Siwezi Rudia Kumpigia Simu Mwanamke Yoyote Usiku, Yaliyonikuta Najuta - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Siwezi Rudia Kumpigia Simu Mwanamke Yoyote Usiku, Yaliyonikuta Najuta

Yaliyonikuta jana siwezi rudia kumpigia simu mwanamke yoyote usiku.

Kuna msichana nilikuwa namchukulia kama dada kwa sababu ni dada wa rafiki yangu na tumekuwa tukipigiana simu ata usiku yeye pia amekuwa akinitumia ujumbe ata usiku ikawa mazoea.

Jana usiku wa saa nne nikampigia simu nimwambie wikend njema,akapokea simu mwanaume anaongea kama watu wa Arusha.

Alivyosikia sauti ya kiume tu bila kuuliza mi ni nani alinifulumishia matusi ya nguoni sana na kuniambia yeye anaenjoy kifuani mimi naangaika kupigia simu wake za wengine.

Akanitukania mama yangu,na matusi mengine makali, nilijitahidi kumwambia siwez rudia kupiga simu sababu sikujua kama ana mwanaume. Na pia nikamwambia uyo ni kama dada yangu lakin hakunielewa .uyo rafik yangu amekuwa akiniambia yuko single hana mtu.

Siwezi rudia kumpigia simu rafik yangu yoyote wa kike usiku, mwisho itakuwa saa 12 jioni. Matusi niliyotukanwa ni makubwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.