Steve Nyerere Afunguka Kuhusu Ishu ya Kusaliti Ndoa Yake na Kuzaa na Wellu, 'Mimi ni Mwanaume Rijali' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Steve Nyerere Afunguka Kuhusu Ishu ya Kusaliti Ndoa Yake na Kuzaa na Wellu, 'Mimi ni Mwanaume Rijali'

Steve Nyerere Afunguka Ishu ya Kusaliti Ndoa Yake na Kuzaa na Wellu Sengo....."Mimi ni Mwanaume Rijali"
Muigizaji wa filamu bongo na mchekeshaji maarufu Steven Mengere maarufu kama Steve Nyerere, amefunguka juu ya tuhuma za kusaliti ndoa yake na kuzaa na muigizaji Wellu Sengo. Kitendo ambacho kimesababisha mke wake kuondoka nyumbani.

Akizungumza na EATV, Steve Nyerere amesema kwamba yeye ni mwanaume rijali na kuzaa nje ya ndoa sio kitu cha ajabu, na mke wake wala hajaondoka kama watu wanavyodai kwenye mitandao ya kijamii

“Mke wangu yuko nyumbani, kakaa tuli katulia mtoto watu hana presha, kuna watu wangapi wamezaa nje!? Sasa mimi kwani sio mwanaume, kuna mwanaume mwenye kasoro duniani!? Labda shoga, mi ni mwanaume tena rijali, mwanaume ni yule anayeyimiza majukumu yake”, amesema Steve Nyerere.

Kutokana na hilo Steve Nyerere ametaka watu kuacha kujadili mambo yasiyo ya msingi kwenye mitandao ya kijamii na kueneza habari za uongo, na badala yake wafanye kazi kujiingizia kipato.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.