Aliyetoka Kimapenzi na Diamond Agawa Mahaba Kwa Mbwa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Aliyetoka Kimapenzi na Diamond Agawa Mahaba Kwa Mbwa

DAR ES SALAAM: Skendo! Video Queen maarufu Bongo, Irene Charles ‘Lynn’ ameingia kwenye skendo nzito baada ya kuachia video zake zinazomuonesha akifanya vitendo vya kimahaba na mbwa wake kama vile yupo na binadamu mwenzake, Amani linakupa habari kamili.

ILIANZA HIVI!

Lynn ambaye amewahi kutoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa anabusiwa na mbwa kwenye shavu pamoja na kumlamba na ulimi wake.

Baada ya kuweka video hiyo akionyesha ni jinsi gani anavyompenda mbwa wake kitendo ambacho kiliwakera wengi na kuanza kumtolea maneno makali kuwa anavyofanya siyo sawa na anajitafutia matatizo ya kiafya.

“Yaani hawa wasanii wa kike sijui wanakuwaga na akili gani hebu ona huyu anavyolambwa na mbwa na yeye anambusu mbwa kama vile ni binadamu mwenzake hata haoni kinyaa, hajui anaweza kupata magonjwa hatari,” aliandika mmoja wa wafuasi wake kwenye mtandao huo.

Gazeti la Amani liliingia mzigoni na kumsaka Lynn ili kujua sababu za yeye kujiachia na kugawa mahaba yake kwa mbwa kama binadamu mwenzake na alipopatikana alianza kwa kujiumauma tu na kusema ni mapenzi yake kwa mnyama huyo na haoni tatizo.

“Aaa…Kwani tatizo liko wapi? Mbona siyo shida ni kawaida maana hata mastaa wa nje ya Bongo huwa wanafanya na hawajawahi kudhurika kwa lolote, nampenda sana mbwa wangu kwa kweli.

“Kuhusu kwamba anaweza kuniambukiza magonjwa siyo rahisi kwa sababu huwa nampeleka anapewa dawa, sindano za chanjo mbalimbali za magonjwa, namuogesha vizuri hivyo hana magonjwa wala hana madhara yoyote,” alisema Lynn.


UWOYA, WEMA WANYOOSHEWA VIDOLE

Tofauti na Lynn mastaa Wema Sepetu na Irene Uwoya wamebaki kunyooshewa vidole kwani nao wamekuwa wakionyesha sana mahaba kwa mbwa walionao.

Amani liliwatafuta pia mastaa hawa ambapo walieleza kwamba wanawapenda sana mbwa wao na wako nao kwa miaka mingi na hawajawahi kudhurika kwa chochote kwani kila mwezi lazima wawapeleke kupatiwa chanjo za magonjwa.


DAKTARI AANIKA YA KUTISHA

Akizungumza na Amani, daktari maarufu jijini Dar, Dk Chale alieleza ya kutisha kuhusu binadamu anapokuwa analambwa au kubusiana na wanyama kama mbwa.

Dk Chale alisema binadamu yeyote anayejihusisha na mbwa yupo kwenye hatari ya kupata magonjwa kama ebola na mengine mengi ambayo ni ya hatari.

“Mbwa ana bakteria nyingi sana sasa mate yake tu yanapogusana na ngozi ya binadamu yanaacha maelfu ya bakteria wa magonjwa hivyo inashauriwa sana binadamu asikae au kushirikiana na mbwa kwa vyakula pia yale manyoya yake yanaambukiza magonjwa kama ya kifua yaani athma,” alisema Dk Chale.


SIRI YA MASTAA NA MBWA

Kapu la udaku limejaa habari zisizo rasmi za siri ya mastaa wengi hasa wa kike ndani na nje ya nchi kupenda mbwa hasa hao wanaofanana na midori ni kwamba mbali na urembo lakini huwatumia pia kujiridhisha kimapenzi jambo ambalo halijathibitishwa laivu na kwamba kinachoonekana kwa mastaa wapenda mbwa ni hayo mahaba yanayopita kawaida kwa wanyama hao.

Stori: Imelda Mtema, Amani. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.