi za pesa zinazotumiwa huko ili nkamuachiemo japo ya matumizi, ,, si ashazeeka sana sasa hivi ?,, alimpoteza maboya mama yake kwa kuingiza mada nyingine tofauti na swali aliloulizwa.

" Miaka miwili tu tokea hujaonana nae, Hajazeeka utamkuta vile vile ,, ina maana huko kunatumiwa pesa tofauti na za huku? ,, alimjibu mwanae, kisha akamtupia swali lengine.

" Um! sasa mama pesa za Tanzania na zenyewe pesa! ,, si makaratasi tu haya hayana thamani yoyote!.

" Ziko wapi sasa mbona hujanionesha.

" Mama hata nkisema nikupe huku hakuna sehemu wanapozitumia zaid ya kwenda kuchange bank au uwanja wa ndege, zingekuwa dola sawa lakini paundi hakuna.

" Haya mwanangu, tumia tu hizo paundi zako tuachie makaratasi yetu sie.....

******
Hamad na Sulaiha walipaki gari mbio mbio baada ya kufika nyumbani, hamad alitembea kwa kukimbia kijasho kikiwa kinamtoka, alifungua mlango na kuingia ndani.

Alipoingia alishangaa ndani kuona pamepambwa, kulikuwa na mkusanyiko wa watu tofauti akiwemo baba yake akiwa katika afya yake, Sulaiha nae aliingia ndani kwa mshangao, yalipigwa makofi mengi huku wakiimba ,,, " Happy barthday Too yuooo!!! ,,, Happy barthday too yoooo!! ,, Happy Barthday You are Hamad ,, happpy barthday Too yuooooooooo!!!..........

Hamad hakuwa na la kufanya zaid ya kuachia pumzi akashika kiuno na kuachia kicheko cha chini.

" Suprize mwanangu ,, alisema Mzee Shaibu akimsogelea mwanae ,, nliamini kabisa kwa harakati zako ulizonazo, utakuwa umesahau kuwa leo ni siku yako ya kuzaliwa ,, Tusamehe kukushtua kijana wangu ila ,, Karibia kwenye shuguli tafadhali.

Hamad alinyanyua uso wake akionekana kuwa na Jazba, aliwaangalia watu waliokuwa wamesimama mbele yake, akamuona Ticha, Waziri wa Elim pamoja na mke wa Ticha, aliachia tabasam jazba zote akaziweka pembeni, alimsikiliza mzee wake akasogea sehemu ilipokuwa kake.

" Naombeni siku nyingine isije kuwa hivi,,huko tulikokuwa karibia tugonge , ,, Mama! ,, Mkwe wako karibu afe kwa presha, hata kama ni suprize ifanyike kwa matukio mengine si kuhusu wazazi, wengine hapa wazazi wetu ndo roho zetu jamani!, Eh......

Aliongea akiwa amevimbisha uso, alimfata Ticha akamkumbatia siku nyingi walikuwa hawajaonana, kilikuwa ni kishuguli kidogo cha haraka haraka cha kuzaliwa kwake, aliwalisha keki wazazi wake mke mtarajiwa wake, Ticha, mkewe, mtoto wa ticha, Waziri pamoja na wengine waliokuwepo anaowajua.......
________

Maisha ya Sauda yaliendelea kuwa mazuri kila kukicha, alibahatika kuzaa mtoto wa kike na mmewe An'war, Watu waliokuwa wakifanya kazi na Masoud walimsahau masoud ndani ya muda mfupi, hasa kwa jinsi Sauda alivyoonekana mkarimu kwa kila mmoja, walijaribu kumdadisi chini chini lakini aliwajibu shot ,, " Hajui kuhusu yeye " ,, basi.

Mida flan hazikuacha kupita stori za kumzungumzia Masoud, ilikuwa ni kama maajabu kwa baadhi ya wafanyakazi kumpoteza jamaa katika mazingira ya kutatanisha, na kupata mshangao zaid walipomuuliza sauda aliekuwa mke wake na kuwajibu anavyotaka yeye.

