Wanafunzi 6 Watumbukia Katika Shimo la Choo - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wanafunzi 6 Watumbukia Katika Shimo la Choo

Vyoo vya nje vya mashimo hutumiwa sana katika maenoe ya mashambani

Wanafunzi sita wa shule moja wa eneo la mashinani Kenya wameanguka katika shimo la choo baada ya choo hicho kuporomoka Jumatano asubuhi, vyombo vya habari nchini vinaripoti.

Leo ni siku ya kwanza ya muhula mpya katika shule ya msingi ya Kisulisuli kaika kaunti ya Nakuru mkoa wa bonde la ufa.

Taarifa zilisambaa mwendo wa saa mbili asubuhi kuwa choo katika shule hiyo kimeporomoka na wanafunzi wamezikwa ndani.

Wazazi walikimbia katika shule hiyo kwa haraka na mara moja jitihada za uokozi zilianza kwa ushirikiano wa jamii na maafisa wa uokozi.

Udongo mbichi ulifukuliwa na mawe yakavunjwa kuwafikiwa na kuwaokoa wanafunzi hao sita.

Awali idadi ya watoto waliozama haikujulikana, lakini baada ya mwalimu mkuu kuwahesabu wanafunzi wote, alithibitisha kupitia vyombo vya habari nchini kwamba wote wako salama.

Choo hicho cha nje katika shule ya msingi ya Kisulisuli kiliporomoka kufuatia mvua kubwana mafuriko ambayo yamekuwa yakishuhudiwa nchini kwa wiki nne sasa.

Uwanja wa michezo wa shuel hiyo pia umefurika.

Katika shule nyingine inayoonekana kuwa mojawapo kubwa huko Bungoma magharibi mwa Kenya, mafuriko yamesababisha vyoo 25 kuporomoka lakini hakuna aliyejeruhiwa.

Maafisa wa afya ya umma sasa wametishia kuifunga shule hiyo kwa muda kuzuia kusambaa kwa magonjwa yanayotokana na maji machafu.

Mkasa wa leo unafuatia msururu wa mikasa kama hiyo nchini Afrika kusini ambapo idara ya elimu sasa imetenga mpango maalum unaopiga marufuku vyoo vya mashimo katika shule za msingi.

Kituo kimoja cha televisheni kimemnukuu mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Kisulisuli aliyesema kuwa kati ya wanafunzi sita waliokolewa, wanne wako salama, lakini wawili walijeruhiwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.