Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 20) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 20)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM

Sehemu ya 20

Alifumba macho akanyoosha kisu kwa mikono miwili, mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio lakini hakuitaji kuogopa ili atimize kile anachotaka kufanya.

" One ,,, Two ,,, Threee !!!!!!.......

Baada ya kuesabu mpaka tatu alijichomeka kisu cha tumbo, macho ya mshtuko yalimtoka mdomo aliuacha wazi, alipiga kiukelele cha chini chini huku akiiangalia picha ya mama yake.
Akiwa katika malue lue ya kuishiwa nguvu, aliiona kama sura ya mama yake inamjia mbele kwa mbele, aliiangalia nguvu zikiwa zinamuishia.

' Mwanangu!, kwa nini umezifupisha ndoto zako kwa ubaya wa mwanadam? ,, Hujafanya vizuri kuvumilia kipindi chote na kushindwa mwishoni. zilikuwa fikra za Raya baada ya kumuona mama yake akajua anatamkiwa maneno hayo, alifumba macho akaanguka chini na kupoteza maisha kisu kikiwa bado kiko tumboni.

**********
Hamad baada ya kufika nyumbani, alisalimiana na Mama yake aliemkuta sebleni kisha akaingia chumbani kwake, alivua nguo akavaa tauro na kuingia bafuni kwa ajili ya kuoga, alipomaliza akajiegesha kitandani huku akitafuta namba ya raya kwenye cm ampigie kumuuliza kama amefika salama au laa!..
Cm iliita lakini haikupokelewa, akaipiga tena na tena bado haikupokelewa, ikabidi ampigie Seid ili kumuuliza kama ameongea nae.

" Ndugu yangu vipi umeongea na Raya?
" Hapana sijaongea nae.
" Naona nampigia hapokei cm.
" Labda atakuwa amelala kutokana na uchovu ebu ngoja nijaribu mimi.
" Sawa hamna shida.

Walizungumza ndani ya dakika moja baada ya seid kupokea kisha wakakata huku wakitakiana usiku mwema, Seid alijaribu kuipiga cm ya Raya bila kufanikiwa kupokelewa, akarudisha majibu kwa rafiki yake kupitia ujumbe wa message ,, Hata yangu hajapokea sijui kwa nini ila nadhani atakuwa kalala ,, .....

*******
Soud na mkewe sauda wakiwa sebleni, walishtuka kupita masaa matatu bila mtoto wao kutoka hata ndani wakati si kawaida yake hata akipigwa, Sauda ilibidi aende mpaka kwenye mlango wa chumba cha raya, aligonga bila mtu kuitika, alirudi seblen na kumwambia mmewe kajifungia ndani.

" Muache mpumbavu huyo mtoto, namuuliza kwa nini naona hauko sawa ananijibu kijeuri navitaka mimi hivyo? ,, kama amejifunza jeuri muache ashibe jeuri yake, ikimuisha njaa ikamkamata atakuja.

" Ila mme wangu umezidi kuwa mkali kwa mtoto, mpaka anakuwa hana Amani jamani, yani nizae wangu umkoromee hivyo weeeee ntachokufanya hutosahau.

Soud alimgeukia sauda baada ya kuongea hivyo.
" Una semaje wee mwanamke?
" hivyo hivyo kwani umesikije? na ungekuwa unajua nnavyoumia soud unavyompiga mtoto wa dad .......... alishindwa kumalizia anachotaka kuongea.

" Ntakugeukia na wewe nikufumue au hunijui vizuri.
" Eti ntakugeukia na wewe nikufumue! Eeheeee! thubutu yakooo, ukinichoka nirudi nyumbani kupigwa sijazoea babu upo? hujaniokota jalalani kwetu kupo na napendwa kama hujui. Sauda alimjibu masoud bila woga, alijua kiasi gani amemteka akili hawezi kunyanyua mkono wake kumpiga.

Masoud aliendelea kumwangalia Sauda kwa hasira, aliona akiendelea kuwa mbele yake anaweza kumtia makofi kweli kwani tayari mikono yake imezoea kupiga piga, alinyanyuka na glass yake akaingia chumbani.

Baada ya kuwa tayari kaingia ndani, Sauda alicheka sana akiwa macho juu, mikono pembeni nayo ikiwa juu juu.

