Vyonne Chakachaka: Alikiba Namuona Kama Mtoto Wangu wa Kiume - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Vyonne Chakachaka: Alikiba Namuona Kama Mtoto Wangu wa Kiume

Mwanamuziki mkongwe kutoka Afrika ya Kusini Vyonne Chakachaka amefunguka na kuelezea ukaribu wake na msanii wa bongo Alikiba ambae kipindi cha nyuma kidogo walishawahi kuonekana kuwa pamoja wakiwa studio na kusemekana kuwa walikuwa wakitengeneza nyimbo mpya ya pamoja.

Vyonne ambae hivi sasa yupo Tanzania aliwahi kufanya mahojiano leo katika kipindi cha Clouds 360 katika Clouds Media na kuongea mengi lakini hakusita kusema kuwa Alikiba ni kama mwanae wa kiume na meneja wa Alikiba ambae ni Seven Mosha ni kama mtoto wake wa kike.

"Namuona Alikiba kama mwanangu wa kiume na meneja wake ni kama mtoto wake wa kike, ninawapenda sana watoto wangu. na katika album yangu mpya inayokuja kuna wimbo nimeimba na alikiba na tuta-perform hivi kesho kwa mara ya kwanza."

Siku ya kesho mwanamama Vyonne ataperform katika mkutano wa Africa Connect ambapo kwa mara ya kwanza wataimba wimbo wa pamoja na Alikiba kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.