Lady JayDee: Sina Mpango wa Kuolewa Hivi Karibuni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lady JayDee: Sina Mpango wa Kuolewa Hivi Karibuni

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee amefunguka na kusema watu wasitarajie kuona ndoa yake hivi karibuni maana hana mpango wa kuolewa.

Lady JayDee alifunguka hayo alipokuwa anamuongelea mpenzi wake msanii kutoka Nigeria anayejulikana kama Spicy Music, baada ya kutomposti Kwenye ukurasa wake wa Instagram tangu Tarehe 4 April.

Lady JayDee ameweka wazi kuwa yeye na Spicy Music hawajaachana kisa tu hamposti Kwenye page yake ya Instagram bali hajaona sababu ya kumuweka humo kwani kipindi anamposti sana ilikuwa ni kwa sababu ya kazi ya wimbo wao pamoja.

Lakini Kwenye mahojiano yake na Bongo5 Lady JayDee ameweka wazi kuwa pamoja na kwamba yupo Kwenye Mahusiano lakini watu wasitegemee kumuona anaolewa anytime soon:

"Watu wasitarajie kuona ndoa yangu anytime soon wasisahau kuwa sio kwamba mimi sijawahi kuolewa, au kuwa nataka sana kuolewa. Kuolewa ni jambo la kujipanga na kwa sasa siko tayari kuolewa na mtu yoyote naweza kuwa na Mahusiano na mtu lakini siko tayari kwa ndoa! Sio sasa”.

- Bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.