Karrueche Aponzwa na Chris Brown - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Karrueche Aponzwa na Chris Brown


Chris Brown na Karrueche Tran

GUNDU! Unaweza sema hivyo kwa maana nyingine baada ya mwanamitindo ambaye pia ni staa wa filamu, Karrueche Tran ‘kupigwa kibuti’ na bwana wake mpya, mchezaji wa mpira wa Kikapu, Victor Cruz huku chanzo kikidaiwa ni staa wa Pop, Chris Brown.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Victor, wawili hao si wapenzi tena na kuthibitisha hilo, juzikati katika Usiku wa Tuzo za NBA, Karrueche alitokelezea kivyake na alipoulizwa alisema;“Nipo singo.”

Chanzo kinazidi kunyetisha kuwa, Victor ameshafuta picha zote za Karrueche katika ukurasa wake wa Instagram huku sababu ya kutemana kwao ikidaiwa kuwa ni kitendo cha bi’dada huyo kumtajataja Chris Brown mara kwa mara wakati walishaachana kitambo.

Pia kwa sasa, Victor yupo Paris, Ufaransa akihudhuria shoo ya ‘Paris Fashion Week’ huku Karrueche akiwa Los Angeles akifanya promo ya bidhaa zake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.