Huyu Ndiye Star Mkubwa wa Marekani Aliyekuja Kutembea Tanzania na Mpenzi Wake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Huyu Ndiye Star Mkubwa wa Marekani Aliyekuja Kutembea Tanzania na Mpenzi Wake

Mtangazaji wa Talk show kubwa nchini marekani anayefahamika kama Ellen DeGeneres ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kipindi chake kuwa na mvuto zaidi kwa sababu ya maudhui yake yalivyokuwa yakihusisha mastaa mbalimbali, Utani na hata baadhi ya story zinazowavutia zaidi mashabiki.

Sasa Good news ni kwamba star huyo wa Marekani yupo Tanzania na hiyo imejulikana baada ya kuonekana akiwa mbuga za wanyama na mpenzi wake Portia Derossi ambaye amepost kwenye ukurasa wake wa Instagram akionesha kuwa yupo bongo na kuandika maneno haya….


”Coffee break. #tanzania @theellenshow @mlorentz23 @pjfaulstick @cliffspot @_honeybuck_” – Portia Derossi
Huwenda hii ikawa ni taarifa nzuri haswa kwenye kukuza utalii wa ndani na tukashuhudia list ya mastaa wa kubwa kuja Tanzania ikazidi kuongezeka kutokana na star huyo mkubwa ambaye ameshawai kuhoji mastaa wengine wakubwa Duniani kuja Bongo.


Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.