Nandy Afunguka Kuhusu Ngoma Yake ya 'Ninogeshe'. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nandy Afunguka Kuhusu Ngoma Yake ya 'Ninogeshe'.

Nandy Afunguka Kuhusu Ngoma Yake ya 'Ninogeshe'
Msanii Nandy amefunguka nini hasa anamaanisha katika wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Ninogeshe.

Muimbaji huyo katika mahojiano na 10 Over 10, Citizen TV amesema kumekuwa na maana nyingi kuhusu wimbo wake huo lakini yeye ameimba kwa ajili ya jinsia zote.

“Ninogeshe kila mtu inai-define jinsi anavyojua kuhusu kunogesha lakini kwangu mimi ni; nipende nithamini, nijali na inabeba kila kitu ndani yake,” amesema Nandy.

“Ni wimbo kwa pande zote, kwa wavulana na kwa wasichana lakini kwa sababu nimeimba mimi mwanamke ninawakilisha wanawake wenzangu,” amesisitiza.

Utakumbuka kumekuwa na utani katika mitandao ya kijamii kuwa ‘mwanaume halisi’ hapaswi kuimba wimbo huo, hata hivyo mwisho wa siku unabaki kuwa utani wa hapa na pale na muziki unachukua nafasi yake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.