Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 13) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 13)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM


SEHEMU YA 13

Ilipoishia......

"Um mbona mlango haujafungwa kwa nje huu na mama haitiki?, Mama!, Mamaa! 
Alimuita tena bila kuitikia.
" jamani ina maana mama hayumo ndani au  vipi?

Songa nayo:

Baada ya kuona kimya alitoka eneo la mlangoni akaingia shambani kumtafuta akidhani uenda umefungwa tofauti na alivyozoea, shambani bado hakumkuta akarudi tena mlangoni na kwendelea kuita upya, Baada ya kuona haitikiwi, maneno yalimtoka akiwa tayari amekunja uso wake.

" Dah, hii ndo shida ya umasikini ninayoisemea mimi kila siku, hapa mama angekuwa na cm si ningempigia tu nikajua yuko wapi!?. Mama! Mama yangu! aliita akigonga mlango kwa nguvu.

" Abee.. ni sauti iliyotokea ndani.

Alishangaa sana kusikia mama yake anaitika baada ya kugonga zaid ya mara tano kwa nguvu, bi najma alifungua mlango akiwa katika hali ya uchovu hali ya usingizi, seid alimuangalia mama yake bila kummaliza mwisho akaachia tabasam na kusema.

" Tatizo nini mama yangu!, nimeita mpaka nimekata tamaa, nikawa na wasi wasi juu yako tatizo nini?
" Ina maana umekuja muda mrefu!?. Aliuliza bi najma.
" hadi nimezunguka nyuma kwenye dirisha nikaenda shambani sikuoni mama yangu!, tatizo nini?. Aliongea kwa sauti ya chini kama mtu anaesikitika.
" Ah! kweli usingizi ni nusu ya kifo, sikusikia kabisaa kiukweli kama umeita, karibu.

Alimpokea mwanae akaingia nae ndani huku akimwambia amsamehe ni uchovu wa usingizi aliokuwa nao siku nyingi, kutokana na kila siku kuamka mapema kufanya kazi nyingi na kukosa muda wa kulala mchana.
" Vipi hali za mjini huko wanasemaje?. Alimuuliza baada ya kuingia ndani, Seid akiwa amekaa kwenye kigoda mama kitandani.
" Namshukuru Mungu salama kabisa.

Walifungua ukurasa wa mazungumzo, alimueleza kila kitu kilichoendelea mjini, pamoja na matokeo kuwa mazuri ya kuingia chuo, Bi Najma alimpa hongera mwanae akionekana kuwa na furaha, alipiga miayo akahisi usingizi bado unamuuma machoni, aliinuka alikokuwa amekaa akachukua maji kidogo kwenye kikombe, akatoka nje kunawa uso ili awe sawa.

Siku zilikatika hatimae wiki ikaondoka,
Maisha ya pande zote tatu yalisonga mbele, Mawasiliano ya karibu sana yakiwepo kati ya Ticha, Hamad na Seid, Huku Seid akitumia muda mwingi kumsaidia mama yake na kufanya mambo yake muhimu kwa kutumia laptop ambayo tayari alipatiwa na Hamad.

Nyumba yao ilikuwa ni ya mawe juu iliezekwa makuti, kama ilivyo kawaida ya nyumba za kizanzibar, ngumu sana kuzikuta hazina umeme, nyumba hii nayo ilikuwa ina umeme japo kulipia ilikuwa ni mara moja moja kutokana na kipato kuwa chini sana, ila msimu huo Seid alitoa elfu 20 katika pesa alizopewa na waziri akalipia umeme wa miezi minne au mitano kutokana na matumizi yao kuwa madogo sana.

Baada ya wiki mbili, mchana mmoja wa jumaa nne seid akiwa yuko anahamisha baadhi ya vitu alivyotumiwa na Hamad kupitia njia ya Email kwenye Laptop akivitoa kwenye Email kuvipeleka kwenye my Memories ( kumbu kumbu zangu), alipigiwa cm ghafla na Ticha wakasalimiana kisha akamualika kwenye harusi yake ambayo ingefanyika siku nne mbele.

" Ticha wangu ulikuwa ujaoa Yakhe!.
Seid alimuuliza kwa mshangao, baada ya kuambiwa anaalikwa kwenye harusi.