" Eti ntakugeukia na wewe, nyooo! hao hao babu si mimi, historia yako yote na wewe mwenyewe nimekuweka Hapa huruki wala ukimbii, kwa wote ulipita kwangu umefika, tena sasa umenasa kubaya maana si mahala pake ,, Tena Shuttuuu babu namuwaza An'war wangu sii wewe, mtoto mdogo kama mimi nikutake zee wewe vijana wameisha au ,, mwanaume una roo mbaya kama nini mtoto karudi na uchovu wake unampiga tu, mama yake ukamuua huyo mwengine ukamtimua unadhani na mie utaniweza ! Thubutuuuuu,, kwanza nakuchelewesha tu hapa na wewe uishimo ishimo! lakini nimekuweka Happa! kiganjani......

aliongea chini chini akiwa anaonekana kufurahi kwa kile alichokisema Masoud, alinyanyuka akaingia chumbani alikokuwa mmewe, alimkuta amelala akamvua nguo kisha nae akajiegesha pembeni yake, Usiku tayari ulishaingia walijiandaa kwa ajili ya kulala. Sauda akiwa amelala pembeni ya masoud mawazo yalimpeleka mbali sana, akaiangalia pete yake iliyokuwa mkono wa kushoto akaibusu huku akionekana kuwa na maumivu makubwa moyoni ....

' Nakukumbuka Sana mme wangu, imenibidi niolewe tu bila mwenyewe kutaka ili kulipiza kisasi juu ya dadaangu, pia kukusaidia wewe, Najua una hali ngumu sana huko uliko ila nistahamilie ndani ya muda mfupi tu ntamuangamiza huyu mtu, ili niishi na wewe An'war, Hakika we ndo kiapo changu An'war, I love you..

aliongea moyoni akiwa anaiangalia pete yake iliyoonekana kuwa ya uchumba mbali na aliyovishwa na masoud, masoud tayari alishasinzia muda huo, machozi yalianza kumtoka taratibu, Kumbu kumbu zilimpeleka mbali tena akayakumbuka maneno ya mtu mwingine muhimu sana katika maisha yake ambae hayuko duniani.

' Mdogo wangu bora umerudi, Sijui kama ntapona kutokana na hii hali nliyonayo, Ila nakuomba uhakikishe unajiingiza kwenye umiliki wa masoud kumlinda mwanangu bila masoud mwenyewe  kujua , wapo ndugu zangu wengi anaowajua  lakini wewe hakujui, alikuwa anasikia tu nna mdogo wangu anaitwa Lubna, Siwezi kuishi tena mimi Lubna na aliesababisha ni masoud, naomba ubadilishe jina uingie mikononi mwake ili kulipiza kisasi juu yangu, ikiwezekana kubali kuolewa nae ili kummaliza kiakili zaid, we ni mzuri sana lubna, we ni mzuri, nakuomba mdogo wangu.

Baada ya kuyakumbuka maneno haya aliiamka na kukaa kitandani, alimuangalia sana masoud kwa jicho la husda, ,, Sijui nikumalizee, nimeishi na wewe miaka miwili sasa kama mke na mme, japo tulijuana muda mrefu nkiwa karibu nawe ili kumwangalia Raya, ndani ya miaka miwili hiyo, nashkuru umenipatia Hat ya nyumba, na nimesaini kwenye makampuni na bank zote ulizowekeza,  nlijaribu kuiteka akili yako juu yangu ili nipate kila kitu, nimeishi na mwanangu bila yeye mwenyewe kujua kama mimi ni mama yake mdogo, Nadhani huu ndo mwisho wako mjinga wewe ,, Raya tayari ashakuwa, na najua akimaliza kusoma ataenda kuishi nje. aliongea na moyo wake Sauda, akaona kwa muda huo hakuna kinachowezekana bado, ikabidi ageukie upande wa pili kulala.

