Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 19) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 19)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM.

Sehemu ya 19

Mawazo yalipita akilini mwake baada ya kumuona dada wa watu alivyofungasha nyuma,  Honi za mfurulizo za gari aina ya fuso  zilipiga gafla, Zilipekea kila raia aliekuwa eneo hilo kugeuka,  kabla ya seid kuonekana kuvuka lilipita alipokuwa amesimama kwa kasi, na kumuacha kila mtu katika swali la kitendawili cha mshangao, huku watu wakishikilia midomo yao wengine " Mungu wangu " kwa  kile wanachokiona.

Wengi waliokuwa roho  juu juu wakihofia kijana wa watu kugongwa, walishusha presha zao baada ya kumuona Seid upande wa pili wa bara bara nae kijasho kikiwa kinamtoka, moyo wake ulikuwa unaenda mbio akiwa bado haamini kama amenusurika,wale waliokuwa na roho ndogo walianza kumshushia matusi huku wakisema Mshamba wa wapi!, Hamad alimuangalia sana rafiki yake akitingisha kichwa, Raya nae akiwa haamini kama kaka yake amekoswa.

" Ndugu yangu dar es salam hii we wakuja nini? ,,, alisikika jamaa mmoja aliemsogelea seid.
" Washamba wengine msiwaletege mjini, ni kutafuta kesi tu ,,, dada mmoja alisikika anasema huku akiwa anatembea.

Alitukanwa kila aina ya tusi na vichaa waliokuwa eneo hilo, Hamad alimshika mkono wakaanza kutoka wakielekea sehemu nyingine, walifika eneo la paking ya Tax, wakasimama huku wakiongea na dereva tax waliemkuta, baada ya kuelewana waliingia ndani ya gari wakaanza safari ya kuelekea ubungo.

" Ndugu yangu ulikuwa unawaza nini? ujue kila mmoja haamini kama umenusurika. ,, Hamad alimuuliza rafiki yake.
" Kiukweli hata mimi bado siamini kama amepona ,, kabla ya seid kujibu Raya alidakia.
" Mimi mwenyewe mnaponiona hapa sijui nimekoswaje koswaje kiukweli.
" Ulikuwa unawaza nini sasa jamaa yangu?.
" Hamad we acha tu, usione kila anaetembea ukajua yuko duniani, wengine tulishajifia zamani ,, mimi nlikuwa navuka bara bara lakini nlikuwa tayari niko mbali kimawazo.
" mawazo ya nini !!? ,,, Raya aliuliza.
" Yani sijui mawazo ya  nini ila nlikuwa sijielewi.

Alishindwa kuwaambia kitu kilicho mpumbaza mpaka akawa katika mawazo tofauti na kujisahau kama anavuka bara bara ,, mpaka wanafika ubungo bado walikuwa  wanamdisi yeye, walimpatia dereva pesa yake ambayo ilikuwa 15000.. walipokuwa wanashuka wapiga debe wawili wa magari ya mkoani walifika wakaanza kuwauliza wapi wanaenda.
" Sisi tunaenda Kilimanjaro tunaitaji xpress ,, hamad alisema.
" Twende haraka ofisini sasa hivi inaondoka!, twendeni ,, leteni mabegi niwabebeeni, fanyeni chap chap gari liko moja tu na bado dakika tano kuondoka.

Walipelekeshwa mbio mbio mpaka ofisini
" Amanda kata ticket tatu haraka haraka uwapatie hawa jamaa ,, alisema mpiga debe baada ya kuingia na wakina hamad ofisini.
" Pesa ? ,, Amanda msichana aliekuwa na ticket aliuliza.

" Sh ngapi ?? Hamad aliuliza haraka haraka kijasho cha kutembezwa mchaka mchaka kikiwa kinamtoka.

" Lete elfu 75 ,, mpiga debe.

Hamad alitoa noti nyekundu nane wakamrudishia Elf 5,  walipatiwa ticket tatu wakabeba mabegi yao ambayo hayakuwa makubwa sana, wakaongozana na mpiga debe mpaka kwenye gari linaloelekea mkoani kilimanjaro.

