Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 24) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 24)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 24

Alishuka chini akaenda mpaka ofisini kuangalia funguo za akiba za chumba cha Seid, alizichukua baada ya kuziona akarudi na kuziingiza kwenye kitasa, lakini bado hakufanikiwa baada ya kuwemo funguo nyingine kwa ndani, alijikuta anachoka kiongozi wa darasa, aliangalia saa yake ikawa inasoma saa mbili na nusu, alitoka mbio akijua ndo muda wa kipindi, alipoingia darasani tu na Mwalim wa kipindi cha muda huo akawa anaingia bila Seid kuwemo class.

Alikuwa amezoeleka kwa ucheshi wake hasa kwenye kuuliza maswali, mwalimu alipomaliza kusomesha muda wa wanafunzi kuuliza maswali ulifika, ikawa hajatokea hata mmoja wa kuuliza, ilibidi awaangalie wanafunzi wote kisha aulize Seed yuko wapi, kwani amemzoea sana kwa usumbufu wake wa kuuliza.

" Mastar, tumejaribu kumuita chumbani kwake lakini hajaitika, hatujui ana nini leo ,, alisimama mwanafunzi mmoja wa kingereza, akasema kumwambia mwalimu.

" Mmejaribu kumuita hajaitika!? 
" ndio mastar
" Ok

Mwalimu alijibu shot kisha akatoka darasan mpaka kilipokuwa chumba cha Seid, ilikuwa inaelekea mishale ya saa nne na nusu muda huo, alifika akagonga mara ya kwanza bila mtu kuitika, akagonga kwa nguvu mpaka mara nne ndo Seid alisikia mlango wake unagongwa, aliamka kwa kukurupuka na kufungua mbio mbio huku akiwa bado amejawa na usingizi.

" Vipi kijana una tatizo? ,, Mwalimu alimuuliza seid baada ya kufungua mlango akaingia ndani, ,, Seid aliwa  katika hali ya sielewi mwili mzima ukiwa katika uchovu.

Hakuweza kujibu swali la Mwalim wake, aliangalia chini akaachia msonyo wa "mchem" akiwa anapeleka vidole vyake machoni kujifuta futa usingizi uliokuwa machoni.

" Pole sana kijana, nadhani ni uchovu ndo umekuweka katika hali hiyo, kwa sababu si kawaida yako, jiandae uende darasani ,,

Ticha mwenyewe alikuwa peace love, kumwangalia Seid tu alijua uenda ni uchovu wa siku nyingi aliokuwa nao, wapo wanafunzi waliozoeleka kuchelewa darasan au kukimbia baadhi ya vipindi lakini si Seid, alimuomba ajiandae aende darasan, huku yeye akitoka nje.

Seid alikaa kitandani akijiuliza kilichomsibu mpaka kushtuka muda huo, alijilaza chali kwa kujiangusha akienda na msemo wa "aaaah" ,,, aliangaza macho yake juu juu na kuanza kuongea na moyo wake.

" Kitu gani hiki kimenikuta leo!?, um!, ila nadhani ni penzi nlilolipata jana toka kwa Tina ,,, kwa namna hii nadhani hata kusoma kutanishinda sasa, au ni kwa sababu ndo mara yangu ya kwanza? ,,, daaaaah ngoja niende class bhna......

Alijiuliza maswali na kujijibu mwenyewe, hakuitaji kupoteza muda, aliingia bafuni akaoga, akajiandaa na kwenda darasan, maneno ya vijana tofauti tofauti yalisikika wakimshangaa seid baada ya kuingia Darasani, walimuuliza kapatwa na nini mpaka muda wote huo wakati si kawaida yake, hakuweza kumjibu hata mmoja badala yake kuwa bize kuandika kile kilichokuwa ubaoni.

Alipomaliza kuandika, alifunga book akisema "Thanks God, ,, aliwaangalia wenzake na kuwaambia " aya sasa leteni stori, huku akitoa cm yake iliyokuwa mfukoni kuangalia kama ametafutwa.