Wapo wengine ambao walifurahi kutokana na ujeuri aliokuwa nao pale mjengoni, lakini wengine walifatilia chini chini habari zake, japo ni ndani ya miaka miwili imepita bila kufanikiwa kujua hata skendo zake.

Sauda hakuacha kwenda kumsalimia mtaalam aliempatia dawa za kumtengeneza Masoud, siku nyingine akimuachiamo chochote kama asante, mambo yake yalishaenda kama alivyotaka lakini hakutaka kumsahau mtu aliemfanikishia kila kitu.

********
Ilipofika jioni jioni ya siku hiyo Seid alianza safari ya kwenda kwa bibi yake kumsalimia, kwa jinsi alivyokua ameng'ara kila aliemuona alimtolea macho.....

" Mtoto wa Bi Najma mmemuona huyoo !!

kipindi anatembea bara barani akitafuta japo gari apate lift, alisikika dada mmoja aliekuwa na wenzake kisimani wanafua akisema.

Wenzake wote waliokuwa wameinama wakikazana kufua waliposikia hivyo waliinuka wakasimama, huku wakiangaza macho yao huku na kule.

" Yuko wapi ?? ,, aliuliza mwingine baada ya kuwa haoni kitu.
" Si yule pale anatembea.

wote waligeuza macho yao na kufanikiwa kumuona.

" Wee adija! yule ni Said!.
" Ina maana mmemsahau mara hii!.
" Mi hata siamini, ,, Yule ni said mtoto wa bi najma pale karibu na kwa mama makame!.
" Ndie yule mnaemuona.
" Alikuwa wapi mpaka kawa vile.
" mmesahau kuwa alikuwa kenda ulaya?
" Heee Ulaya? nlikuwa sijui mie, Wallah.
" Alifaulu form six akasoma chuo akafaulu katoka hapa miaka miwili nyuma naona sasa hivi ndo karudi.

" kweli Ulaya ni ulaya tu jamani mi bado siamini kabisa kama ndie, hizo pesa za kusafiria kazitoa wapi.
" Sasa si kuna mikopo, au utajuaje kama ana ndugu zake wana pesa, hata kwa msaada wa waziri anaweza kwenda pia si msomi?.

Walifua fua mpaka walipomaliza wakiwa bado wanamdisi Seid.

" Jamani ndo itokee bahati naolewa nae mie yule mbona raha ,, alisema dada mwengine kati ya kikundi hicho cha wadada watupu waliokuwa wanafua.

" Si mpaka itokee! ,, ashindwe kutafuta wasomi wenzake wa mjini wanaojua kuoga wakatakata warembo aje kukuchukua weye kuoga kwenyewe Eid hadi Eid inahusu......

" Eti kuoga eid hadi idiii! labda weye ndo eid hadi Eid.
" Hata kama si id hadi id lakini kwa mwili huo akutaki ,, Said wa zamani sawa lakini si wa sasa, mtu kafika hadi Ulaya tena miaka, kashakuwa wa Ulaya mwenzako,, wazungu kibao anao huko watu wanaojua mahabba ,, anataka akiwa kitandani apetiwe na mikono milaini laini, ,, ya mwenzangu na mie hapa migumu kama boflo za juzi aanzie wapi kukutaka ...

Walisutana wenyewe kwa wenyewe juu ya Seid, Seid alifanikiwa kupata gari lililomfikisha maeneo ya nyumbani kwa bibi yake.

Alipokuwa anapiga hatua kuitafuta nyumba cm yake ilianza kuita ,, kuangalia ilikuwa ni Skype call kutoka kwa Christina.

