Ray C Azitaka Media Zisipige Nyimbo Zake Akifa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ray C Azitaka Media Zisipige Nyimbo Zake Akifa

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amezijia juu Media za Bongo (Vyombo vya habari) huku akiwataka wasipige nyimbo zake akifa.

Ikiwa ni siku moja tangu msanii wa Bongo fleva Sam Wa Ukweli aage dunia, Ray C ametupa Dongo kwa baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikipiga nyimbo za msanii huyo tangu jana ilihali alipokuwa hai hazikupigwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ray C amesema kuna baadhi ya media zina mambo ya kibafki kwani msanii ukiwa hai hawa pogo nyimbo zako ila ukishakufa tu ndio wanaanza kupiga jambo alilolipinga na kusema yeye akifa wasipige nyimbo zake:

"Media za Bongo bwana! Kufa leo uone nyimbo zako zitapigwa wiki nzima hata zile ambazo hazijatoka studio lakini! Tusapotiane tukiwa hai pia….Nikisha kudai hata msihangaike kunipa promo….Maana hakutakuwa na maaana Tena RIP Sam”.

Msanii Sam wa Ukweli alifariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya kuugua kwa kipindi cha mwezi mzima malaria na UTI sugu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.