Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 23) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 23)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 23

Alitoa bastola iliyokuwa nyuma ya surual kiunoni na kumnyooshea kwa ajili ya kumshut.....

Kabla ya kufanya chochote, Sauda Yai alikuwa amelishikilia mkononi, aliliachia mbele ya masoud likapasuka pasuka. Hapo hapo masoud mikono ilishika ganzi, hakuweza kuishika tena bastola, taratibu aliiachia, alimuangalia Sauda bila kummaliza sauda nae alimwangalia kwa hasira akiwa amefinya mdomo na macho yake.

Hali ya Masoud ilianza kubadilika, alihisi sehemu za siri zinawasha, kujaribu kushika chini ya zipu ili kujikuna tayari kitu kilisha vimba ndani.

" Nadhani hicho ndo ulichokuwa ukikitaka, Mali zako isiwe sababu ya kutuulia ndugu zetu na kuwanyanyasa wengine, Uliuchezea mtaa wa kwanza ukaweza, huu ni wa tatu huuwezi kwa round zake, hayo ni maisha yako uliojichagulia, nisamehe sana ,, Sauda aliongea akiwa anatabasam.

Masoud akili zake zilipotea ndani ya muda mfupi, uchizi ambao hakuutegemea ulimuingia gafla, alimsogelea sauda kwa ajili ya kumshika, Sauda alimkamata mkono kwa nguvu akatoka nae hadi nje ya geti kisha akamuachia.

" Nenda salama safari yako, hapa huna chako tena, kuanzia leo maisha yako yatakuwa hayo.

Masoud alianza kutembea bila kujua anaelekea wapi, akili hazikuwa zake tena, alitoa suruali baada ya kuona kama anaumia kwa ndani kutokana na mayai yake kuwa tayari yamevimba, hakufika mbali miguu nayo ilianza kuvimba taratibu, Sauda baada ya kumtupa nje alirudi ndani akajitupa kwenye sofa, alifikiria ndani ya dk tano akanyanyuka na kwenda chumbani, alifungua droo akatoa hat zote za nyumba kuziangalia kama ziko sawa, alijikuta anaachia tabasam la furaha alipokuta maneno yaliyoandika " Sauda ndie mmiliki wa nyumba hii, ,, pamoja na Saini, huku nyaraka zote alizokuwa akizimiliki masoud nazo zikiwa zimeandikwa kwa jina lake.

Alichukua cm yake ya mkononi kwa furaha, akawapigia ndugu zake na kuwaambia ashamaliza kila kitu, ndugu hawakuamini waliitaji waende kwa sauda ili waamini, walifunga safari mpaka nyumbani kwa sauda, wakiwa njiani walifanikiwa kumuona masoud akikatiza bara bara akiwa tayari ni mwehu asiejielewa, walipofika hawakuitaji kumuuliza chochote kwani walishajionea, walimpongeza huku wakifurahi kwa kuagiza vinywaji na kufanya kama sikukuu kwao siku hiyo.

Maisha yalisonga mbele Masoud akiwa tayari amepatikana, huku msemo usemao " Malipo hapa hapa duniani" ukifanya kazi kubwa wakati huo, baada ya kupitia shida nyingi akiwa anaishi na najma, kitabu kikimsaidia kuufurahia ulimwengu wa furaha ndani ya muda mrefu akiwa na maisha ya kitajiri, Hatimae anarudi kwenye umasikini wa mateso, ambao haujulikani mwisho wake, baada ya kuutumia utajiri wake vibaya na kusahau alikotoka, Aliona ashapata maisha ya milele hapa duniani, akatesa na kiungo cha mtu ndani ya mwili wake, akamsahau mwanamke aliefanya mpaka leo hii anaishi, Akamuacha Najma akiteseka na maisha ya shida, akabadilisha wanawake anavyotaka, huku najma kwa kulinda heshima kuonesha namna alivyoithamini ndoa yake akashindwa kumjua mwanaume tena wakati uwezo wa kuolewa alikuwa nao.

Hakuna aliemfahamu masoud kwa jinsi alivyobadilika ndani ya muda mfupi, Sauda alienda sehemu aliyokuwa anafanya kazi Masoud akaanza kufanya yeye kazi badala yake, baada ya miezi michache mbele alirudi dubai kwenda kumchukua mpenzi wake aliekuwa akiishi nae huko kipindi anasoma, alimleta waishi Tanzania huku wakifunga ndoa ya kifahari iliyoshuhudiwa na watu tofauti tofauti.