" Hello beutfull ,, alipokea.
" Hello too Nimekumiss Seed.
" Na mimi pia nimekumiss mrembo wangu uko poa?
" Niko Poa vipi hali ya Tanzania.
" Huku ni vizuri tu Uingereza wanasemaje.

waliongea huku akiwa anatembea mpaka alipofika kwenye nyumba ya bibi yake kwa nje, alisimama wakaendelea kuongea hadi walipomaliza.

Alikata cm akiwa ni mwenye kutabasam, alitembea haraka haraka mpaka mlangoni akagonga hodi.

Niko Huukuuuuuu Zungukaaa!!!!

Sauti ya kizee aliisikia ikitokea kwa nyuma, moja kwa moja alijua bibi yake yuko chini ya mti mkubwa ulioko nyuma kwenye kivuli.

" Ooooooh Bibi Uyoooo!!!!

Alimshtua bibia yake baada ya kumuona, Bibi aligeuka aliposikia sauti, ,,, hakuamini macho yake kama anaemwona mbele yake ni mjukuu wake, Seid alisogea mpaka alipokuwa amekaa bibi, akapiga magoti wakakumbatiana.

" Mjukuu wangu umerudii !!

Aliuliza bibi huyo baada ya kuwa tayari wamesalimiana.

" Yah Bibi nimerudi vipi za hapa..
" Hapa! ,, Hapa salama tu mjukuu wangu.

Waliongea kwa muda mrefu mpaka usiku ulipoingia, Seid siku hiyo aliamua kulala huko huko kumfurahisha bibi yake, ilipofika asubuhi na mapema alianza safari ya kurudi kwa mama, alipita sokoni sehemu ambayo kulikuwa na vijana wenzake aliokuwa nao tokea kitambo, walisalimana wakapeana hi akawaachiamo mshiko japo wa Juis kidogo ,, huku akiwaacha katika mshangao wa kuwa hawaamini kama amebadilika kiasi hicho.

" Amy yangu acha masihara Ulaya ni Ulaya tu si unaona jamaa alivyobadilika, yani kang'aa unaweza kusema ni mwarabu....

" Mkiambiwa msome hamtaki, kwa sababu ya kusoma tu kafika hadi huko mwenzenu si mnaona mambo hayo, tulikuwa tunalia nae njaa wote hapa kijiweni lakini sasa hivi si mwenzetu tena, mwili wake wote unanukia pesa.....

" Ujue mi nlikuwa siamini ila aliponionesha picha akiwa yuko katikati ya mashabiki kwenye uwanja wa manchesta na ile katikati ya jiji la london hapo ndo nkaamini ,, jamaa si mwenzetu tena kweli huyu.

Yalikuwa ni maneno ya watu tofauti tofauti wakizungumza kuhusu Seid baada ya kuwaacha, ,, Seid alizunguka sehemu tofauti kuwasalimia vijana wenzake, wengine akiwaaga kabisa, kila aliemuona alibaki katika mshangao kwa jinsi alivyokuwa amemependeza, uzuri nao ukimzidisha kung'aa....

**********
Miaka miwili masoud akiwa katika mateso mazito ya kuishi majalalani, pamoja na baadhi ya magonjwa kumtembelea yakiwemo ,, Matende ""Uvimbe wa miguu"" ,,, pamoja na ugonjwa wa uharibifu wa ngozi.

Kuna baadhi ya watu waliokuwa wanamjua vizuri walimuona pindi anapokatisha mabara barani, lakini hawakuweza kumtambua kwa alivyokuwa amebadilika.

Tamaa za kijinga na kukiona kile alichokuwa nacho kipindi anaanza maisha kama kimepitwa na wakati baada ya kupata mali ,, ndo kilichomponza Masoud mpaka muda huo akawa anapata mateso makali ambayo hakutarajia ,, aliona dunia yote ameimiliki alipopata mali, aliona hakuna mjanja zaid yake, Miliki ya pesa aliyopewa na Mungu mara alipomaliza masomo yake akiwa katika shida ,, aliamua kuzitumia vibaya na kusahau alikotoka, kitu ambacho kimemletea matatizo makubwa.....

