Chid Benz Asakwa Usiku na Mchana - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chid Benz Asakwa Usiku na Mchana

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wamiliki wa Sober House Tanzania, Pilli Missanah ametangaza rasmi kumtafuta msanii maarufu Chid Benz kwa lengo la kutaka kumsaidia kutoka katika janga la utumiaji wa dawa za kulevya ili aweze kurudi katika maisha yake ya kawaida kama alivyokuwa awali.

Pilli ametangaza hilo kupitia kipindi cha eNewz inayorushwa na EATV baada ya Chid kurudi kwa mara nyingine tena kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya mpaka kufikia hatu ya kupoteza muelekeo wa maisha yake huku marafiki, ndugu na baadhi ya jamaa kuonekana kama wamemtenga kwasababu ya mambo yake.

“Mimi ndio mtu wa kwanza kumshauri Chid Benz aje Sober house, nimeshamfuatilia sana na hata sasa hivi bado naendelea kumfuatilia ili niweze kumsaidia kwasababu ni kijana bado tuna muhitaji. Kuna uwezekano mkubwa wa Chid kuacha vitu anavyo vitumia na kuwa mtu wa kawaida. Ila tatizo ni moja tu anapaswa akubali tatizo na wala asifiche fiche mambo“, amesema Pilli.

Pamoja na hayo, Pili ameendelea kwa kusema “Chid anahitaji huruma yetu sisi wala tusimnyanyapae, tusimseme vibaya wala kumnyoshea vidole. Kusaidiwa kwake ni kumchukua na kumpeleka kwenye tiba ndio msaada mkubwa anaohitaji kwa sasa. Mimi mpaka sasa hivi nimeshamuwekea ‘deffender’ mtaani yani akionekana tu akamatwe hata kwa nguvu ili wamlete kwangu”.

-EATV

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.