Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 15) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 15)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM


SEHEMU YA 15

Seid alitoka ndani akiwa mwenye kung'aa, walimuaga mama wakaingia ndani ya gari na kuanza safari.

Wakiwa mwendo kasi kuwahi chuoni kutokana na umbali uliokuwepo pia muda kuwatupa mkono, Cm ya seid iliita haraka akaitoa mfukoni kuangalia nani anapiga, alijikuta anatabasam baada ya kuona jina la Raya, alibonyeza kitufe cha kupokelea kikawa hakibonyezeki, alijaribu tena na tena akashangaa kila akibonyeza hakikubali.
" Huu ndio ubovu wa cm vimeo haibonyezeki!. alisema akimwambia rafiki yake
" Tatizo nini!. Aliuliza hamad.
" Sijui.

Mpaka cm inakata bado ilikuwa haijakubali, aliiangalia bila kuimaliza akaachia msonyo na kusema
" Dah! Kwa namna hii bora nisimiliki cm kabisa, yani mtu anapiga haipokeleki nitairembeaa mimi shenzi zake.

Aliongea kwa hasira, sura yake akiwa tayari ameikunja.
Hamad aligeuka kumwangalia Seid, aliachia tabasam baada ya kumuona mshkaji wake alivyokunja uso kisa cm, Seid aliizima kisha akaiwasha, Raya nae muda huo huo alikuwa anapiga tena alijaribu  kuipokea ikawa imekubali kupokeleka, Raya alimuuliza mbona hupokei cm au nimekusumbua?.
" Hapana rafiki yangu unajua hivi vimeo vyetu sijui vinakuwaje Akyamungu Mambo?
" Poa ushafika?
" Bado Raya si nilikuambia kuwa naishi shamba?
" Ndio nakumbuka.
" Basi ndio niko na Hamad tunakuja huko
" Ok Poa msalimie Hamad.
" Yuko hapa nikupe uongee nae?

Kabla hajajibu cm ilikata, japo alipiga lakini kwa ongea yake alionekana yuko bize huko aliko.
" Hivi Hamad uliwai kumpigia huyu mwanamke au kuongea nae?. alimuuliza hamad cm ilipokata.
" Nani! Raya?
" Yah.
" Naongea nae kila siku hata leo nimeongea nae asubuhi.
" Ok maana nilimtumia namba yako kipindi flan hivi,
" ni rafiki yangu sana huyu mdada ila baba yake sasa, Eeeeee afai.
" Kwa nini unasema hivyo.
" Yani yule baba ni shida amekaa kama mchawi, mkali alafu malaya hatari, anapenda vitoto vizuri balaa!

Waliendelea kupiga stori tofauti tofauti mpaka walipofika Eneo la chuo kikuu cha Zanzibar, nje ya geti kulikuwa na msongamano wa magari ya wanafunzi pamoja na walimu yakiwa yanaingia ndani, Ilibidi watulie kwa nje kama dakika tano ili  yaishe,Yalipomalizika ndipo waliingia wakiwa wa mwisho.

Waliongozwa na mlinzi aliekuwepo kwa ajili ya ulinzi wa magari mpaka eneo la kupaki gari lao, waliliweka vizuri sehemu husika kisha wakashuka, Walianza kutembea mpaka walipokuwa wanafunzi  wenzao wote, wengi wakionekana ni wapya katika macho yao, huku Uso wa Seid ukigongana ana kwa ana na Uso wa Raya, waliachia tabasam wote na kupeana hi ya mbali mbali.

Ilikuwa ni kama hatua ya mwisho katika umasikini wa Seid, Baada ya kuangaika miaka mingi tokea utoto wake mpaka anafikisha miaka 21 na kupata bahati ya kuingia chuo, Sasa alihisi upepo wa mali unamjia mbele yake, aliamini hakuna kikwazo chengine cha kumfanya asimalize chuo na kuajiriwa moja ya ofisi kubwa Tanzania, Japo hakuwai kumuona baba yake lakini aliamini anafata  nyendo zake za kielimu, hakuacha kumshukuru Mungu kwa kila hatua anayopiga, Baada ya Mungu hakuamini kama kuna wa muhimu tena zaid ya mama alieangaika nae kipindi chote cha shida, na kupigana juu chini kuhakikisha mwanaye anapata elimu iliyo bora kabisa, huku muda mwingine akimshukuru sana Hamad kwa jinsi alivyomsaidia mpaka kufika pale alipofika.