Kama ilivyo kuwa baada ya kupata mali, Watu wakubwa wakubwa wote walikuwa marafiki zake, Maofisi makubwa yote yalikuwa yake, viti vizuri vizuri vyote alivikalia.. ,,, ndivyo hivyo hivyo baada ya mali kumtupa mkono ,, na kuingia katika ulimwengu mwingine wa watu wasiojielewa. ,, majalala yote yalikuwa marafiki yake ,, Uchafu nao ukawa ndo swahiba yake mkuu, huku vyakula vibaya vyote visivyoandaliwa kwa ajili ya mlo vikawa ndo vyakula vyake.

Sikia tu mtoto wa flan ni chizi au jamaa flan kawa chizi, lakini omba uchizi usitembelee nyumbani kwako, Tena ulioambatana na mateso ya magonjwa, Bora uugue ukimwi utatumia dawa utadunda duniani kama kawaida, ila si kuwa Chizi, na bora uchizi wa kupewa na Mungu uenda ukapona, ila si wa masoud wa kutengenezwa na watu...

Nlitegemea kuona Masoud akitesa na mali zake huku Najma akijivunia kuwa na mwanaume msomi mwenye pesa baada ya kumvumilia katika shida, ila imekuwa kinyume chake kutokana na usahaulifu wa mwanadam ambao hufanywa na watu wengi......

******
Baada ya wiki mbili Seid alifanya harakati zote za kwenda Dar es Salam, katika jiji ambalo aliapa lazima arudi atapomaliza masomo, Aliwaaga marafiki zake wote wa karibu, rafiki yake kipenzi hamad pamoja na familia nzima ya mzee shaibu, bila kumsahau Ticha na mke wake.

" Mama naenda Dar ,, Ila nkikaa wiki moja ntarudi kuja kukuchukua, nadhani hii ni hatua ya mwisho ya ugumu wa maisha yetu.. Kesho kutwa ntakuwa ofisini kama mambo hayatoenda tofauti,  Naomba dua yako mama ili Mungu aniongoze....

Alipokuwa tayari amewaaga watu wote waweze kumuombea dua ya mafanikio, anakoenda kuanza maisha mapya ,, alirudi kwa mama yake akamwambia maneno hayo! jioni moja wakiwa jikoni wanapika huku akiwa analengwa na machozi.

Bi najma alimuangalia mwanae aliekuwa amekaa pembeni yake, aliachia mguno macho yakilengwa lengwa na machozi kutokana na moshi uliokuwepo,  aliweka vizuri chungu jikon, akaongeza kuni jikoni kisha akamwambia.....

" Hakuna mzazi anaesikia mwanae anaenda kwenye mafanikio akamuombea dua mbaya ,, moyo wangu ni mweupe juu yako babaangu , hapa hata nikifa naamini mwanangu nimekuacha sehemu salama, dua yangu nliyokuwa naiomba kila siku kilio kikubwa kikinitoka nadhani Mungu ameijibu, Nenda salama mwanangu na Nshallah Mungu atakuweka mbali na huzda za watu, macho ya watu na midomo ya watu, Ila! ,,, Naomba ujiangalie sana mwanangu, usije kuwa kama vijana wengine wanaopata mafanikio wakasahau walipotoka, una miaka 24 tu, hayo mafanikio unayotaka kuyapata ni kwa uwezo wa Mungu, Usiitaji umaarufu, wala usije ukafanya mambo ambayo aliyafanya baba yako, kwa kuwa umepata nyumba nzuri tena uanze mambo ya miziki, wanawake sijui nini utakuwa unanidhalilisha mama yako, fanya vitu vizuri na mimi roho yangu irizike, Nenda ukafanye kazi, Nenda ukaanze maisha, ukihisi huwezi kuishi peke yako naomba uje utafutiwe mwanamke, Uoe, Sawa babaangu.