" Aaaaaah nlikuwa bado bhana, sasa hivi ndio nachukua jiko.
" Aissee hongera sana ticha wangu, mpemba, wa bara au wa hapa hapa unguja.
" Huyu bhana wa unguja hapa hapa.
" Basi hapo najua mambo mazuri, Ikifika Ramadhani mambo ya vireja, na keki keki hazikosekani.

Ticha alicheka sana aliposikia hivyo, mwisho wa kicheko akamilizia na maneno,
" Hamna bhana ,, !
" Itakuwa jumaa mosi?, aliuliza seid
" Hapana ni ijumaa jioni. Nataka nifate sunna za ukoo wetu..
" Rusha roho la nguvu la kukesha au itakuwa mwendo wa madufu?..
" Yani hilo la kutosha baada ya harusi mimi nitakuwa ndani nakula vitu nje mnaendeleza.
" Hahahaaaaaa aya mwalimu wangu nitakuja asubuhi na mapema japo imekuwa ghafla.
" Hapana si ghafla, watu wengi washajua hilo ila wewe nilijua hata nikikutaarifu siku yenyewe hutokosa kuja.
" Kweli, kweli kabisa mwalimu wangu.

Waliagana ticha akakata cm Seid akiwa anacheka, aliangalia screen ya cm kisha akaiweka pembeni, mama yake Bi Najma akamuuliza.
" vipi mbona furaha?. Seid alimgeukia akamjibu.
" si unamkumbuka yule Ticha aliekuja na Hamad nikakuambia amepigwa Risasi?.
" Ehe!
" Anaoa Ijumaa..
" Mashallaah! Mungu amuongoze jamani!.
" Aameen!, Seid aliitikia akiweka sawa baadhi ya mambo kwenye laptop.

Alifungua upande wa email ili amchek rafiki yake hamad kama yuko online amtumie ujumbe mfupi, bahati nzuri alimuona yuko online akaingia upande wa kuandaka message."Una taarifa kuwa Ticha anaoa ijumaa?

alipomaliza kuandika aliutuma, akatoka upande wa email akaingia upande mwengine huku akiongea na mama yake.

" Mwanangu unapenda Sana Raha Mashallah, hiyo laptop utafikiri ulikuwa nayo miaka mingi na maji yako pembeni mwenyewe. Aliongea baada ya kumuangalia mwanae kwa muda mrefu anavyochezea mashine..
" ndio maana mama niliwahi kukuambia kuwa mimi sio mtu mwenye hadhi ya shida, Shida nimezipata bahati mbaya tu mimi.

Message kutoka kwenye email iliingia.
Aliifungua na kuiangalia. " Nilikuwa sina habari hizo ila kanipigia sasa hivi na kunambia kuhusu hilo.
(Repley >> " Hata mimi kanipigia muda huu kunipa hizo habari, vipi!?, sisi ndio watu wake wa karibu, na Shary yule mhindi anasema katika kitabu chake, Kwenda kwenye ndoa ya mtu unae mjua bila zawadi yoyote ni sawa na kinyonga kubadilisha rangi mbele ya mtu mjinga >> Send.

" Mama vipi umepitiwa na usingizi.
Alimuuliza mama yake baada ya kujibu ujumbe wa Hamad, alivyoona hajajibiwa aligeuka nyuma na kukuta tayari mama yake kalala zamani.

Alimuangalia sekunde kadhaa, aliporudisha macho yake kwenye screen tayari alikuta ujumbe akaufungua na kuusoma. >> "Hahahahaaaa naomba unambie hayo maneno yako katika kitabu gani nimekisahau,  ikifika hiyo siku wewe njoo tu mjini mambo yote tutayamalizia huku na tutaingia katika harusi yake kama wafalme.

Seid roho yake ilisuuzika aliposoma maneno ya rafiki yake, hakupoteza muda akaripley. << Wao Niko na furaha sana kusikia hivyo, ndio maana nasema wewe ni zaidi ya rafiki kwangu, hayo maneno yanapatikana katika kitabu cha "SHARK SHARQ" mwandishi na mtunzi ni Sharq Muzdeil mwenyewe, humo kuna vitu vizuri hata huyo william mwenyewe haoni ndani.

