Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 22) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 22)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 22

Yu alishindwa kuvumilia tabia hiyo ya mmewe kubadilika kila siku, ikabidi aanze kufatilia nyendo zake ili ajue kwa nini mmewe amebadilika kiasi hicho......

Asubuhi  kama kawaida masoud alijiandaa kwenda kazini, alipotoka tu Yulaina nae akajiandaa kwenda kazini kwa mmewe kuangalia kama atamkuta, Bahati nzuri alipofika gari lake akalikuta limepaki mbele ya jengo la kampuni akajua yupo,  aliweka paking sehemu ambayo kuna kibustani kidogo ngumu mtu akiwa anatoka eneo la baking ya kampuni kuona, kisha akashuka na kwenda sehemu tofauti kwa ajili ya kutulia.

Haikupita nusu saa alimuona mmewe anatoka kwenye jengo la kampuni mpaka kwenye gari lake akawasha na kuanza safari, Yu nae baada ya kumuona akatoka mbio alipokuwa na kuacha kinywaji alichokuwa ameagiza akaingia ndani ya gari safari ikaanza, alihakikisha gari ya masoud iliyokuwa mbele yake kidogo haimpotei japo kulikuwa na msongamano wa magari, alilifatilia mpaka lilipofika katika nyumba moja ambayo ni ya kawaida, likaweka paking kwa nje kisha masoud akaingia ndani ya nyumba hiyo, Yu hakuwa mbali baada ya masoud kuingia ndani nae alisogea na kupaki gari lake, alishuka akasogea mpaka karibu na hiyo nyumba, alilisogelea dirisha lililokuwa pembezoni mwa mlango kusikiliza kama atasikia chochote lakini hakubahatika, akakaa kaa nje ya nyumba akijiuliza afanye nini, ndipo alichukua uamuzi wa kufungua mlango kuingia ndani.

Hakuweza kuvumilia baada ya kumuona mmewe akiwa amekaliwa uchi uchi akipata penzi kutoka kwa mwanamke  mwingine, alitoa macho ya mshangao akiwa ameshikilia mlango akaanguka chini na kupoteza fahamu....

" Jamani! huyu mwanamke kafikaje huku?  ,, Masoud aliongea akiwa katika mshangao mkubwa baada ya kumtupa pembeni Samira.
" Beib, kwani nani huyu ? ,, Samira aliuliza akivuta khanga yake iliyokuwa pembeni kujifunika.
" Si ndo yule kikaragosi nlokuambia naishi nae nyumbani!...

Samira alishtuka kidogo alipojua kuwa ndie mkewe, Hakukuwa na chakupeana mapenzi tena, walisogeza feni karibu ili limpepee apate hewa, kisha wakakaa kwenye sofa, masoud akiwa na wasi wasi kibao.

" Beb itakuwaje sasa hapa ? ,, aliuliza  Samira akiwa anataka kuvaa nguo zake kabisa akijua hapatoshi tena.
" Yani sijui wanawake wengine wakoje kiukweli, mtu unamfata hadi kwenye starehe bhna ,,,, Usivae mamaa ngoja aamke nimtimue tuendelee na ya kwetu, mtoto unavitu vitamu mpaka napagawa yani usivae kabisaa kipenzi changu.

" Um beib si ntauliwa mimi.
" Wewe ndo switty wangu bhna sii huyu, hata wewe ukimuwahi unaweza kumuua vile vile..

Yulaina alishtuka akaamka, alimuangalia sana mme wake bila kuongea chochote, alisimama machozi yakiwa yanataka kutoka.

" Naomba twende nyumbani masoud, ,, alisema baada ya kusimama akiwa bado anaskilizia maumivu.

" Umekuja peke yako, fungua mlango uende mimi nakuja ,, Alijibu akiwa anaangalia chini.
" Mme wangu, naomba twende nyumbani please nakuomba masoud.
" Na mimi please nielewe mwanamke, tangulia nakuja.

" Yani mme wangu nimekufumania bado unanijibu kijeuri namna hiyo kwa nini lakini!.
" Unatoka utoki ?