Uhusiano wa hamad na Seid ulizidi kuwa mkubwa baada ya kuanza chuo, ilifika muda wanafunzi wenzao wakawa wanajiuliza hawa jamaa vipi, damu zao zilionekana kuendana sana, kutokana na ugumu wa masomo seid ilibidi ahamie mjini karibu na chuo zilipokuwa bweni kwa ajili ya kujisomea, Hamad nae alifanya hivyo hivyo, kundi lao likawa la mtu tatu, akiongezeka Raya.

Seid kama kawaida yake hakuacha kuwa muwazi juu ya maisha yake kwa Raya, Raya baada ya kuyajua maisha yote ya Seid alitokea kumpenda sana kwani aliamini ni kijana wa tofauti sana, ngumu mno kijana kukuambia maisha yake yalivyo magumu hasa akiwa chuo, alizidi kuwa nae karibu, akishirikiana kwa karibu na Hamad ili kumuwezesha Seid asijione kuwa yeye maskini.

Walifurahi na kucheka muda wote waliokuwa pamoja, Kuanzia darasani mpaka nje ya darasa walikuwa wamoja, Hawakwenda kokote baada ya kutoka darasani kwanza walikutana na kueleweshana mawili matatu kuhusu kile walichokisoma, japo masomo yalikuwa magumu sana lakini wakawa watu tishio darasani, walikuwa wakiulizwa swali lolote lazima walijue, hawakuwa na tuisheni yoyote kubwa zaid ya kujipa bidii wao wenyewe, huku wakiona swali gumu sana wanamuita Ticha ambaye ndio mtu wao wa karibu sana wote watatu na kuwaelewesha.

Waliendelea kuwa na uhusiano wa karibu mpaka mwaka ukaisha tangu wako chuoni, walifanya mitihani na kufunga chuo kwa muda wa wiki moja, kila mmoja hapo ndipo alipata nafasi ya kurudi nyumbani, Seid kidogo alishatakata na kuwa kama vijana wa mjini, mafuta mazuri pafyumu na nguo nzuri vyote alivijua mara tu alipohamia mjini, Mwili wake tayari ulishang'aa, nywele ziliendana kwa karibu na za kiarabu kutokana na kuzitengeneza vizuri,  mwili wake uliokuwa umejazia kila kiungo, ulionekana kuwa safi muda wote, Bi Najma alishangaa sana baada ya Seid kufika nyumbani  kumuona mwanaye alivyobadilika, walikumbatiana wakajualiana hali, kisha wakaingia ndani kwa ajili ya maongezi ambayo yangechukua muda mrefu.

Waliongea mengi wakiwa ndani, Bi Najma alitumia muda mrefu kumuangalia mwanaye aliefanana na chotara wa kiarabu, ambayo ndio asili ya upemba,  bi najma alijikuta akiupa nguvu msemo usemao "kweli duniani hakuna mbaya zaid ya shida kusababisha tu, Seid akawa mtu wa kutabasam kila alipomuangalia mama yake, Kitabu kilishaanza kuiva kichwani, hakuwa na zawad kubwa ya kumpa mama yake baada ya kurudi nyumbani zaid ya Cm aina ya nokia tochi, Bi najma alishukuru sana, baada ya kuipewa alimmwagia mabusu kila sehemu ya paji la uso mwanaye, Huku akinyoosha mikono juu kumshukuru Mungu, kwani hakuamini kama atamiliki tena cm, wakati mara ya mwisho ilikuwa kipindi yuko kwa mume wake kabla ya kuipasua kwa hasira alizokuwa nazo baada ya kugundua mambo anayoyafanya mume wake.
" Mungu akusaidie sana mwanangu.
" Ameen mama.
" Eh jamani yani sikutegemea kama nitakuwa na mawasiliano tena kiukweli.
" Usijali mama, ila sijamsahau na bibi pia.
" Ehe!!
" Nae yake hii hapa.
" Mungu Wangu, Ebu fanya haraka umpelekee, atakushukuru mpaka basi, yani Jamani, Mmwaaaa mwanangu yani hapo dua zote ataziomba leo Eh Mungu akubariki sana baba yangu kuzaa raha jamani..

Seid hakuwa na la kuongea zaidi ya kutabasam, aliitaji apumzike kisha kesho yake ndio aende kwa bibi yake kumsalimia na kumpelekea Zawadi.

Usiku uliingia walijiandaa kwa ajili ya kulala, Seid alikumbuka maisha aliyokuwa akiishi mwaka mmoja nyuma kabla ya kuhamia mjini, Mama hakuitaji kulala kitandani alimuachia mwanaye alale, Yeye alishusha shuka iliyopo katikati akatandika  chini akalala, japo mbavu zilikuwa tayari zishakuwa za uzee zee, ila ilimbidi kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo juu ya mtoto wake ambaye ilikuwa ni kama mboni yake moja..