Walipoingia ndani ya gari, sity tatu tu ndo zilikuwa zimebakia, mbili zilikuwa mbele na moja iko nyuma, Hamad na raya waliwai wakakaa sity mbili za mbele kisha seid akaelekea kwa nyuma akiongozwa na moja ya wahusika wa gari.
" Wewe itabidi ukae hapa ,, Aliambiwa Seid.

Alipatwa mshangao kidogo baada ya kuona pale anapotaka kukaa kuna msichana mzuri amekaa sity ya dirishani aitwae Nancy akiwa amepigilia miwani, sura yake ilivyokuwa pamoja na umbo bila hata kuuliza ulijua huyu ni mtoto wa kichaga, Nancy alimuangalia Seid ndani ya miwani, Seid hakujali akawa amekaa.
" Sorry Anko naomba uje ukae upande huu huku wa dirishani sipawezi nna mafua, nlikaa tu kwa sababu sity nliona hazijajaa!.

Sauti tu ilimfanya Seid asiweke coment nyingine, nancy alipoinuka macho ya seid yaligonga moja kwa moja kwenye makalio.

Moyo wote uliripuka baada ya kuona mtoto alivyojazia, aliinuka akasogea sity ya dirishani kumpisha nancy akae sehemu aliyokuwa amekaa yeye.

" Asante ,, nancy alishukuru baada ya kupishwa 
" Ok Usijali, unaitwa nani? alipoambiwa asante akaona ni chansi nzuri ya kumuliza hata jina.
" Naitwa Nancy
" Ok nimefurahi kukufahamu.

Safari ya kutoka ubungo ilianza, ukimya kwa abiria wote ndani ya basi ulitanda, Kutokana na kasi ya gari Tangazo la abiria wote kufunga mikanda lilipita, kila mmoja akakazana kufunga mkanda uliokuwa pembeni ya sity yake, huku gari likianza kukata mawimbi ya bara bara baada ya kuwa tayari limepita kwenye foleni za ubungo......

Seid muda wote hakuacha kupiga jicho mara moja moja kumuangalia Nancy, jinsi alivyokuwa amependeza akichanganya na uzuri aliokuwa nao alijikuta anachanganyikiwa.

" Ukiwa na mwanamke kama huyu ndani hata kufa ukumbuki akyamungu tena!! ,,, mwanamke mzuri mpaka kero jamani ,,, Kuna sehemu ambazo ukizaliwamo ni burudani tu, si zanzibar masaa 48 wee unaona mishungi tuuuuu! mambo mazuri haya hapa ,,,, Sijui huku hakuna wanawake wabayaaa maana sijawaona mie, kila nnae mwona sura chuma,  mwili huo, akiwa mwembamba mwembamba wa kichuna si znz viwanawake vyembamba vya mnyooko bhna.....

mawazo mazito yalimchukua Seid,  kifundo cha mkono alikiweka dirishani huku akishikilia tama, alishtuliwa na sauti ya nancy akimpatia apple
" Asante sana ,, alipokea tunda alilopewa na kuanza kula.

" Na wewe unaelekea Kilimanjaro? ,, seid aliona avunje ukimya.
" Yah naenda kilimanjaro.
" Ok mi pia naenda huko kwa ajili ya kutembea tu kama siku tano hivi then nageuza.
" ok sawa unatokea wapi?
" Natokea Zanzibar.
" ni mtu wa huko huko?
" Ndio wewe je!
" Mimi ni mchaga ila naishi Dar nasoma.
" Wao chuo au.
" Yap nimepata kirikizo kidogo ndo nkaona niende kukilia nyumbani.
" Basi nimefurahi sana kukufahamu kwa sababu hata mimi bado niko chuo, nimeongozana na wenzangu wako mbele hapo, tunaenda kwa ajili ya mambo ya histori kuhusu mlima.
" Kuupanda sio.
" Yah na kuchukua mambo flan flan hivi si unajua ukiwa unapiga kitabu.
" Kweli ni vizuri.