Asubuhi ya siku ya pili ilikuwa ni jumaa pili masoud alikuwa haendi kazini, wakiwa mezani wanapata Chai, Sauda alimuuliza Masoud kuhusu Raya, masoud alijibu kwa mkato akiwa bado amekazania jeuri yake, sauda alishindwa kuvumilia akainuka na kwenda mpaka kwenye mlango wa chumba cha Raya, aligonga bila kuitikiwa, akaugonga mlango kwa nguvu lakini wapi, akajaribu kuchungulia kwenye kitundu cha kitasa, hakuona chochote funguo ilikuwa imezuia, alirudi kwenye meza ya chakula akiwa hana raha tena, kila alipomuangalia masoud hana wasi wasi.

" Hivi mme wangu! we una uchungu na mtoto kweli? ,, tokea jana jioni mtoto chumbani hatoki, usiku hatujala nae, chai bado hatumuoni bado huna wasi wasi tu.

" Ebu kaa chini hapo tunywe chai yeye si jeuri? ,, masoud alijibu kwa mkato.

" Mme wangu ebu kuwa na roo ya uruma basi jamanii, mwanao yule kumbukaa lakini, wa kuchukulia poa alikuwa ni mimi kwa sababu mtoto mwenyewe haniusu zaid ya kunifanya niumie nnapoona mme wangu alizaa na mwanamke mwingine wakati mi sijazaa, inakuwaje mimi naumia wewe mwenye mtoto huumii lakini.
" Mi mwenyewe nashangaaa wewe unaumia kwa nini wakati mwanamke mwingine angekuwa anafurahi hapo ,, yule mtoto mimi namjua kajifunza ujeuri, ebu kaa chini hapo usisumbue akili yako, ule vinono mwanamke uzidi kupendeza bhna ,,,

Masoud alimuangalia sauda huku akitabasam, umri kidogo ulishaenda lakini alijikuta anafurahi kumiliki mwanamke mzuri mdogo mdogo, sauda alikuwa hana amani tena, Alikaa kwenye kiti wasi wasi kibao, chai haikunyweka, alishahisi kitu tofauti kwa Raya.
" Sijui huyu mwanaume yukojeee!!!, si Mtanzania nini huyu, Muonee! ,, aliongea  akiwa amempiga jicho la kuvimbisha mdomo moyoni mwake.

" Yani sauda nnavyokupenda wewe mwanamke basi tu, nimeishi na wewe miaka miwili lakini sina dalili hata ya kukuchoka, mtoto unang'aa tu kwenye nyumba ulikuwa wapi miaka yote ? ,,  na huo unene sasa yani umeendana na Mama raya Yulaina akyamungu.....

Sauda alivyoambiwa mama raya tu aliachia msonyo akainuka kwenye kiti akaenda ndani....

" Tatizo la huyu mwanamke sasa nsimtaje Yulaina ,, Sasa yule si alishapita maamaa, sasa hivi si ni wewee kipenzii changuu !!!? ,,,, Aaah hawa wanawake bhna yani anamuonea wivu hadi mwanamke ambae sinae tena, tena sasa alishajifia zamani jamaniii.... ,, aliongea Masoud akionekana kufurahi huku akipiga chapati yai na chai ya nguvu.

Sauda alipoingia ndani alifungua begi lake, kati kati ya moja ya nguo zake akatoa picha ya kijana mwenye asili ya kiarabu, alimuangalia machozi yakiwa yanataka kumtoka, akaisogeza mdomoni akaachia kiss kwenye paji la uso, kiss lililokuwa limeambatana na maneno ,," I love You An'war, Miaka miwili nimekaa mbali na wewe, ila naamini bado unanisubiri, I love you my Switty, mwaa!

aliirudisha haraka akiogopa masoud kuingia ndani, alifunga beg akalirudisha mahala pake akarudi sebleni.

" Vipi hasira zimeisha? ,, aliuliza masoud baada ya Sauda kufika kwenye kiti na kukaa...

Sauda hakujibu kitu, alinyanyuka tena akaingia jikoni ili kuchukua vifaa vya maandalizi ya chakula cha mchana,
Alichukua mazaga zaga yote, vitunguu, nyanya, mchele, na vingine ,, akachukua na baadhi ya vyombo ambavyo alienda navyo mpaka kwenye meza ya chakula.