Seid akiwa kitandani, alijikuta anakuwa na mawazo mengi juu ya Raya msichana alietokea kumpenda ghafla, alitamani siku moja ammiliki msichana mzuri kama yeye lakini alijikuta akiogopa hata kumwambia kuwa anamuitaji kimapenzi kutokana na kuhisi atavyomchukulia vibaya, waliishi kwa karibu sana ndani ya mwaka mzima bila kumwambia chochote juu ya mapenzi, alijigeuza huku na kule kitandani, Kila alipokumbuka sura yote ya Raya alijikuta anapokea  ujumbe flan mtamu kwa ajili ya mapenzi.

" Rayaaaaaa! Mwanamke ninaye hisi kabisa umeniteka kimapenzi, Simjui mwanamke alivyo akiwa amevua nguo tokea nizaliwe, nimezizuia hisia zangu mpaka hapa nilipofikia, Lakini sasa hivi nahisi kabisa kushindwa, Raya wewe ni mwanamke mzuri na unapendeza kwa watu, sijui kama huna mtu kwa uzuri wako, Ila lazima nijaribu bahati yangu, sijiwezi kwako Raya, nakupenda..

Aliwaza peke yake akiwa amelala chali mkononi akiwa ameshikilia kisimen chake, alijiuliza maswali mengi juu ya kumpata Raya, mwisho akaona haiwezekani liwalo na liwe tu, alitoa lock cm akaingia katika uwanja wa message, akaandika ujumbe mfupi kwa ajili ya kuutuma kwa Raya  ,, " Raya nisamehe sana kama nakukosea, Ila huu ndio ukweli utokao moyoni mwangu, Raya najua mimi sina uwezo wowote, na uenda sio type yako au sina hadhi ya kuwa na wewe, Ila nahisi nina hisia kali sana za mapenzi juu yako, Nakupenda kimapenzi Raya, nimejizuia mwisho nimeshindwa, naomba usinifikirie vibaya na nisamehe kama nakukosea, pia usipanik ukanijibu vibaya tafadhali. Nakupenda..

Mpaka anamaliza kuandika ujumbe huo jasho lilikuwa linamtoka, huku akiwaza endapo atautuma atajibiwa kitu gani, aliachia pumzi kubwa ambayo kama bi najma angekuwa hajasinzia lazima angeuliza, Aliingia upande wa majina akaselect Raya, Akaituma text na kuanza kuirejea rejea mara mbili mbili kama iko sawa au laa!.

Baada ya kuona imeenda alihisi amemkosea sana Raya, moyo ulienda mbio zaidi ya mota, kulikuwa na kibaridi lakini jasho lilikuwa linavuja usoni kama mtu aliekimbia masafa marefu, aliona hatojibiwa chochote zaidi ya kuambiwa ,, " Huna hadhi ya kuwa na mimi? au " Umenikosea sana, au "Jieshim Seid kukaa na wewe karibu isiwe chanzo cha hadi kunitaka kimapenzi.
" Dah! Mungu nisaidie, sijui kwa nini nimeituma hii message, Nimpigie cm sijui nimwambie nimekosea namba!, Loh.

Jasho lilizidi kumtoka kijana, alichukua shuka la kujifunikia ikabidi ajipanguse usoni huku macho yakimtoka na kujilaumu kwa nini ameituma, alihisi kabisa presha inapanda na kushuka, juu ya kula chakula cha kushiba usiku lakini alihisi njaa ya ghafla kwa jinsi tumbo lilivyoanza kuuma.

Akiwa anamaliza kujifuta, alisikia cm ikifanya Tin Tin, Tin tin, ikiambatana na muungurumo wa vibret, akajua moja kwa moja ni message kutoka kwa Raya, alitamani asiifungue mpaka kesho kwa woga wa kukutana na jibu baya, akiwa hajakaa sawa alisikia nyingine ikiingia, neno "Mungu wangu!, lilimtoka.

" Um hapa hakuna jibu zuri zaidi ya kutukanwa tu, na sijui itakuwaje nikikuta kanijibu vibaya, nitalala kweli?, na itakuwaje nikirudi chuo hatonichamba mbele ya wanawake wenzie?, Dah huu ndio ubaya wa kufanya kitu bila kufikiria.
mawazo yalikiandama kichwa chake, Ghafla tena alisikia Tin tin, Tin tin, ikiwa mara ya tatu, alinyanyua cm yake akaitoa lock huku akisema "Ah kama amejibu vibaya poa tu" ,,, alibonyeza katika kitufe kilichokuwa katikati, akaingia kwenye mkusanyiko wa text zote, alishangaa macho yakamtoka baada ya kuona message  tatu zote ambazo hazijafunguliwa zinatoka katika ofisi za Zantel. Nguvu zilimuishia ghafla, aliachia msonyo ulioambatana na maneno" Pumbavu zenu kabisa nyie" ,, aliitupa cm pembeni akageukia upande wa pili kulala, ndipo alisikia cm kwa nyuma inaita.

