Betri Inayojaa Chaji Ndani ya Dakika 5 Kuanza Kuuzwa Hivi Karibuni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Betri Inayojaa Chaji Ndani ya Dakika 5 Kuanza Kuuzwa Hivi Karibuni

Betri za simu za kisasa za Smartphone ambazo zinaweza kujaa chaji katika muda wa dakika tano pekee huenda zikaanza kuuzwa sokoni mwaka ujao.

Teknolojia hiyo iliwekwa kwenye maonesho mara ya kwanza mwaka 2015 na kampuni ya Israel ya StoreDot.

Kampuni hiyo iliwasilisha kwenye maonesho ya kila mwaka ya teknolojia mpya ya CES mjini Las Vegas betri hiyo maalum iliyopewa jina FlashBattery.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Doron Myersdorf ameambia BBC kwamba sasa wanatarajia kuanza kuzalisha na kuuza betri hizo mapema mwaka 2018.

Hata hivyo, Ben Wood, mchanganuzi wa teknolojia katika kampuni ya CCS Insight amesema ana shaka kidogo kuhusu ahadi hiyo.

Bw Myersdorf amesema hawezi kufichua kwa sasa ni kampuni gani ambazo zimepata idhini ya kutengeneza betri kwa kutumia teknolojia hiyo.

Mwaka 2015, aliambia BBC kwamba betri hizo za kampuni yake zimeundwa kwa kutumia viungo ambavyo vinawezesha kufanyika kwa shughuli za kemia kwa haraka isiyo ya kawaida na pia kuhamishwa kwa nguvu za umeme kutoka sehemu moja hadi nyinginwe kwa kasi sana.

Baadhi ya miundo ya betri hizo ilikuwa kubwa kuliko betri nyingi za smartphone za wakati huo, lakini Bw Myersdorf anadai sasa wameandaa betri ambazo zinaweza kuanza kuuzwa sokoni.

"Tutachaji simu ya smartphone kwa dakika tano," alisema.

Aliongeza kwamba teknolojia hiyo tayari inafanyiwa majaribio na watengenezaji betri wawili China na kwamba utengenezaji kwa wingi wa betri hizo unatarajiwa kuanza robo ya kwanza ya 2018.

Lakini ingawa Bw Wood ana shaka kwamba betri hizo zinaweza kuuzwa haraka hivyo, amekiri kwamba iwapo betri hizo zitafanya kazi kama ilivyoahidiwa, basi utakuwa ni ufanisi mkubwa sana katika sekta hiyo.

Kubahatisha kuhusu teknolojia ya betri kunaweza kukudhuru. Nimejifunza kuwa na shaka kila wakati kuhusu ahadi hizi. Hebu tusubiri," aliambia BBC.

Alieleza kuwa muundo wowote ambao unatoa joto kwa wingi unaweza kuathiri utendakazi wa betri.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.