Alishangaa alipoiangalia akakuta missed call 7 pamoja na message tatu, alifungua missed call zote zilikuwa zinatoka kwa Christina, message pia nazo zote zilikuwa zinatoka kwa Tina, huku zikionekana kutumwa muda mrefu.

" Maskini weee! ,, maneno yalimtoka moyoni, alijua atakuwa amemkosea sana Tina, aliingia katika uwanja wa message akaandika text ya msamaha na kuituma haraka.

Jioni alipotoka class kama kawaida yake aliingia bustanini huku wengine wakiingia kwenye maswiming poor kwa ajili ya kuogelea wengine mpira, Tina nae alikuja sehemu alipo Seid wakakiss, wakaungana katika kusoma, walitumia dk kumi na tano kujisomea eneo alilokuwa amekaa seid, waliamia chumbani ambako mwisho wa habari seid aliitaji kurudia kamchezo alikokacheza jana.

Tina hakuweza kumkatalia, Nusu saa mbele wote walikuwa hoi kitandani, Seid aliogelea kwa mara ya pili katika penzi la mtoto wa kingereza, dunia ya mapenzi alianza kuizoea, msimu huu muda walikuwa nao wakapata fursa ya kucheza game zaid ya mara mbili.

Mwendo wa maisha ya uingereza kwa seid ukawa katika muundo huo, alikazana na masomo yake akiwa karibu na Tina.

Katika maisha ya kawaida, Seid itakuwa ngumu sana kuisahau uingereza hata kama akitoka huko, ni sehemu ambayo itakuwa ni yakukumbukwa sana katika maisha yake, ni sehemu ambayo amempata msichana aliemtoa bikra na ushamba wa mapenzi aliokuwa nao, Mapenzi yao yalizidi kuwa karibu kila kukicha, baadhi ya wanafunzi waligundua kuwa seid yuko katika mausiano na mrembo huyo wakampongeza.

Tina alikuwa ni shabiki mkubwa wa mpira hasa akifatilia kwa karibu ligi kuu ya uingereza, tem yake kubwa ilikuwa ni Man u, jumaa mosi moja ambayo Man u ilikuwa inacheza na Chelsea, Tina hakuitaji kuadisiwa game hiyo wakati uwezo wa kwenda uwanjani anao, alimuomba seid watoke jioni hiyo kwenda katika jiji la manchestar kushuhudia mtanange huo.

Walianza safari iliyokuwa imezungukwa na furaha wakitumia gari la gharama la mrembo huyo, Jiji la manchestar lilikuwa geni sana kwa Seid, alitumia muda mwingi kuangalia majengo ya kifahari na mazingira  namna yalivyo mazuri kipindi chote cha safari, walipiga stori za hapa na pale kama wapenzi, baada ya nusu saa kuanza safari walifanikiwa kufika nje ya jengo la uwanja wa old trafford.

Seid alitoka kwenye gari na kusimama, alinyanyua macho yake juu akaona bango kubwa lililokuwa linamelemeta likiwa limeandikwa "OLD TRAFFORD" ,, alishika kiuno na kuachia pumzi, Tina alisogea pembeni yake nae akaangalia alikokuwa akiangalia seid kisha akauliza.

" Nini ?

" Tina, usitake kuniambia kuwa niko kwenye ule uwanja wa mashetani wekundu ambao nauona kwenye tv kila jumaa mosi na jumaa pili kule Tanzania.

" Yah ndo huu Seed tatizo nini? ,, Pliz twende haraka mpira unaanza muda si mrefu bhana.