Masoud aliamua kutumia ukali kidogo alipoona mtu anaambiwa kistarabu haelewi, aliinuka alikokuwa amekaa na kumwambia atoke mara tatu, Yu bado alikuwa haamini kama ni mmewe aliemfumania na anamtoa kinguvu, alisema kwa sauti ya juu kumwambia atoke bila kutoka, alinyanyua mkono na kumtia makofi Yu huku akimsukuma nje.

Yulaina alianguka kwa nje baada ya kusukumwa, alinyanyuka chini kabla ya watu hawajaamuona, palikuwa karibu na njia, akaenda mpaka kwenye gari lake akawasha na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwake akiwa tayari amepata kujua kwa nini mmewe amebadilika.

Ilipofika saa mbili na nusu usiku, Masoud ndo alienda nyumbani kwake, Yulaina muda huo tayari alikuwa ashalala, alipofika hakuongea chochote, alivua nguo zake akaingia bafuni kuoga, alipomaliza alirudi kitandani akalala.

Maisha ya Yulaina tokea siku hiyo yakawa maisha ya kuonewa kila siku, alivumilia kwa sababu alimpenda sana Masoud, kuna muda alimkalisha chini akimuomba abadilike lakini hakuna alichoambulia zaid ya kipigo, Mkono wa shetani wa kupiga ulihamia kwake, bila kujua hilo tatizo la kupigwa pigwa litaisha lini.

Ukali kila siku kwake ulizidi, kila kukicha ilikuwa bora ya jana, Yulaina alikuwa katika nyumba nzuri lakini alianza kupukutika mwili wake, Mpaka siku hiyo Masoud alipoamua kufanya kitendo kama ambacho  alichokifanya kwa Bi najma cha kumletea mwanamke ndani.

Baada ya miaka zaid ya mitano ndani ya mateso huku Raya akiwa tayari na umri wa miaka 15, ufahamu wa kila kitu anao.
Masoud aliamua kumleta mwanamke ndani ya nyumba hiyo aliokuwa akiishi Yulaina mbali na Samira.

" Karibu Sana Fetty, jisikie uko nyumbani sawa mamaa, hapa ni kwako, cha mmeo ni chako bhanaaa au vipi heheheeee ,, alimkaribisha mwanamke huyo sebleni, ilikuwa ni kama picha rejea kwa bi najma, baada ya kukaa na mwanamke wake seblen bila kutokea mtu yoyote, alimuita Yulaina, yulaina alikuwa mbali kidogo lakini alisikia, alienda mpaka sebleni akashangaa baada ya kukutana na sura ya mtoto wa kike akiwa amekaa karibu na mme wake kwa kukaribiana.

" Ammmmm! Yulaina, huyu anaitwa Fetty si mbaya ukimuita Fatma, Nimemleta aishi hapa na ndo mke wangu kipenzi huyu, kama hutojali, endelea kuishi hapa lakini kama house garl kwa sababu huyu ndo mama mwenye nyumba kuanzia leo, sahau kuhusu mimi na wala mimi sio mmeo, talaka zote tatu nshakuacha ,,,,, na na nafanya hivyo, ili usije kusema hoo masoud kanifukuza mie, Mara vile mara hivi staki, Ishi hapa ila kama msichana wa kazi utapoona umechoka utaondoka mwenyewe kwa hiari yako.

Yulaina alihisi kama ametwishwa mlima wenye kila aina ya mawe kichwani kwake, Raya alikuwa pembeni akiangalia picha yote huku mchozi yakimtoka, Yu alitoka akaenda mpaka jikoni, presha ilikuwa inapanda na kushuka muda huo, hakukuwa na joto lakini mwili mzima ulishawa na jasho kwa wasi wasi, alichukua kisu na kurudi nacho seblen akiwa amekiweka nyuma, alipunguza presha na kumwambia Masoud huku akisogea karibu walipokuwa wamekaa.