Walizoeana ndani ya muda mfupi, wote walikuwa ni waongeaji wazuri, Walijuzana na kuulizana mengi, waliifanya safari yao iwe ni nyepesi kwa stori tofauti tofauti za hapa na pale, nancy hakuamini kama amepata kampany ambayo hakuitegemea ndani ya basi, mlima wa kilimanjaro alikuwa anaujua vizuri, alimpatia mawili matatu kama somo seid kuhusu mlima ili hata akifika sehemu ambayo kunapatikana watu wa kuwaongoza na kuambiwa baadhi ya vitu asivioni vigeni, Masaa yalizidi kukatika,  Safari ilisonga mbele, ukimya mkubwa ukiwa umetanda ndani ya basi, mlio wa gari na honi tu ndo vilisikika, ,,, Saa tisa na dakika kumi wakawa ndo wanaingia katika stend kuu ya kilimanjaro.

Kwa kuwa tayari walikuwa wameunda kama urafiki ndani ya muda mfupi, walipatiana namba za cm, huku kila mmoja akisema atamtafuta mwenzake.
Gari liliweka paking abiria walianza kushuka, Seid alifika chini akaungana na wenzake, wakatembea huku wakiwa wameongozana na dereva tax.
" E bhna sisi tunaelekea sehemu ulipo mlima kilimanjaro. ,, hamad aliongea akiwa anamuangalia dereva tax aliejulikana kwa jina la Mgabe.
" Ok msijali ntawapeleka ila ni mbali sana, kutoka hapa hadi huko ni kilometa 40 mpaka 45.
" Ina maana ni nje kidogo ya hapa sio.
" yah yah kwa sababu ni mpakani mpakani.

Walielewana bei safari ya mwendo kasi ili kuuwahi usiku ilianza ,,, walitumia masaa mawili na nusu kufika eneo la hotel hotel za kulala watu wote ambao wanakuwa wanajiandaa na safari ya kwenda mlimani.
kwa kuwa usiku ulishaingia ilibidi walipie vyumba viwili hotelin kwa ajili ya kulala, hawakuwa na muda wa kupoteza kutokana na uchovu wa safari waliokuwa nao, waliingia kwenye kirestaurant kidogo kilichokuwa eneo hilo, wakapata Dina kisha wakaingia vyumbani kupumzika.

*******
Asubuhi na mapema seid na mwenzake waliamka wakaenda kumgongea Raya chumbani kwake, Raya nae alikuwa tayari ashajiandaa kwa kila kitu, aliungana nao wakapita mapokezi kurudisha funguo, wakatoka nje ambako walikutana na mtu wa kuwaongoza hadi sehemu ambazo kuna watu maalum wa kuongozana nao mlimani.
Baada ya nusu saa tayari walikuwa katika ofisi za waongozaji watalii, walifanya prosess zote zilizotakiwa, wakapatiwa watu watatu ili kuwaongoza kwelekea huko.

" Hivi huu mlima bosi unapandika kweli hadi juuu au ni egesha tu za watu? ,, Hamad aliuliza akiwa ndani ya gari lililokiwa linaendeshwa na moja ya waongozaji tayari kwa ajili ya safari.

" Chalii yangu huu mlima unapandika vizuri tu hadi juu, na kuna njia sita za kuupanda ili kufika juu kabisa, tano zote ngumu ila moja ndo nyepesi ya kupitia lango la marangu.
" Na inachukua siku ngapi.
" Siku sita, tatu kupanda na mapumziko kwa ujumla nne, mbili kushuka.

" Sasa huku ndo tunaenda kufiako kabisa ,, Seid aliongea na kuwafanya wacheke ,, msicheke, we safari ya wiki nzima kwa kutembea si ni kufa huko huko, wengine miguu yetu hapa ilishajiozea zamani.

" Hiyo njia nyepesi wengi wanaitumia sio ?  hamad aliuliza tena.
" Yah ndo njia ambayo mtu wa kwanza kabisa kuupanda mlima huu aliitumia.
" Basi na sisi tupitishe huko huko, ,, una urefu wa mita ngapi?  ,, Hamad tena.

" Huu mlima unaaa mita 5, 895 na futi 19, 340
" Duuuuuh! ila poa, Hayo ndo mambo muhimu sana sisi kuyajua.