Walitoka eneo la nje wakaingia ndani, Seid bado alikuwa akishangaa mazingira ya maeneo, ghafla maneno yalimtoka moyoni ,,, " Ukisikia ya waswahili kuwa ukishangaa ya firauni utaona ya musa ndo haya,, Maisha ni mzunguko kwa kila binadam, Ni Seid mimi kweli ambae nlikuwa nashindia mihogo na viazi mara nalala njaa mara natukanwa leo naingia kwenye uwanja wenye hadhi kubwa duniani na kwenda kuwashuhudia wachezaji wakubwa? ,, au naota? ,,, Tina alifanikiwa kukutana na marafiki zake waliokuwa Tem pinzani, wengine wakiwa tem anayoshabikia yeye, waliingia uwanjani wakabahatika kupata ticket japo walichelewa, walienda wakatulia kwenye city huku Seid ikiwa bado haamini kama yuko ndani ya uwanja wa mpira wa manchesta, huku akiwa amezungukwa na watu weupe tupu weusi wa kuesabu.

Ghafla alijiona kwenye moja ya screen za uwanjani, aliachia meno yote 99 nje, Hazikupita dk 20 tokea kuingia kwao uwanjani wachezaji waliingia uwanjani, alijikuta akisema " Haaaaaa,, kwa kuachia mdomo wake taratibu baada ya kuwaona wachezaji wakubwa live kama Wayne Rooney, Ashlay young, Robin Van parsie Andr shurlle, Edn Hazad, Didie Drogba na wengine.

Tina alikuwa anaipenda sana clab ya machesta, hujiisi kuumwa inapofungwa na tem kubwa kama chelsea, alifatilia kwa karibu sana bila kupwesa macho yake, Ikiwa dakika ya 25 mtanange kuanza, Alishuhudia man u ikipata goli la kwanza kupitia kwa mshambuliaji robin van parsie, Ushangiliaji wake na namna watu walivyokuwa wamejazana ulimfanya apoteane na Seid.

Seid aliangalia huku na kule bila kumuona Tina, Tina nae baada ya raha ya ushangiliaji kuisha alitazama kushoto kwake alikokuwa seid bila kumuona, alipata mshangao mkubwa, ilibidi arudi nyuma kidogo kumwangalia bado hakumuona, Furaha aliyokuwa nayo iliisha ghafla na kuanza kazi ya kumtafuta Seid akiwa tayari amekunja sura yake.
___________

Hamad baada ya kukaa kwa muda mrefu Italy akiwa bize na masomo yake, alifanikiwa kupata bahati ya kupata mpenzi nae ikiwa ni kwa mara ya kwanza tokea azaliwe, Alikuwa ni mtoto wa kiarabu kutoka katika koo za falme za kiarabu Dubai, alikutana nae siku ya kwanza alipoanza chuo, wote walikuwa wanasoma class moja, walizoeana mwisho kupendana, Jioni hiyo ya jumaa mosi nao waliamua kutoka kwenda kupumzika sehemu kwa ajili ya maongezi, huku Roho ya hamad ikiwa imetulia baada ya muda mrefu kutamani kuingia kwenye mausiano ya kimapenzi na mwarabu.

Tina na Seid waliendelea kutafutana ndani ya uwanja mechi ikiendelea, mpaka zilipokamilika dakika tisini Man u ikiondoka na ushindi kwenye uwanja wake, bado Tina hakumuona Seid na kjikuta anachanganyikiwa.

Seid alipoona anamtafuta mwenzake bila kumuona aliamua kutoka mpaka nje lilipokuwa gari lao akasimama,  akijua Tina atapomaliza huko ndani lazima ataenda sehemu hiyo  ili waondoke.

" Sirias huku ndo duniani ,, Yani huku mtu kama mtu hasa ili ujulikane kuwa ni mtu ndo pakuishi, sii kule vichakani mwa dunia, ,, we mtu ukiangalia ramani ya dunia sehemu ipo pembezoni kabisa bwana ,,  aliwaza akiwa ametazama juu akikunjiana mikono yake.

Tina nae alipotafuta muda mrefu, watu wakiwa wanaisha uwanjani baada ya game kumalizika, aliona bora aende lilipo gari lake ikiwezekana ampigie cm, ndipo akamuona Seid akiwa amesimama, Alimkimbilia akamkumbatia akimpiga piga kwenye bega.