Waliokuwa na mapenzi juu ya masoud walishtuka hasa Ofisini, waliona miezi inakatika bila kumuona, hata kama kila kitu kimeandikwa kwa jina la mwanamke, walipojaribu kumuuliza Sauda aliwajibu kwa mkato, huku wengine wakiachana nae, waliamini ni kwa ujinga wake wa mapenzi, hivyo hawakuitaji kufatilia kiundani zaid....

Maisha ya masoud yalianza kuwa maisha ya kuishi majalalani, vyakula vyake vikawa mabaki ya vyakula vya watu vinavyotupwa, huku mavazi yake yakiwa matambara mabovu, shipa ndani liliendelea kujaa kila leo (Busha), miguu yake ilivimbiana matende, mateso makali alikuwa anayapata jamaa lakini kwa bahati nzuri akili alikuwa hana tena, afya yake ilianza kuzorota kidogo kidogo, Urijali wote ulimtoka, na kubakia mtu ili mradi mtu kwa kuwa anaishi duniani.

Baada ya miaka kadhaa, Hamad na Seid walimaliza masomo yao ya chuo, huku  Sauda akifanikiwa kuuendeleza utajiri wa mali alizozipata kupitia mikono ya Masoud akisaidiwa kwa karibu na mme wake aliejulikana kwa jina la An'war.

Ticha maisha yake yaliendelea kuwa mazuri kila siku, Mke wake Rahma alimpenda mmewe kuliko kitu chochote, hali iliyopelekea Ticha kutembelewa na ubora wa afya kila siku.

Seid pamoja na wanafunzi wengi wa chuo kikuu cha Zanzibar walifanikiwa kumaliza masomo yao, baadhi wakapata bahati za kuchaguliwa kwenda kusomea nje kwa ajili ya Digrii na kuchukua mastarz, na Miongoni mwa waliobahatika kupata bahati hiyo ni pamoja na  hamad na Seid.

Siku zilipopita mara baada ya kumaliza Chuo, Seid alimuaga mama yake kwa furaha kuelekea uingereza ambapo alipangiwa kwenda, huku hamad yeye akielekea nchini Italy, tokea waanze masomo yao hawakuwai kukaa mbali mbali ndo kwanza inatokea, Bi Najma alimpa baraka zote mwanae, Seid alikuwa wa kulia kila muda, hakufikiria siku moja kwa umasikini alionao kama angebahatika kwenda nje ya nchi tena uingereza, Siku ya safari si bi najma wala bi suria mama mzazi wa hamad wote walikuwa hoi kwa vilio, walijua watakuwa mbali na watoto wao ndani ya miaka miwili mpaka mitatu, Hamad na seid walikutana wakaagana na kupeana maneno ya kishujaa, waliingia uwanja wa ndege kwa pamoja wakatofautiana nusu saa kuondoka, alietangulia alikuwa ni hamad akipanda ndege ya Italy, Seid akafata kwa kupanda ndege inayoelekea uingereza.

Ndege zilianza kupasua mawingu juu ya anga, huku marubani wote wakionekana kuwa makini, Seid alibahatika kukaa na mdada ambae alikuwa ni mwingereza na kutengeneza nae urafiki ndani ya muda mchache, Hamad alikuwa ni mtu wa kupitia baadhi ya vitabu vya kihistoria na vitabu vingine alivyokuwa akivipenda muda wote wa safari, mpaka ndege ilipokaribia kufika mwisho akabahatika kujuana na mtoto wa kike aliejulikana kwa jina la Marcy nae akiwa anaelekea huko huko nchini italy.
_______

Baada kutumia muda mrefu wakiwa ndani ya safari, hatimae wote wawili walifanikiwa kufika salama, Hamad ilikuwa vyepesi kuwatafuta wazee wake na kuwaambia amefika kwa sababu haikuwa mara yake ya kwanza kwenda italia, Seid alipata mtihani mkubwa wa kujiuliza atafanyaje ili kumfikishia taarifa mama yake.

Uongozi wa chuo alichokuwa amepangiwa kusoma ulifika airpot kumchukua, Nembo ya shati alilokuwa amevaa ilimtambulisha kuwawekea wepesi watu waliomfata, aliingia ndani ya gari dogo leusi, akaanza safari ya kutoka uwanja wa ndege Heathrow na kuelekea sehemu yalipo mabweni ya chuo kikuu cha york, Hamad nae alitolewa airpot mpaka maeneo ya chuo kikuu cha bologna Italia.