Walifika eneo la kununua nunua vitu, Hamad akanunua camera, baada ya kutembea muda mrefu kidogo ndani ya gari, waliingia kwenye lango la marangu ambapo walishuka na kuanza kutembea kwa miguu.

Ilikuwa ni safari nzuri kwao, walipata kujenga urafiki na watu wengi ambao ni wageni, Wafaransa na wajerumani walimkoma hamad kutokana na yeye kuzungumza vizuri hizo lugha mbili , Raya akipata kampani nzuri kutoka kwa watoto wa kike watatu wa kihindi aliokutana nao na kujuana nao, huku Seid nae akipata kampani ya kuongea na watu tofauti tofauti wakiwemo warabu.

Ulipofika usiku tayari walishajikongoja hadi kufika mandara camp ambapo ndo hatua ya kwanza, Walifika eneo la mahema kupumzika ili kesho kwendelea na safari, huku wakipata kuwashuhudia wanyama mbali mbali wakiwemo nyati na ndege.

Kipindi Seid ametulia hemani alijawa na kumbu kumbu nzito za kumkumbuka nancy, msichana aliekutana nae kwenye gari. " Kiukweli Mungu ulijua kuumba, yani yule mtoto namna alivyo mzuri Dah,, Sijui huku kama netwek inashika nimpigie japo sm, nijifanye kumuuliza kama amefika salama.

Mawazo yake yalivyompeleka ndivyo alivyofanya, aliipiga cm bahati nzuri ikapatikana ,, Nancy alipokea wakaongea kama dakika tatu kisha akamtakia usiku mwema. Alijikuta anafurahi sana kuisikia sauti ya mwanamke aliehisi ni mzuri hakuna mfano wake kati ya aliowaona, Aliachia pumzi ndefu kidogo akageuka na kuanza kuutafuta usingizi.

Ilipofika asubuhi na mapema safari ilianza upya, wakiwa zaid ya watu 40 walielekea Maundi Creta, Hamad akiwa na camera yake kuchukua kila kitu anachokiona mbele yake, muda mwingine akiitumia kupiga picha akiwa yuko na watu wa nchi za kigeni.
Safari ilikuwa ndefu sana ikiwa imeambatana na mapumzi mafupi, ulipoingia usiku walirudi tena mandara kwa ajili ya kulala, siku iliyofuata walielekea sorombo ambako walilala huko huko, wakapata mapumziko mpaka saa sita usiku, wakaanza kupanda kuelekea kilele cha mawenzi, walifika sehemu na kukiona bila kufika kileleni kwenyewe  kutokana na palivyo, walipita kibo mwisho wao na kuanza safari ya kurudi wakiwa tayari wametumia siku tano.

Kwa jinsi walivyokuwa wamechoka hamad aliona hakuna umuhimu wa kutumia usafiri wa basi wakati wa kurudi Zanzibar, ikabidi atumie gharama nyingine kubwa kidogo kwa ajili ya kulipia usafiri wa anga ili watumie muda mfupi kufika. Kila mmoja alionekana kuchoka kwa safari, huku Raya akilalamika miguu yake iko hoi, walipofika Z,bar Karume airpot, kila mmoja alichukua tax kuelekea kwao, hawakuitaji kupoteza muda wa kuanzisha mazungumzo mengine tena wakati kila mmoja kachoka kivyake.

Raya alipofika nyumbani alimkuta baba yake akiwa tayari amerudi safari zake, alimuangalia akamsilimia pamoja na mama yake mdogo kisha akaingia chumbani kwake. Hakuwa na mapenzi kama aliyokuwa nayo mwanzo juu ya baba, moyoni ilishaingia chuki baada ya kugundua baadhi ya vitu kupitia kwa Bi najma, ambavyo alivifanya. ,," Kumbe babaangu ana roho mbaya kiasi hicho,, nlizani nimeyashuhudia kwa mama tuu, kumbe kafanya makubwa ya kinyama huko nyuma,,  Kama aliweza kukataa mimba ya mwanamke alieishi nae ndani akamvumilia kila aina ya shida, si anaweza kuniua hata mimi?  ,,Alizongwa na mawazo baada ya kuingia chumbani na kulala kitandani, aliwaza mengi sana mpaka akataman kuondoka kuliko kuishi na baba aliefanya unyama kwa mwanamke anaeonekana mkarimu na mpole.

