Video Queen Agness Adakwa Kwa Wizi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video Queen Agness Adakwa Kwa Wizi

MUUZA sura kwenye video za Kibongo ‘Video Queen’ aliyejipatia umaarufu kwa kutupia picha za utupu mitandaoni, Agness Mmasi, yamemkuta mazito, baada ya kuswekwa rumande kwa tuhuma za utapeli Ijumaa linakumegea ishu kamili.

Akipiga stori na Ijumaa, chanzo wa kuaminika kilieleza kwamba muuza sura huyo, mpaka juzi (Jumatano), alikuwa bado akisota rumande katika Kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa takribani siku nne.

“Mnahabari kamba Agness amedakwa kisa kutapeli nguo maeneo ya Kijitonyama? Kama hamjazidaka ni kamba alichukua kwa mkopo, baadaye akawa anamzungusha mwenye mzigo, mara amtukane hapo ndipo alipodakwa na mpaka sasa anasota nyuma ya nondo,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta anayedaiwa kuwa ndiye mwenye mzigo huo wa nguo ambazo Agness alichikichia nazo, aliyefahamika kwa jina moja la Nyange na alipopatikana alikiri kutapeliwa na mwanadada huyo.

“Ni kweli alichukua mzigo wa nguo, jinsi sita zenye thamani ya shilingi 90,000. Alichukua akidai anakwenda kuzijaribu na siku iliyofuata angetoa pesa, lakini aliingia mitini. Nilipokuwa nikimtafuta baadaye alikuwa akitukana na kudai hakuna ambacho ninaweza kumfanya.

“Ndipo nilipomfungulia mashitaka kwenye Kituo cha Polisi Mabatini kwa jalada namba KJN/ RB/3851/I6L (matusi), akatafutwa na kutiwa mbaroni,” alisema Nyange.

Nyange aliongeza kuwa baada ya kumkamata ndugu wa mwanadada huyo waliomba wayamalize kwa kuzungumza namna watakavyomlipa pesa zake.

Hata hivyo mpaka gazeti hili linakwenda kitamboni Agness alikuwa nyuma ya nondo, kwa hiyo hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hili.


-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.