" Pliiiiz usiniache peke yangu Seed nakupenda!.. ,, alisema tina kwa sauti ya chini chini akiwa anataka kulia...

" Siwezi kukuacha peke yako Tina wangu.

waliangaliana kisha wakaingia ndani ya gari.

" Kwa nini umepotea ? ,, aliuliza tina kipindi anawasha gari tayari kwa ajili ya safari ya kurudi bweni.

" Lilipoingia goli pale, ulipoanza kushangilia kuna watu wengi walisogea kwa mbele, nkawa sijakuona tena, sasa ile tafuta tafuta nkajikuta niko wapi sijui huko nkajua leo nimeingia cha kike.

" Ina maana ulikuwa hujawai kufika maeneo haya?
" Kwanza nifate nini mimi huku, nlikuwa sijawai kabisa, nadhani na ushamba pia umeongeza nipotee.
" Hahahaaaaa acha matani basi Seed...

Alikanyaga mafuta mtoto wa kike mpaka bweni, waliingia moja kwa moja kwenye room ya Seid, siku ambayo huwa sii ya chuo hata mwanafunzi akilala kwenye room ya mwanafunzi mwingine sawa, Tina siku hiyo alilala room kwa seed ili wapeane vitu adim vizuri, kesho yake ilikuwa ni jumaa pili, waliondomorana siku hiyo mpaka wakachoka wao, Seid  ujanja ujanja wa mapenzi ulianza kumuingia.

Siku zilisonga mbele hatimae siku ya kufanya mtihani ilifika, mawasiliano yaliyokuwepo kati ya Seid na hamad ni kuviber na kuskype, Mtihani ulikuwa ni mgumu sana upande wa seid na wanafunzi wengine wengi, Seid alihakikisha achezeshi mbali mawazo zaid ya kwenye peipa ili matokeo yakitoka yawe vizuri, aweze kutimiza ndoto zake.
__________

Kila kitu kilienda vile alivyopanga Mungu, Baada ya Miaka miwili Muda wa seid kusoma ulimalizika, alibidi amuage Tina ili arudi Tanzania,  ilikuwa ni siku mbaya sana kwa Tina ambae alikuwa fall in love kwa Seid, hakuamini kama Seid anarudi Tanzania na kumuacha.

" Seed, naomba unikumbuke pliz ,, kipindi wamekumbatiana aliomba hilo tu.
" Siwezi kukusahau Tina, umenifanyia mengi sana, we ni zaid ya mpenzi kwangu, siku moja ntakukaribisha Tanzania.

Alimsindika mpaka katika uwanja wa ndege, huku akiwasiliana kwa karibu sana na Hamad ambae yeye tayari alirudi Tanzania jana ya siku hiyo, walipofika airpot Seid alipanda ndege  akaanza safari ya kurudi, akimuacha Tina katika simanzi za kuamini amempoteza mwanaume aliekuwa amempenda.

Yalipopita masaa kumi na nne Seid aliingia Tanzania akiwa katika hali ya kung'aa, kuanzia kichwa mpaka mwili wake wote tayari ulikuwa umeshiba Elimu ya shahada za p,h,d na mastaz, Bi najma hakuwa na taarifa za kurudi kwa mwanae, ilikuwa ni kama Saprize, mtu aliempokea alikuwa ni Hamad, walikutana wakakumbatiana wote wakitokwa na machozi ya furaha.

" Seid ,, Ni wewe kweli ? ,, Hamad aliuliza.
" Its Me Hamad Siamini kama tumekutana tena, Namshukuru sana Mungu.
" Dah Seid Seid Seid, kweli Mungu ni wa maajabu, nlikuwa siamini kama ni siku hii iliyopangwa kukutana tena mimi na wewe, nlikumiss sana ndugu yangu.
" Hunizidi mimi ndugu yangu, Hamad kakaaaaa ,, alimuita akimvuta tena kukumbatiana.

