Harmonize Amvisha Pete Ya Uchumba Mpenzi Wake Sarah - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Harmonize Amvisha Pete Ya Uchumba Mpenzi Wake Sarah

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Kwangwaru’ Harmonize amemvalisha Pete ya uchumba mpenzi wake mwenye asili ya Italia Sarah Michelotti.

Harmonize na Sarah walikuwa kwenye mgogoro wiki chache zilizopita baada Sarah kumtuhumu mpenzi wake huyo kwa kuchepuka baada ya kuona picha zake na mtangazaji kutoka Nigeria Nancy Isime na kudai ni wapenzi.

Lakini Sarah na Harmonize walionekana kumaliza tofauti zao siku chache zilizopita baada ya kuonekana pamoja Kwenye shoo ya Kusi Night wakiwa wanakumbatiana stejini.

Hatimaye wawili hao wameweka wazi kuwa wamechumbiana baada ya Kuposti video iliyomuonyesha Harmonize akimvalisha Sarah Pete na Sarah Kuposti Kwenye ukurasa wake wa Instagram na Kuandika “Thank You Baby ♥️“.


Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.