Akiwa anamaliza kuandika alama nyekundu ilionekana pembeni ya Laptop akajua charj inataka kuisha, na umeme ulikuwa umekatika muda huo, aliisend haraka akafunga laptop na kuanza kufanya mambo mengine ambayo yalibidi wakati huo..

Asubuhi na Mapema ya siku ya Ijumaa alijiandaa pamoja na mama yake kwa ajili ya kwenda kwenye harusi ya Ticha, Ticha alimuomba sana aende na mama yake ili nae kumpa heshima kwenye harusi, Mpaka kufika saa mbili na nusu walikuwa tayari wako mjini, ambapo walipata mawasiliano ya haraka kutoka kwa Ticha baada ya kufika, Seid aliwasiliana na Rafiki yake Hamad ili wakutane, Mama seid alipanda gari nyingine kwenda kuungana na wakina mama wenzake nyumbani kwa bwana harusi kwa ajili ya maandalizi ya vyakula, akiwa tayari amepata kuelekezwa sehemu yenyewe na kutumiwa watu wa kumfata endapo atafika sehemu husika.

Hamad alimfata seid darajani haraka baada ya kupigiwa cm na kuambiwa tayari ashafika, walipokuwa tayari wameonana walikumbatiana kisha wakaanza kutembea kuingia ndani ndani town sehemu zinapouzwa zawadi za harusi, Walinunua vitu kadhaa vya thamani ili kupeleka kama zawadi kwa Ticha, Huku Hamad akitumia tena kiasi cha laki moja na nusu kumnunulia Suti moja matata sana Seid ambayo ilikuwa ikifanana na ya kwake, Ili wakiingia kwenye harusi waweke utofauti wa watu wengine, na watu wajue kuwa kweli hawa ni mabest wa huyu jamaa.

Harusi ilikiwa inaanza saa kumi kamili, waliitaji kutumia muda mfupi uliokuwa umebakia kuhakikisha wanajiandaa vilivyo, walisaidiana kulipamba gari aina ya Suzuki grand Vitara alilokuwa anapenda kutumia hamad kuhakikisha linapendeza, kwani walitakiwa kuongozana na  magari matatu ya watu muhimu ambayo yatakuwa yanatoka kumchukua bibi harusi na kumpeleka nyumbani kwa bwana ambapo kuna harusi yenyewe.

Ilipofika muda wa saa saba tayari kila kitu kilishakamilika, Ticha alikuwa ni mtu wa kupiga cm kila wakati kwa kina Hamad ili wawahi, Wazazi wote wa Hamad nao walishaenda kwenye shuguli hiyo ambayo tayari ilishaanza, Seid na hamad walijiandaa kwa ajili ya kwenda mbweni sehemu anayotoka bibi harusi, ili kuungana na msafara utaokuwa umemchukua bibi kumpeleka mchina mwanzo.

Hamad na Seid walivalia na kupendeza wakiwa nyumbani anakoishi hamad, Seid ni kama mtu aliekuwa amezaliwa upya kwa jinsi suti ilivyompendeza na kumfanya ang'ae, Hamad alijikuta akimwambia ,, "Ndugu yangu wewe ni Hand some shida tu ndio zinakufanya uonekane mwanaume wa kawaida. Alienda kwenye kioo kikubwa kilichokuwa chumbani kwa hamad na kujitazama, Yeye mwenyewe alijishangaa namna alivyopendeza, huku akikumbuka msemo usemo "Shida zitakufanya ufanane na nyani hata kama sura yako nzuri zaid ya tunda la apple.

Walitoka nje wote wakiwa ndani ya Suti zenye rangi tofauti tofauti za kung'aa, walifungua gari wakaingia ndani na kuanza safari ya kuelekea Mbweni.
Hamad upara wake aliutia mafuta ya kutosha kiasi cha kumeremeta, walikanyaga mafuta mpaka mbweni ambapo waliwakuta watu tayari wakiwa wamejiandaa, Salam za hapa na pale zilipita, Masheikh waliotakiwa kusimamia ndoa tayari nao walikuwa eneo hilo, Mabasi zaid ya manne yalishaajaza watu kwa ajili ya kumsindikiza mwari wao, huku ngoma aina ya madufu yakipigwa, yaliyoambatana na nyimbo au Qaswida za harusi.