Hawakuitaji kupoteza muda waliingia kwenye gari kuanza safari, Seid alishangaa alipoingia kwenye gari akakutana na sura ya mtoto wa kike, alimpa hi kisha akaendelea kupiga story za hapa na pale na Hamad.

" Ndugu yangu huyu ndie shemeji yangu nini ?? ,, ulipopita ukimya mfupi wakiwa ndani ya safari ya kuelekea Kiwengwa alikokuwa anaishi Bi Najma, ndipo seid alivunja ukimya uliokuwepo kwa kumuuliza Hamad.

" Yah huyu ndo shemeji yako bhna ,, aliongea huku akicheka.

" Mashallaaah hongera sana ndugu yangu, yani hongera na Mungu atakuongoza Shem wangu vipi hali ? alimgeukia mwanadada huyo alieonekana kubeba asilia yote ya warabu wa dubai.

" Huyo bhna hajui kiswahili kaka. ,, alisema hamad.
" Haaa!  ina maana mwarabu mwarabu kweli.
" unadhani nlivyokuambia naitaji mwarabu nlitaka kufanya masiara!.
" Ilikuwaje sasa ndugu yangu.
" Stori ndefu kidogo, ila kiufupi, nlipofika Italy na kuanza masomo, nlikutana nae nkazoeana nae mwisho tukajikuta tunapendana, tulipomaliza ikanidi nibaki miezi miwili kwa ajili ya prosess zake, nlienda hadi kwao Dubai nkatoa kila kitu nkamaliza, kesho kutwa tu hapa mambo yanakuwa shwari.

" Kaka usitake kunambia kuwa unataka kuoa!.
" Alaaaaa! sasa mimi ncheleweshe nini wakati umri unaruhusu, nlikuwa nasoma mwaka mmoja tu na nusu, na huyu bibie alikuwa anasoma mwaka mmoja na nusu, tulipo maliza nkasema sikubali lazima nirudi nae Tanzania, mambo ya mahari, posa na uchafu gani sijui nshamaliza, Ijumaa ijayo ndugu zake wote wanashuka Tanzania jumaa nne Harusi.

Seid alicheka sana aliposikia hivyo ,, " We kaka ni hatari, ina maana kumbe masomo yameisha muda mrefu kabisa hadi ukafanya na mambo yote ya Kuch kuch.

" Kibaya zaid sasa ni kuwa miezi miwili mbele Tanzania hayatokuwa makazi yangu.
" aaaaaaaaaa kaka mbona unataka tutiane presha wapi tena?
" Si unakumbuka maneno yangu, siwezi kufanya kazi kwenye hii nchi wakati nna mastaz kichwani ya kufanya kazi sehemu yoyote.
" So ni wapi sasa.
" Hii ngoma ni Dubai.
" Karibu na wakwe, ndo kuna maisha yako yote!
" Yani huko ndo kutakuwa nyumbani, kampuni kubwa ishaandaliwa kwa ajili yangu, kwani wewe umepangiwa sehemu yoyote au umebahatika kupata naniliu yoyote ulipokuwa huko.

" Si kubahatika!, Nshasainisha mikataba ya kampuni moja iko huko Dar wamiliki wake ni watu wa huko huko uingereza, kwa mara ya kwanza ntaenda kukalia kiti cha ubosi ndugu yangu, hapa nakuwepo kwa wiki moja then naingia dar kuanza kazi, ,, sasa rafiki yangu mimi na wewe kukaa mbali tena mbona ngumu?

Walifika kiwengwa muda wote wakiongea wawili na kumpa ukimya mkubwa Sulaiha ambae ndo mtarajiwa wa Hamad.

" Nadhani mamaangu atakuwa ndani ,, Hamad alisema.

" Habby huku wapi ? ,, Sulaiha alivunja ukimya akauliza kwa lugha ya kiarabu.