" Nashkuru sana Masoud, Nashkuru, nadhani huu ni mshahara wa dhambi kwa nlilotenda kwa mwanamke mwenzangu, Ila hiki hapa kitakufanya unikumbuke maisha yako yote masoud, na hii ni kama trela, nkiondoka yapo yatayokukuta siku moja na kukufanya umkumbuke Najma, pia utajua mimi nlikuwa si mwanamke wa kuchezewa kiasi hicho.

alipoongea hayo alikuwa karibu na miguu ya masoud, alimwangalia mwanamke aliekuja na mme wake akatoa kisu kwa nyuma na kumchomeka cha tumbo huku akiwa bado analia presha juu juu, bado hakurizika alitoa na kuchomeka tena akakizungusha ndani kwa ndani kuukata kata utumbo wote, alipomaliza nae akajichoma cha tumbo akitumia ujasiri ambao hakuwa nao.

Alianguka chini, Raya akamkimbilia mama yake huku akimuita, Masoud muda wote hakujua afanye nini na kubaki akiwa ameshangaa, kitendo alichofanya Yu kilimpagawisha, kicheko alichokuwa akicheka kiligeuka kilio, hakuwa na jinsi zaid ya kupiga cm police na hospitali, ndani ya muda mchache gari la wagonjwa lilifika haraka likawachukua wote wawili na kuwapeleka hispitalini, Yulaina alifanikiwa kufika akiwa mzima Fatma alifia njiani, huku masoud akipelekwa ndani kama egesho mpaka pale uchunguzi utapoisha.
********

Sauda aliangua kilio kisicho cha kawaida baada ya kujua mambo yote aliyofanyiwa dada yake, uso wote ulichafuka kwa machozi, macho yalishakuwa mekundu, Luninga ilitoeka ukutani aliangalia pembeni dada yake hakumuona, alitikisa kichwa akijiuliza afanye nini!, Masoud alishtuka ghafla na kumkuta sauda analia, aliuliza vipi sauda hakujibu kitu, alinyanyuka kitandani kwa hasira akafungua mlango na kwenda kulala chumba cha pili, hakuitaji kumuona masoud hata machoni mwake kwa mambo aliyoyafanya kwa Yulaina....
*******

Kwenye maisha  siku zote kuna mambo matatu muhimu sana kwa mwanadam yoyote, hayatimii mpaka utumie akili kuyatimiza, ukiyaendea papara kwa tamaa zako basi hakika dunia utaiona chungu. Kuna kitu kinaitwa bahati duniani, wasemi wa mambo wakapata kusema " Bahati haiji mara mbili, na ikija mara mbili basi ile ya pili si kama ya mwanzo, huku mshairi akisema, " Ukiona Jiwe la karatani limekaa mahala pake, Basi usiliondoe Ili kuepuka matatizo, Usidhani utavyofanya kwa wa kwanza akakubali, basi na wengine watakubali hivyo hivyo laa, Wengine wana utata wao ambao wataitaji kuutumia ili kukupa fundisho... Sijui Masoud aliwaza nini kumuacha Bi Najma baada ya kupata mali.

Asubuhi palipokucha, Baadhi ya watu waliondoka makwao, wakiwa tayari wamemaliza siku tatu za kuomboleza msibani, ndugu nao waliokuwa wakikaa mbali waliaga na kuondoka, huku kundi lote la ndugu upande wa Sauda nalo likiondoka na kumuachia kazi moja tu Sauda.

Sauda hasira alizokuwa nazo usiku hasa baada ya kushuhudia mambo aliyofanyiwa Yulaina zilishaanza kuisha ilipofika asubuhi, mawazo ya kulifikiria jambo lililomtokea usiku yalimuingia kila mara, chuki ndani ya moyo wake zilishaingia juu ya Masoud, alihisi moyo wake kuunyima furaha endapo atamuacha masoud salama.

baada ya siku tano kupita, Sauda alimuomba masouda amruhusu aende kwao mara moja akiwa na nia aruhusiwe ili aende kwa babu alikoelekezwa na dada yake, Masoud alimruhusu akiwa hajui nia ya mke wake huyo, sauda alianza safari, akitembelea gari lake binafsi, alifika kwa mtaalam aliekuwa anapatikana Daraja bovu, akiwa na lengo moja tu la kuhakikisha anamtengeneza masoud ikiwa kama kisasi.

" Karibuni sana Bint ,, mtaalam alimkaribisha Sauda baada ya kufika.
" Asante.