" Mbona anaonekana hayuko sawa mwanangu ,, Soud alimuuliza mke wake, wakiwa wamekaa kwenye sofa sebleni.
" Labda atakuwa amechoka si unajua mambo ya safari, tena mikoani huko.
" Ebu ngoja niende kumwangalia kwanza,, Soudy aliinuka kwenye sofa na kwenda mpaka kwenye mlango wa chumba cha binti yake, aligonga hodi raya akafungua haraka. aliingia chumbani kwa binti yake akakaa kwenye kiti.

" Mbona unaonekana hauko sawa ,, alimuuliza mwanae.
" Kivipi? ,, raya nae aliuliza.
" Nakuuliza na wewe unaniuliza ndo nini?
" kwa sababu mimi naona niko sawa kisha wewe unasema siko sawa.
" Ok umerudiiii ,, ukanikuta baba yako niko nimekaa ukasalimia juu juu na kuingia ndani ndo nini?
" Basi tu nimeona nifanye hivyo.
Alijibu kwa mkato akiwa amesimama mlangoni. Japo alijibu hivyo ila alijishtukia kwa sababu baba yake alimjua vizuri, dakika mbili mbele.

" Basi tu,, yani unajibu unavyotaka ndo ulivyofundishwa huko ulikokuwa umeenda kuwa baba yako akikuuliza hivi jibu hivi si ndio, soud aliuliza akionekana kusikopendezeshwa na jibu la mwanae. Raya alikaa kimya baada ya kuulizwa, soud alikuwa kwenye miaka 42 ila nguvu bado alikuwa nazo, aliinuka kwenye kiti akiwa tofauti, Raya alimuangalia baba yake akajua tayari pamekucha, woga ulimuingia huku moyoni akisema " Ukinigusa kwa ajili ya kunipiga tu sikubali leo, nshachoka, umeniulia mama yangu kwa mambo yako, ukamtesa mamkubwa na mimi pia!?.

" Rudia kile ulichokisema! ,, soud alimsogelea mpaka alipokuwa amesimama akamuuliza, ilikuwa ni kawaida yake kila anapokosea kidogo tu basi humpatia kipigo, japo alishafikisha miaka 21 lakini aliishi ki dicteta, ,,Raya hakujibu kitu huku mwili tayari ukiwa unatetemeka, soud alimuangalia mwanae akamvuta kwa nguvu huku akisema " Si naongea na wewe? rudia kile ulichokisema ,, Raya bado alikuwa kimya ndipo alipoanza kubamizwa makofi huku akiambiwa " Siku nyingine nsije kukuuliza ukanijibu unavyotaka wewe, unasikia?.

Alipomaliza alitoka chumbani akiwa amekunja sura, Raya alilia kama mtoto mdogo akiwa amekaa chini mpaka kilio cha kwikwi cha kimya kimya, aliangalia ukutani na kuiona picha ya mama yake, aliinuka mbio mbio akiwa anatoa machozi akafungua mlango na kwenda mpaka jikoni, alipekura kwenye vyombo akaona kisu, alichokichukua kisha akarudi tena chumbani kwake, alifunga mlango kwa ndani kisha akasogea mpaka karibu na ilipo picha ya mama yake ,, aliiangalia machozi yakiwa yanambubujikaa akalalamika ,, " Mama tokea uniache nimekuwa mwenye kupigwa tu kila siku, sina amani baba anapokuwa ndani, akisafiri natamani afie huko huko kwa sababu najua akirudi mambo ndo kama haya, Nlizani ni wewe tu umepitia kwenye mateso yake, kumbe yupo mwengine ambae ameteswa zaid yako? ,, Naomba nikufate uko uliko Mama. Alifumba macho akanyoosha kisu kwa mikono miwili, mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio lakini hakuitaji kuogopa ili atimize kile anachotaka kufanya.

" One ,,, Two ,,, Threee !!!!!!

Tukutane Sehemu ya 20 kesho hapa hapa kwenye app yako bora zaidi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.