" Huku ni kwa mama yangu mpenzi ambae ni mama wa rafiki yangu hapa.
" Ok hakuna shida.

" Aisseeee kwa hali hii kaka hapa lazima unenepe ,, Seid alidakia.

" Hahahaaaaaaa Kwa nini kaka ,, aliuliza hamad akiwa anashuka kwenye gari huku seid na sulaiha nao wakishuka.

" Yani  sauti tu na hii lugha ndugu yangu, mbona hapa raha.

walitembea mpaka mlangoni Seid akaanza kupisha hodi. Sauti ya bi najma toka ndani ilisikaka ,, " Nakuja ",,

Juu ya uzee aliokuwa nao, baada ya kufungua na kumwona mwanae yuko mbele yake,  furaha alizopata ghafla zilimfanya amfate mbio mbio Amkumbatie kwa nguvu, Machozi yafuraha yalimtoka huku nafsi yake ikionekana kurizika kurudi kwa mwanae.

Walikumbatiana ndani ya dk mbili, Alimuangalia hamad nae akamkumbatia, wa mwisho akawa sulaiha japo alikuwa hamjui, waliingia ndani wote wakionekana kuwa na furaha, Bi najma nae kiarabu kilikuwa kinapanda, ikabidi waongee kutumia lugha hiyo ili Sulaiha asije kuona kama anatengwa.

Baada ya kuongea kwa muda mrefu, Hamad pamoja na mtarajiwa wake waliaga kuondoka, Bi najma alifurahi sana, akamshukuru kwa kumletea mwanae, Hamad na mwenzie walitoka wakiwaacha seid na mama yake ndani, Bi najma bado hakuamini kama alioko mbele yake ni mwanae, aliitaji kumkumbatia tena, alimmwagia kila aina ya mabusu usoni, Seid alikaa chini akamueleza kila kitu mama yake, mwanzo wa safari mpaka kurudi kwake, mafanikio yake aliyokuwa nayo mpaka muda huo, mipango yote iliyopo ya kuanza kazi ya kuwa kiongozi wa moja ya kampuni kubwa zilizoko Dar.

" Mama angu muda si mrefu maisha yetu yanabadilika amini hilo.
" Eh! Kweli ulaya ni ulaya tu, mwanangu umeng'aa kama nyota jamani ,,
" Mama achana na hayo bhna.
" Yani hapa bado kufanya kama alivyofanya mwenzako, utafute mke uoe.
" Eh mama mapema yote hii.
" Sasa unataka kusubiri nini?

Bi najma aliandaa chakula kizuri siku hiyo kwa ajili ya mwanae, moyo wake ulikuwa umetawaliwa na furaha tupu, bado alikuwa anaona kama ni ndoto kijana wake kurudi, kila muda alimuangalia bila kummaliza, Seid alikuwa ni wa kuachia tabasam kila alipoangaliwa na mama yake.

Hamad na Sulaiha wakiwa njiani wanarudi mjini, waliendelea na mazungumzo ya furaha. Hamad cm yake ilianza kuita ambayo alikuwa nayo Sulaiha, aliingalia jina likiwa my matha, alimpatia Hamad, Hamad akaweka sikion.

" Mwanangu nakuomba ufike nyumbani haraka baba yako ameanguka ghafla.

Hamad alichanganyikiwa baada ya kusikia maneno hayo upande wa pili wa cm, Mama yake alipomaliza kuongea hivyo alikata cm, moyo ulianza kumuenda mbio kijana, alijaribu kuipiga huku Sulaiha akiuliza kuna nini, cm haikuita, alijaribu tena na tena majibu yakawa haipatikani, kijasho kilianza kumtoka, aliongeza mwendo wa gari ili afike nyumbani haraka kuangalia baba yake kapatwa na nini.

Tukutane Sehemu ya 25 kesho mahali hapa hapa. Share na Marafiki Pia.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.