Nay wa Mitego Amshambulia Babu Tale Kisa Daimond na Zari - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego Amshambulia Babu Tale Kisa Daimond na Zari

Nay wa Mitego Amshambulia Babu Tale Kisa Daimond na Zari
BAADA ya hivi karibuni Meneja wa Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’; aitwaye Hamis Taletale ‘Babu Tale’ kuibukia Afrika Kusini ‘Sauz’ kwa ajili ya kumuombea msamaha msanii wake huyo kwa mzazi mwenziye, Zarinah Hassan ‘Zari’, Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amemvaa meneja huyo kwa kuchelewa kwake kuchukua hatua.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Nay alisema kitendo cha Babu Tale kwenda Sauz kumuombe msamaha Diamond ni kizuri lakini angekifanya tangu awali na kuhoji kwa nini amesubiri yeye (Nay) aoneshe nia ya kuwapatanisha wapenzi hao ndiyo akachukua wazo hilo na kulifanyia kazi.

“Suala la Babu Tale kwenda kumuombea msamaha Diamond ni zuri lakini alitakiwa afanye hivyo muda mrefu na siyo asubiri mpaka nizungumze mimi kwamba nitawapatanisha. “Nashukuru wazo langu limekubalika na kila mtu na yeye mwenyewe kuliona linafaa na kufanyia kazi.

“Diamond ni mshikaji wangu wa muda mrefu sana, japo mapenzi hayaingiliwi lakini kwa upande wangu namkubali sana mama Tee (Zari) maana akiwa naye mambo yake yanakuwa kwenye mstari kwani anakuwa mtu wa kazi sana tofauti na akiwa na hawa wanawake wengine.

“Kutokana na kuliona hilo ndiyo maana niliona nimpe ushauri kupitia ukurasa wangu wa Instagram na kuahidi kuwarudisha pamoja, lakini kabla sijafanya hivyo, Babu Tale akalifanyia kazi, siyo vibaya nimefurahi sana kwa kweli,” alisema Nay.

ILIKUWA HIVI

Awali baada ya Diamond kuachia wimbo mpya wa Iyena, Nay alimpongeza kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiweka na maneno mengine makali ya kuwaita wanawake anaokuwa nao kwenye uhusiano hawana nyota ila Zari ndiye mwenye nyota.

Baada ya kuandika hivyo na maneno mengine makali yasiyoandikika gazetini watu mbalimbali mitandaoni wamekuwa wakimwita Hamisa Mobeto ambaye pia ni mzazi mwenza na Diamond jina baya. Nay alipoulizwa kuhusiana na jina hilo alisema hakumtaja mtu bali alijiandikia kwa watu wote na hajamtuma mtu kumwita Mobeto jina au maneno aliyoandika yeye. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.