" Umeleta tusaidiane? ,, masoud aliuliza alipoona mazaga zaga yote pamoja na vyombo vinaletwa mezani.
" Sii tusaidiane, leo zamu yako kuandaa mimi ntapika tena ngoja nkalete kisu.

aligeuka huku sehemu za nyuma akizitingisha, masoud aliangalia mke wake anavyofanya shuguli ndani kwa ndani, akatingisha kichwa " nna haki ya kukupatia hat zote za nyuma na pesa zote zilizoko acount, Mtoto ukitembea tu unaa unaa unanikosha hadi uti wa mgongo!.

Sauda alitafuta kisu bila kufanikiwa kukiona, aliangalia sehemu zote za vyombo bila kukiona, ndipo ghafla alishtuka akaingiwa mawazo " Isije kuwa Raya ndo kakichukua na kujifanya anachojua yeye.

Moyo wote uliripuka, alirudi mbio mbio mpaka alipokuwa masoud.
" Mme wangu naomba twende tukamgongee Raya ,, aliongea akionekana kuchanganyikiwa flan.
" Kuna nini kwani?
" A a mimi sijui ila nna wasi wasi twende Masoud nakuomba, Yuuuuuuuuh!!! Jamani raya naomba isije kuwa kweli ntamjibu nini mimi D....... ,, alichanganyikiwa na kutaka kusema dada, ghafla akawa kama mtu asiejielewa.
" Utamjibu nini D ndo nini mbona sikuelewi ghafla we mwanamke.
" Mme wangu twende usiwe mbishi, Kisu sikioni jikoni nna wasi wasi atakuwa kakichukua raya twende mme wanguu.

Masoud alipoambiwa hivyo ilibidi ainuke, walienda mpaka kwenye mlango wa chumba cha raya, waliita Raya raya kimya, wakaita tena kimyaa, na tena kimyaa.

Ndipo Sauda akamuomba mmewe wavunje mlango, walitafuta chuma kilichokuwa jikoni na kuanza kuuvunja mlango ili waangalie raya kama yupo au laa, wakiwa bado hawajui kuwa raya kafa zamani...

*********
Hamad na Seid upande wao walishachanganyikiwa, hawakuwasiliana na mwenzao tokea jana jioni, kila walipoipiga cm yake iliita bila kupokelewa, Wakahisi uenda kuna tatizo, Hamad alimuomba Seid atoke shamba aje mjini haraka ikiwezekana waongozane hadi anapoishi Raya wakaangalie inakuwaje kuwaje, huku akimuomba asimwambie chochote mama yake na wala asimwambie kama kila wakimpigia Raya cm hapokei. Seid alimuaga mama yake haraka ili aende mjini.

" Mwanangu mbona hutulii weyee siku hizi? kila siku mjini mjini mjini, tokea upajue mjini imekuwa kero, jana tu si umetoka safari weye, au sie,, aliongea bi najma baada ya seid kuaga kwenda mjini.
" naomba uniruhusu mamaangu kuna kitu cha muhimu naenda kukifatilia pliiz. ,,, Aliruhusiwa na kuianza safari ya kwenda mjini haraka...

Masoud aliendelea kuhangaika kuvunja mlango wa chumba alichokuwemo raya, haikuwa kazi ndogo kutokana na uhimara wake, Sauda pembeni alikuwa tumbo joto japo bado alikuwa hana asilimia mia za raya kujifanya kitu kibaya, ila picha iliyokuwa mbele, Kisu hakionekani na raya hajatoka ndani aliogopa.

" Mbona unaonekana kuumia sana mke wangu kuna ajenda gani! ,, Masoud alimuuliza sauda alipoona kachanganyikiwa kuliko hata yeye mwenye mtoto.
" Bhna vunja hukoo mtoto naishi nae kila siku alafu iwe ghafla tu unadhani ntajisikiaje kama mwanamke? ,, alijibu hivyo huku ndani ya moyo wake akisema ' Na ole wako nikute kajifanya kitu kibaya nakuuwa Masoud, akyamungu lazima nikufanye kitu ambacho hutosahau katika maisha yako.

Jasho lilikuwa linawatoka wote wawili, masoud alirudi nyuma kidogo kisha akasukuma mlango kwa nguvu, ndipo ukafunguka akaingia nao mpaka ndani.
Sauda hakujali kuanguka kwa mmewe na mlango, alipita moja kwa moja hadi ndani.