" Nimekuelewa mama, Mimi ni msomi ntafanya mambo yangu kisomi, nna shahada ya mastaz kichwani, sitokuangusha mama, ntayakumbuka maneno yako siku zote ntazokuwa huko.

Mpaka chakula kilipoiva walishamaliza kuongea, waliingia ndani kula, ,, walipomaliza Bi Najma alimuomba kijana wake alale mapajani mwake, Seid alifanya hivyo huku wakiwa wanaongea mpaka usingizi ulimpitia......

Alijua ikifika kesho hatolala na mwanae tena, aliamua kuyafanya mapaja yake kuwa kitanda chake usiku huo, ikiwa ni ishara ya kuonesha kiasi gani anampenda mwanae, Wataokupenda ni wengi katika maisha ila si kama mama!, Mapenzi ya mama ni tofauti na mapenzi ya mtu yoyote duniani, Utamuona mpenzi wako ni muhimu sana kwa kuwa anakufurahisha kwenye faragha ya kimwili, Ila utakuwa kwenye giza ukisema mpenzi wangu ni zaid ya mama yangu ,, au mama yangu ni mchawi tu siwezi kumpenda kama nnavyompenda mke wangu/mme wangu,, hata ukisikia ni mchawi, mpiganie, mtetee mpaka hatua ya mwisho kwani angetaka kukuroga akakuua angekuulia mapajani kipindi anakutoa tumboni, au angekuzaa kisha akakuwekea sumu kwenye maziwa yake ukinyonya utoeke duniani, Kitendo cha kukuweka tumboni akakutumikia ndani ya miaka miwili ya kunyonya kwako, ukiwa hujui hili wala lile, huna cha kumlipa, Hata umjengee nyumba baharini au angani.....

Seid alilala kwenye mapaja ya mama yake mpaka asubuhi huku Bi najma akiwa ameegamia ukutani, ni siku aliyolala mapema kuliko siku zote lakini pia ni siku aliyoamka akiwa amechelewa kuliko siku zote.

Bi najma aliamka mapema akamuangalia mwanae namna alivyo lala, hakuitaji kumuamsha akawa anampiga piga kidogo kidogo kichwani mpaka ilipotimia saa mbili na nusu seid akaamka.

Walijuliana hali Seid akainuka kwenda kupiga mswaki, aliporudi alimuuliza mama yake.

" Ina maana mama nimelala mapajani mwako usiku mzima.

Bi najma aliachia tabasam la unyonge huku akiwa anamuwekea mwanae nguo vizuri kwenye begi.
" Ndio mwanangu ,, mbona umeuliza.

" Daah kweli mama ni mungu wa pili wa mwanadam, Yani mama usingizi nliolala leo, Wallah sijawai kuulala tokea unizae, Kwanza nimeota ndoto nzuri vibaya mno, pili nlikuwa nahisi nimelalia godoro jipya zuri wakati kila siku nalala chini, aiseee Nakupenda sana mamaangu.

Bi najma hakujibu chochote, aliendelea kumkunjia mwanae nguo, Seid akiwa pembeni anamuangalia mama yake kwa huzuni.

" Kweli mamaangu unanipenda, bado siamini kwa hali hiyo uliyonayo umenilaza mapajani mwako mpaka asubuhi, ntakuthamini siku zote za maisha yangu mama, I love you my mum....

Akiwa katika mawazo mazito moyoni, Bi najma alimpiga jicho akamuuliza ,,, " Mbona unaniangalia, unawaza nini ? ,, kabla Seid hajajibu ilisikika honi ya gari ghafla kwa nje, walishtuka wote wawili kwani walikuwa hawana taarifa yoyote ya mtu yoyote kuja na gari.....

Tukutane Sehemu ya 26 kesho mahali hapa BongoSwaggz, Share na Marafiki pia.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.