Seid alipofika maeneo ya chuo, alishangaa sana kuona wenzetu walivyoendelea, hakuamini kama muda mchache ujaao ataanza kusomea kwenye chuo kilichojengeka kwa ustad mkubwa, mazingira ya nje tu yalimchanganya, alifika kwenye jengo la kifahari na kupatiwa chumba chake atachokuwa anakaa mpaka atapomaliza masomo yake, alitembezwa sehemu zote za maeneo ya chuo kusoma mazingira, mshangao ulizidi kwake alipoona ndani ya chuo kuna maswiming poor, Mauwanja ya michezo mbali mbali ,, tenesi, mpira wa miguu, wa kikapu, bembea, na mambo mengine, huku pembezoni kukiwa kumezungukiwa na kimsitu cha aina yake.

Bi najma alikuwa ni mtu wa maombi kila leo juu ya mwanae, mpaka inapita wiki nzima bado alikuwa hajapata kujua kama alifika salama au laa, muda ulipowadia Seid alianza masomo, darasa aliloanza nalo kusoma alibahatika kukutana na waswahili wenzake watatu ambao wao kidogo walishazoea mazingira, kwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kusoma tu si mchezo, alijiwekea utaratibu wa kukaa katika bustani za chuo pindi anapotoka darasani ili kukipitia kwa undani kile anachokisoma, mara nyingine akipenda kutembelea Maktaba kubwa ya vitabu ya chuoni hapo kwa ajili ya kuchagua baadhi ya vitabu vizito vizito na kujipa pindi "J. B. Morrell Library ambayo ndo maktaba kuu ya chuo cha york..........

" Hi

Jioni moja akiwa ametulia bustanini alipata bahati ya kupewa Hi na mtoto wa kike wa kiingereza alietokea kwa nyuma yake, aligeuka kumwangalia huku akifunga kitabu baada ya kusikia sauti ya kike.

" Hi too how are you
" I'm fine and you? 
" I'm okey too welcom
" Thanks ,, alipita na kukaa pembeni ya Seid.
" Naitwa Christina.
" Naitwa Seid.
" Nani?
" Seid ,, Seed
" ok! nimefurahi sana kukufahamu, nimeona uko peke yako wakati wenzako wako kwenye michezo, nkaona si vibaya nkisogea kukupa kampany.
" nimefurahi sana kusikia hivyo Christina, sipendelei michezo kwa sababu nimekuja huku kwa ajili ya kusoma tu.

Walizoeana ghafla wakapiga story za hapa na pale, walisoma soma baadhi ya vitabu, waliombana waingie chumbani kwa Seid au kwa Tina ili kusoma zaid, wakiwa ndani waliulizana kuhusu Relationship zao zikoje kila mmoja akajibu yuko single, Kuanzia hapo urafiki wao ukawa karibu sana, walichukua mazoea ya kutembeleana kila muda hasa wanapotoka darasani, Siku za wiki end Tina alikuwa anaamua kumtoa Seid kwenda kumtembeza baada ya kumwambia yeye uingereza ni mgeni, alimpeleka sehemu tofauti tofauti zilizomfanya Seid achanganyikiwe kuona Uingereza ilivyojenga, huku akijisikia burudani ya kuwa miongoni mwa watu walioko duniani.

Siku zilizidi kusonga mbele masomo nayo yalizidi kuwa magumu, alijaribu kukabiliana nayo ili ahakikishe anaendeleza mwendo ule ule wa kufaulu japo yuko katika nchi za watu, Hakuwa na kampani nyingine katika masomo zaid ya anayopata toka kwa Tina, alijikuta akipata furaha ya ghafla ambayo hakuitegemea, muda mwingine akiutumia kwa ajili ya kujiuliza maswali yaliyomchanganya, hasa alipofikiria uzuri wa nchi ya london namna ulivyo, na kuviona vingi ambavyo Tanzania havipo na haviwezi kuwepo.

Akiwa ameegamia dirishani chumbani kwake akitazama kwa nje na fikra kuwa mbali,  Christina aliingia bila ya yeye kuwa na habari, alimsogelea mpaka karibu akamshika kiunoni, Seid alishtuka kusikia mikono ya kike milaini inamshika kiuno, aligeuka akamkuta Tina akiwa ameachia tabasam.

" Hi
" Hi too umenishtua.

Tina hakujibu chochote, walikuwa wamesogeleana kwa karibu sana, alimuangalia seid akiwa ameliachia tabasam mwanana, aliusogeza mdomo wake na kuanza kula Romanc.