Walisalimiana na kujuliana hali, waliongea mawili matatu ili kufahamiana, mwisho Sauda akaingiza jambo lake lilimpeleka.

" Heheheeeee Binti, kwa nini unaamua kufanya hivyo ,, aliuliza mtaalam.
" Kwa sababu kamtendea unyama mtu muhimu sana katika maisha yangu, Kiasi chochote kile niko tayari kukupatia naomba unisaidie.
" Ok sawa, nimekuelewa, Laki tano zipo ?
" Ndio zipo ,, Sauda alijibu haraka haraka bila kuchelewesha.
" Unataka tumfanyeje.
" Ikiwezekana awe Chizi au umpige shipa tu aaibike, vikishindikana vyote, awe chini ya imaya yangu.
" Basi mimi ntavifanya vyote kwa pamoja.
" Nimefurahi sana kusikia hivyo mtaalam.

Baada ya kufanya mambo yake.

" Nakupatia hili yai binti liangalie vizuri, ,,,, Hili yai, unatakiwa ukalivunje mbele ya miguu yake, Tena inabidi umwambie kabisa, flan umenifanyia hivi na hivi mimi ni flan imekuwa kadhaa kadhaa kadhaa, na mimi naamua kukufanya hivi kwa sababu nna maumivu, ndipo unaliangusha hili yai chini, hapo hapo hali yake itabadilika.

Sauda aliachia tabasam huku akisema asante sana, alifungua mkoba wake akatoa kitita cha laki tano akampatia mtaalam.
" Hapana Siitaji pesa yako, nenda kwanza dawa itapofanya kazi ndo utaileta.
" No Mtaalam mimi nakuamini asilimia mia pokea tafadhali.

Mtaalam alipokea, Sauda akatoka akaanza safari ya kurudi. Alitumia muda wa dk 40 kutoka daraja bovu mpaka alikokuwa anaishi mazizini.

" Leo nadhani utaijua vizuri hii familia uliokuwa unataka kuichezea ,, aliongea akiwa anashuka kwenye gari tayari kwa kuingia ndani.

Alipofungua mlango akamkuta masoud akiwa amekaa sebleni anaangalia baadhi ya habari, alisimama karibu na mlangoni akamuangalia, kisha akatembea mpaka ilipokuwa tv akaizima akiwa amekunja uso wake.

" Mbona umezima sasa wakati naangalia taarifa muhimu ,, Masoud alimuuliza sauda akiwa amekaza sura.

" Nadhani hizi unazoziangalia hazina umuhimu kama hii nnayotaka kukupatia sasa hivi hapa.

" Hazina umuhimu kama unazotaka kunipatia sasa hivi, Zipi?

" Masoud,,, Nakupa pole sana, ,,na nakusikitikia sana ,, aliongea kwa sauti ya kupanda na kushuka,, Juzi tumetoka kumzika Raya, ulikuwa ukiniuliza siku zote kwa nini nalia sana juu ya Raya wakati si mwanangu, Sasa basi! ukweli ni kuwa, Mimi na Raya ,, mtu na mama yake mdogo.

Alishangaa sana Masoud kusikia hivyo, macho yalimtoka kumwangalia Sauda.

" Nadhani Yulaina aliwahi kukuambia kuhusu Lubna, ndie mimi hapa mbele yako, kwa ajili ya dadaangu tu, nkatoka lubna hadi kuwa Sauda.

Mapigo ya Moyo yalianza kwenda mbio kama mtu anaefukuzwa kwa ajili ya kuuawa, kijasho chembamba kilimnyemelea kusikia habari ambazo aliona kama maajabu kwake.

