Shamsa Ford: Kuna Watu Wanatabia Ngumu na Hazibadiliki - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shamsa Ford: Kuna Watu Wanatabia Ngumu na Hazibadiliki

Mwanadada Shamsa Ford ambae kila siku amekuwa akitoa ushauri kwa watu hasa wanawake wenzie kuhusu mahusiano ,amefunguka na kusema kuwa wanawake wengi wamekuwwa wakiumia kwa sababu wanajikuta wakiingia katika mahusiano na wanaume ambao tayari wanakuwa wanajua kuwa wanatabia ngumu lakini mawazo yake yote anahisi akiwa nae basi yeye atambadilisha.

"Kitu kikubwa ambacho wanawake tunajidangaya ni kuanzisha mahusiano na mwanaume ambae unajua kabisa kuwa ana tabia ngumu , huku ukijipa moyo kuwa utambadilisha na atabadilika , tabia ya mtu ni kama nguo ameshindwa kumbadilisha mama yake utambadilisha wewe".

Shamsa amekuwa akitoa maneno makali sana kwa jamii huku mengine yakienda wa jamii moja kwa moja na watu kujifunza kitu kupitia yeye huku wengine wakimsema na kupingana ane kabisa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.