Hawakuwai kuambiana kama wanapendana, ulikuwa ni mshangao kwa seid kuona mtoto wa kike anabonyea kwake na kudendeka, nae hakujali kwani kitendo cha kushikwa kiunoni alishalegea, waliendelea kubadilishana mate huku tina akiishusha mikono yake kwenye zipu ya Seid, hakujua kama Seid hajawai kufanya mambo hayo tokea azaliwe, alitaka kumuingiza kwenye dunia ambayo si yake, mhogo wa Seid ulishasimama imara kwa ajili ya kushambulia mapigo, hazikupita dk nyingi wote walikuwa kama walivyozaliwa Kitandani, huku seid jasho likimtoka na kichwani kujaa fikra za kitendo alichokifanya.

" Asante Seed ,, Baada ya game kuisha  Tina alimshukuru Seid,  ,, nlikuwa na miezi mitatu sijafanya kitendo hiki, nliachana na mwanaume wangu kwa sababu nlikuwa simwelewi, naomba moyo wako niukabidhishe kwako.

Seid hakuwa na pingamizi juu ya hilo, penzi alilopewa tu lilishamuacha hoi, muda wa kila mmoja kuwa chumbani kwake ulifika, Tina alivaa nguo zake akamwachia Seid kiss akatoka nje, Seid alibaki ndani akiwa ameduwaa na mawazo kibao kitandani.

" hhhhmmm kumbe ni raha kiasi hiki, ,,,,, kweli nimechelewa kujua, ,,,, He lakini katoto kana mastyle hako!, ,,, Ah tina wee mbona utanifanya nizidi kupagawa sasa, sijui itakuwaje ntaporudi Tanzania ,,, no kurudi hapa mambo yenyewe haya.

Alicheka huku akiinuka kitandani, alisogea mpaka kilipokuwepo kioo akajiangalia mwili wake wote.

" Mtoto kaoza kwa hii face dadeq ,, Eti hooo Hi! mara ppu karuka mdomoni, mara Tih kaingia kitandani kumbe na mimi hand some e! hadi wazungu wananikubali nkirudi kwa washamba washamba huko si ndo nawamaliza Tumbafu, ,,,,, wanaohonga nyumba wana haki kwa hali hii, maana ni utamu utamuni.

Alijiangalia kwenye kioo ndani ya dk kumi,  baada ya kutosheka alitoka akaingia bafuni na kuoga, aliporudi akakuta cm yake inaita, kuangalia kwenye screen ni Tina.

" I love you ,, yalikuwa maneno toka upande wa pili wa cm baada ya kupokea.
" I love you too ,, Seid aliitikia akiwa kwenye tabasam.
" Good night.
" Thank you, and you too good night ,,,, nice dream.

Tina alikata cm baada ya kusikia maneno ya mwisho kutoka kwa Seid, Seid alijitupa kitandani akirusha rusha miguu huku na kule kwa furaha, hakuwai kuingia kwenye mausiano ya mapenzi zaid ya yale ya raya kabla ya kugundua kuwa ni dada yake, penzi tamu alilopata toka kwa tina lilimchanganya sana, alitamani Tina awepo muda huo warudie tena na tena, hakuitaji kusoma kitabu chochote usiku huo akihofia kukutana na kitu kikamuaribia furaha yake, badala yake alifanya maandalizi ya kulala.

Mpaka inafika saa mbili asubuhi muda wa kuingia darasani seid bado alikuwa hajaamka, wanafunzi wanaokaa eneo hilo ilibidi wamgongee huku wakijiuliza imekuwaje wakati si kawaida yake,
kundi la vijana wa kingereza lilimgongea kama mshkaji wao ili waende darasani, lakini Seid siku hiyo kwa usingizi aliokuwa nao hata kusikia hodi zao hakuweza. Wanafunzi waliingia darasan, kiongozi wa class aliuliza mbona Seed haonekani, baada ya kupewa majibu ilibidi yeye mwenyewe aende kugonga, alipofika aligonga mpaka akachoka, wasi wasi ulimuingia alipoona mtu ndani haitikii, akafikiria haraka haraka na kuona hapana! bora aende ofisini kuchukua funguo za akiba ili aje afungue mlango wa chumba chake ulioonekana kufungwa kwa ndani.

Alishuka chini akaenda mpaka ofisini kuangalia funguo za akiba za chumba cha Seid, alizichukua baada ya kuziona akarudi na kuziingiza kwenye kitasa, lakini bado hakufanikiwa baada ya kuwemo funguo nyingine kwa ndani, alijikuta anachoka kiongozi wa darasa, aliangalia saa yake ikawa inasoma saa mbili na nusu, alitoka mbio akijua ndo muda wa kipindi, alipoingia darasani tu na Mwalim wa kipindi cha muda huo akawa anaingia bila Seid kuwemo class.


Tukutane Sehemu ya 24 kesho mahali hapa, Pakua App yetu usipitwe na Uhondo. >>Bofya Hapa<<

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.