*********
Rahma ambaye ni mke wa ticha alikuwa tayari ana mimba ya miezi saba, Ticha hakuitaji kucheza mbali na mkewe, mimba ya Rahma ilikuwa ni miongoni mwa zile mimba za kuwachukia wanaume, alijikuta anamuona mumewe kama mavi anapokuwa mbele yake. mara tu baada ya kufikisha mimba ya miezi minne, vituko vilikuwa vidogo vidogo lakini ilipofikisha saba vikakua, Upo muda hakuitaji kumuona nyumbani na upo muda alimuitaji.

Usiku huo ticha aliambiwa alale ubarazani, hakuweza kukataa kwa sababu ya kumuelewa vizuri mkewe, alikuwa akinuna zaidi ya sana pindi anapokataa, kitu ambacho aliambiwa sio kizuri na wataalam.

Alitoa mswala nje kwenye ubaraza Ticha akaweka ubavu kupiga usingizi, alikaa muda bila kulala akaona arudi ndani achukue japo mto aweke vizuri kichwa chake uenda angepata usingizi.

Rahma bado alikuwa hajasinzia, alimuangalia sana alipoingia ndani, akainuka na kumuuliza.

" Umesahau nini?
" Hapana, nimekuja kuchukua tu mto huu niende kulalia.

Alipouchukua rahma alitoka kitandani mbio akisema "Wee weee weee! Una mto hapa!, Ebu lete mto wangu hukoo! si nishakuambia sikuitaji nenda bhana huna chako hapa wee vipi?.

Alimnyang'anya mto akaurusha kitandani na kumuomba atoke mbele yake, Ticha hali hiyo ilikuwa inamuuma sana lakini alijua tatizo ni mimba.

" Si utoke? ,,Aliongea rahma akionekana kukasirika kwa kuzidi kumuona Ticha mbele yake.
" Lakini mke wangu unavyonifanyia sii vizuri jamani kwa nini lakini! ,, aliongea ticha katika hali ya kutaka kulia, rahma alianza kubadilika usoni, alimuangalia Ticha bila kummaliza, kinyaa kilianza kumjia taratibu, mara alikimbilia chooni kwa ajili ya kutapika ili kumuonesha jinsi anavyomchukia kwa muda ule.

Alipomaliza alisukutua mdomo akarudi, bado alimkuta ticha akiwa amesimama,
" Jamani bado umesimama hapo tu si uondoke Aaagh.

Ticha alitoka kiunyonge, baada ya kuwa tayari ametoka nje ya mlango, Rahma alienda mbio mpaka kwenye mlango, akaufunga kwa ndani.
" Mianaume mingine sijui ikoje ushaambiwa hutakiwi bado unang'ang'ana tuuuu mpaka nimetapika, yani ungejua nnavyokuchukua we mwanaume, msiiiiiiiu.

Alirudi kitandani akalala, Ticha alitoka mpaka kwenye baraza ulipokuwa mswala (mkeka) akaweka ubavu kwa mara nyingine kuangalia kama usingizi utapatikana.

" Dah Kiukweli hata kama ni mimba hii sasa ni too mach, juzi juzi tu hapa kanitimua kwenye nyumba yangu kama mwizi eti hataki kuniona, jana amenambia nipige mguu mpaka mjini yeye akiwa kwenye gari, mchana hajaitaji nile, sasa hivi nisilale jamani!, hii adhabu ni kwangu mimi tuuu au wanandoa wote? Mbona mateso haya jamaniii!

Ticha aliongea peke yake kwa hasira na uchungu machozi yakiwa yanamlenga lenga.

********
Seid hakuitaji kuiangalia cm yenyewe, iliita mpaka mwisho bila kujua nani kapiga, ilipokuwa tayari imekata aligeuka upande ilipo cm, aliishika akaangalia nani kapiga jina likaja raya.

moyo wote uliripuka, cm ikaanza kuita tena jina likiwa hilo hilo,  hakusubiri, akapokea haraka moyo wake ukiwa  una dunda, aliiweka sikioni na kusikiliza kitachoongelewa upande wa pili.


Tukutane Sehemu ya 16 hapa kesho, waalike na washkaji kupata uhondo huu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.