Pozi zote zilimuishia alipomuona Raya akiwa amejichomeka kisu, alitoa macho akaweka mikono mdomoni na kujiachia  " Haaaaaa! ,, Ooh God God God God God God ,, kilio kilianza huku akisema God god god mpaka kilipokolea,  alimsogelea Raya akamshika kichwani, Masoud nae akiwa haamini anachokiona pale.

Taratibu machozi ya kiume yalimdondoka, Sauda aliangua kilio kama mtoto mdogo, Masoud alimfata mpaka alipokuwa amechuchumaa, akamshika begani ili amuinue juu, Sauda alimjibu " Niacheee" kwa sauti ya kulia.

" Mke wangu ebu usiwe hivyo basi, mi mwenyewe najisikia vibaya lakini lishatokea hilo unadhani wote tukisema tukae tuanze kulia kitafata nini?

Sauda alisimama mbio mbio, akabinya macho yale na kumwangalia Masoud.

' Ulikuwa hunijui Masoud, Dadaangu amekufa kwa ajili ya mambo yako ya kipumbavu, mwanangu anakufa kwa ajili ya upumbavu wako pia, Ulivifanya kwa hao!, hapa ndo mwisho wako ,,, Mimi ni Lubna nlifundishwa wai kumuangamiza adui yako kabla ya kukuangamiza, Una siku chache tu za kuishi ukiwa Salama duniani.

aliongea na moyo wake sauda akiwa anamuangalia masoud kwa jicho chafu, Masoudi hakuweza kuongea chochote muda wote alioangaliwa, alitoa cm mfukoni akapiga kwa police ambao huwa anawaamini sana na anajuana nao ili waje haraka kwenye tukio
Askari walifika eneo husika ndani ya dakika kumi na tano, Walipima kila kitu ndani, wakabeba maiti na kuipakia kwenye gari kwenda kuifanyia uchunguzi, huku akipiga tena cm kwa ndugu zake kutangaza msiba wa mtoto wake.

Kutokana na umaarufu aliokuwa nao Masoud, ndani ya nusu saa nyumba yake iliyokuwa eneo la mazizini tayari ilishajaa watu baada ya kupeleka mawasiliano ya haraka, ndugu kutoka sehemu tofauti tofauti za karibu na mbali walishafika, Sauda muda wote alikuwa ni mtu wa kulia, Masoud alipiga cm upande wa ndugu za yulaina mwanamke aliezaa nae raya, nao wafike, bila kuelewa ndio wazazi wa Sauda, huku wengi wakijiuliza mbona imetokea ghafla.

Bibi yake Raya ambae ni mama mzazi wa Yulaina na Sauda alifika eneo husika akiwa analia, akamuita sauda pembeni ambako hakukuwa na watu.

" Naomba unambie uzuuuuuuri kimetokea nini mpaka mjukuu wangu amekufa? Aliulizwa sauda.
" Mama, Raya ametoka safarini akiwa amechoka masoud ndo akampiga kisa kamjibu shot, tunakuja kushtuka kesho yake kafatiki.
" Ina maana na mjukuu wangu tena huyo huyo masoud ndo kasababisha.
" Ndio mamaaa , ,, alijibu machozi yakiwa yanambubujika.
" Hivi anaitafuta nini famili yangu huyu mwanaume lakini, Je ashafahamu kuwa kuna mchezo unachezeka nyuma yake na kujua chochote kati yako na Yulaina?
" Hajajua kitu mama na nshafanikiwa kuchukua kila kitu.

" Basi ngoja msiba uishe alafu tumfundishe dunia huyu baba asituletee mchezo hata kidogo mpuuzi mkubwa, Alikuja kwetu kumposa mtoto wetu vizuri mwisho akamuua sasa tunataka kumuonesha kuwa sisi ni watu wa dizaini gani asituchezee kabisaaa sawa mamaa!...
" Sawa mama.

Walimaliza kuongea wakaongozana mpaka walipokuwa wakina mama pamoja na baadhi ya ndugu, Muda huo huo Gari nyeusi ilikuwa inaingia katika geti la nyumba ya masoud, ndani ikiwa imewabeba Seid na Hamad.

TUKUTANE SEHEMU 21 Kesho Mahali Hapa Hapa, Pakua App Yetu Uwe Karibu na Uhondo >>Bofya Hapa<< KuDownload/Update.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.