Bibi harusi alikuwa ni binti wa kizanzibar mwenye umri wa miaka 22 aitwae Rahma, tayari akiwa ndani kwao alishaandaliwa na kupewa mafunzo yote ya kwenda kwa mume, machozi yalikuwa yakimtoka pindi alipowaza maisha mapya ya ndoa yake na kuyaacha maisha ya nyumbani aliyoyazoea.

Taratibu walimtoa nje kumpeleka kwenye gari ambalo lilikuwa na mandhari nzuri ya kifahari, aliingia ndani watu wakiwa wanapiga vigele gele huku nyimbo  za "ai yaya kuolewa utarudi nyumbani kutembea zikiendelea kwa baadhi ya marafiki zake waliokuwa wakimfaham, na majirani waliokuwa wameizunguka nyumba hiyo, Wengine wakitoa machozi ya furaha kumuona mwenzao kapata mwanaume wa kumuoa mara tu alipofeli, huku kukiwa na mirindimo ya watoto na wasichana wadogo wadogo waliokuwa wakiendelea kupiga ngoma ngoma zilizosababisha tafrani.

Baba yake hakuweza kuudhuria harusi hiyo kwa sababu alikuwa nje ya nchi kimajukumu ya kazi japo tayari alishatoa baraka, ni mama yake na ndugu zake wengine tu waliokuwepo kwenye shuguli hiyo mpaka Rahma anaolewa.
Rafiki yake kipenzi aitwae Raya ndio alikuwa amekaa nae kwenye gari aliloingiamo kwenda kwa mumewe mtarajiwa, hakuitaji kukaa na mtu mwengine wala kusimamiwa na yoyote zaid ya rafiki yake huyo, ambae walikuwa wakisoma wote kidato cha sita shule moja darasa moja ila yeye akafeli na rafiki yake akapita kuendelea na chuo.

Walikuwa wameshibana zaid ya mapacha wawili, wakiwa ndani ya gari ni machozi tu yalikuwa yakiwatoka, Rahma akilia  juu ya maisha yake mapya ya kwenye ndoa, Raya akilia kukaa mbali na rafiki yake huyo aliemzoea.

" Rahma, Huna haja ya kulia sana, Kwani yote ni mipango ya Mungu, ila mimi ndie napaswa kulia zaid ya sana kutokana na machungu niliyo nayo, Kwanza naingia chuo rafiki yangu niliekuzoea ukiwa haupo, pili kutumia muda mwingi kuwa mbali na wewe kitu ambacho itanichukua muda kukizoea, Ila mimi nakutakia maisha mema ya ndoa yako, nina amini Mungu atailinda na kuiweka mbali na mitihani ya kila mara, nakupenda sana my real friend, my Mchumba, my Husband, my mpenzi, my Every think kiukweli naumia sana Rahma.

Raya aliongea huku akilia kwa rafiki yake, Dereva alishangaa kusikia watu nyuma wakiitana my mchumba my husband, alitoa macho na kuachia tabasam, aliekuwa pembeni yake akamwambia "mambo ya watoto wa kike hayo achana nayo.

Baada ya kufika kwenye harusi yenyewe ambako kulikuwa na maandalizi yote, Gari zilipaki sehemu husika za kupakia magari, Seid na Hamad ndio walikuwa wa kwanza kushuka kwenye gari lao, kisha wakaenda kufungua milango ya gari alilokuwa amepanda bibi harusi na Raya, makofi ya taratibu yalipigwa kutokana na wale wa uswazi uswazi wote kuishia nje kidogo ya shuguli, Bibi harusi alishuka pamoja na Raya, kisha milango yote ya gari ikafungwa.

Kipindi Raya anapiga hatua nyuma ya bibi harusi huku umati wa watu ukiwa unapiga makofi, kwa bahati mbaya alikanya gauni lake refu akaanguka chini, Upepo kidogo ulikuwa unapiga muda huo, gauni lote lilipanda juu surual ya jinzi aliyokuwa ameivalia  ndani ndio ikawa imemnusuru kumwaga radhi mbele ya umati wa watu, huku baadhi ya watu wakianza kutoa macho na maneno ya mshangao kwa kitu wanachokiona.


Tukutane Sehemu ya 14 kesho hapa hapa, waalike na marafiki, tuachie comment hapa chini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.