AliKiba Amuonya Mbwana Samatta - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

AliKiba Amuonya Mbwana Samatta

Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, ‘Alikiba’ amemuonya  mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta kwa kumwambia kuwa atahakikisha timu yake inafanya vizuri watakapokutana Jumamosi katika mchezo maalum wa kuchangia elimu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alikiba amesema kuwa atahakikisha mpinzani wake anaondoka akiwa analia kutokana na kuchagua kikosi bora kwa ajili ya mchezo huo utakaowajumuisha wachezaji wengi wa kimataifa.

“Nitahakikisha Samatta anaondoka analia kwani kikosi changu kipo vizuri nikiwa na wachezaji wanaocheza ndani na nje ya Tanzania, tunaye Uhuru Selemani ambaye naamini kwa ushirikiano wake na wengine tutapata matokeo mazuri”, amesema Kiba.

Jumamosi, timu ya Alikiba na timu ya Samatta, zitapambana katika uwanja wa taifa ukiwa ni mchezo maalum wa kuchangia elimu. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.