" Nlikuwa naumia sana ulivyokuwa unamtesa Raya, nlijaribu kuweka hasira zangu pembeni ili nifanikishe kile nlichokuwa nakiitaji, Nashkuru kwa mapenzi yangu tu nlokuwa nakuonesha, ukanipatia hat zote za nyumba, Mikataba yote ya kiofisi, na nyaraka zote unazozimiliki.
Nlikubali kulala na mwanaume alielala na dadaangu, nkamsaliti habiby wangu, kutokana na kumweshim sana dadaangu, Masoud tokea unioe sijawai kukupenda hata Kidogo, na sijawai kupata raha yoyote ndani ya mapenzi yako.
Nlikuwa ndani ya game nkishirikiana kwa karibu na ndugu zangu bila wewe kujua, na huu nadhani ndo mwisho wake, kisa umepewa mali ukaona umnyanyase kila mmoja, kwetu huwezi Masoud, Ukoo uliokuwa umeingia ni wa watukufu, ila una roho chafu zaid ya shetani pindi unapoweka uibilisi wako,  Yu alipoondoka alikwambia hii ni trela yapo yatayokukuta ntapoondoka, na hili ndo kubwa linalotaka kukukuta kwa sasa.

Sauda machozi yalishaanza kumtoka, Masoud bado alikuwa anaona kama utani mambo anayoambiwa, alimuangalia Sauda bila kummaliza huku akimsikiliza kwa makini.

Naomba nikuambie kitu kilichofanyika baada ya Yulaina kupelekwa hospital kabla ya kupoteza maisha yake, kisha mwisho wa habari utajua kwa nini nasema hivi.

Dadaangu alipofika hospital, alimuomba docta achukue cm iliyokuwa mfukoni mwake na atupigie ndugu zake, Mimi ndo nlikuwa nimetoka Dubai masomoni, Tulikuwa tunajiandaa kuja kwako ghafla cm ikaingia ndipo tulikimbia haraka mpaka hospitalini.

Tulimkuta yuko katika hatua za mwisho za uhai wake, nlikuwa na miaka nane sijamwona dadaangu nliumia sana kumuona akiwa katika hatua za kuchukuliwa roho wakati nna kiu kikubwa cha kuongea nae, alinyanyua kinywa akasema mbele ya ndugu zangu wote ,," Mimi nakufa ila aliesababisha ni Masoud, kanipatia mateso ambayo hakuniahidi, akavunja mapenzi aliyokuwa amenambia atanipa ,, yaliniuma sana maneno hayo masoud yaliniumaa, ,, Alinishika usoni akiashiria kuniita nami nkamuitikia akanambia " Lubna mdogo wangu we ni msichana mzuri sana, Naitaji uwe karibu na masoud bila kujua kama wewe ni ndugu yangu ili umwangalie Raya mpaka atapomaliza masomo, nadhani wewe ndo umemaliza kila kitu sasa hivi, then akikuitaji kukuoa, kubali usikatae, ukiwa ndani ya ndoa uweze kummaliza, kumpatia maumivu kama aliyoipatia familia yangu, endapo ataitaji mambo ya wazazi sema mimi yatima sina ndugu ,, Baada ya kuongea hayo hakuweza kuongea lengine na hiyo ndo ikawa kauli yake ya mwisho, nliita dada dada lakini wapi, Mazishi yalifanyika, ndani ya muda mfupi tukaweka kikao na kulipanga hili familia nzima, nlijaribu kuwa nawe kwa bahati nzuri kweli ukaitaji kunioa, ukanioa nkakubali kumsaliti Habiby wangu alioko Dubai kwa ajili ya kulipiza kisasi cha dada, Mimi sio mtu mwema kwako masoud, Nisamehe....

Sauda machozi yalishaloanisha paji lake la uso, Masoud yote aliyoambiwa hakuyajali, alisimama alikokuwa amekaa na kumfata taratibu Sauda huku akikunja mikono ya shart.

" Nlizani naishi na mtu kumbe naishi na chui mkubwa si ndio! ,, asante sana kwa kujirudi ukanambia kila kitu, kama ulitumwa ukashindwa kufanya kile ulichotumwa, ngoja nikuoneshe kuwa mimi ni mtu wa aina gani, Nadhani sasa utamfata huyo malaya mwenzako pamoja na hilo litoto lako kuzimu.

Alitoa bastola iliyokuwa nyuma ya surual kiunoni na kumnyooshea kwa ajili ya kumshut........

Tukutane sehemu sehemu ya 23 kwenye Uhondo zaidi. Tunaomba usiache kuwashirikiesha marafiki stori hii nao wasome, Bofya Share Ili kuwatumia washkaji pia.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.