Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 12) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 12)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM


SEHEMU YA 12

Mzunguko wa kutangazwa habari za kurudiwa kwa matokeo ya kidato cha sita ndani ya muda mfupi ziliwashtua wengi, maradio mengi yalitangaza habari hiyo, huku Tv ya Z B C nayo ikitangaza habari za matokeo hayo na kupata fununu za chini kwa chini za waziri wa elimu kupiga cm kwa kijakazi wake na kuitaji ajiuzulu kazi ndani ya masaa 24 bila kujulikana chanzo chake nini.

Nini kiliendelea?. SONGA NAYO...

Seid bado alikuwa njiani kuelekea nyumbani alipokuwa akiishi na mama yake, Cm yake ya simen ilianza kuita, akazima mziki akaitoa mfukoni na kupokea haraka baada ya kuangalia kwenye screen na kukuta jina ni Hamad.
" Nambie rafiki yangu.
" Vipi ushafika?
" Bado ndio kwanza naiacha bububu.
" Ok!, habari zishaenea za kurudiwa matokeo.
" Usinambie!
" tayari vyombo vya habari vishatangaza kila kitu.
" Furaha kwangu hiyo rafiki yangu. Alisema kwa tabasam zito lililosheheni vizuri mdomoni mwake.

Waliongea zaid na zaid kisha hamad alikata cm, Seid alipiga mayoe ya furaha akaachia ngoma na kwendelea kudundika ndani ya gari, aliona dunia yote ameitawala yeye ndani ya muda mfupi, baada ya kupita sehemu iliyokuwa na msongamano kidogo wa magari alikanya mafuta speed ikasomeka 100 kamili, aliviangalia vitu vinavyowaka kwenye gari akasema akitabasam peke yake 
" Haya ndio maisha sasa, yani mtu upo kwenye chombo raha yake utafikiri tayari uko peponi manina, hadi moyo unacheka ndani kwa ndani, ukonde kwa lipi sasa!? na nikizipata mie, Eheeeeee! mbona wajiandae!, haiwezekani nilie shida miaka yote kisha nije kuzipata nishindwe kula bata kwanza, Lazima niwapige shenzi time alaaa!.

Ni taa tu zilikuwa zinaonekana kutokana na mwendo kasi wa gari, ndani ya nusu saa alifanikiwa kufika nyumbani kwao, alipaki gari nje akigonga honi za mfurulizo, Bi Najma alikuwa amekaa ndani ikabidi atoke nje kuangalia honi za nini usiku huo.

Alishangaa alipokuwa tayari ametoka nje kuona gari zuri limepaki, Seid alishuka kwa mbwembwe zote akamkimbilia mama yake aliekuwa amesimama mlangoni.
" Shikamoo mama.
" Maraaba.
"Mama haya ndio maisha yangu ya badae.
Alimsogelea mama yake na kumwambia hivyo mara alipomaliza kumsalimia.

" Wewe mtoto, hili gari umelitoa wapi?.
" Rafiki yangu kanipatia nirudi nyumbani bila kutumia usafiri wa dala dala akijua utanisumbua, Ila Haya ndo yatakuwa maisha yangu ya mbele mama yani ni gud time tu hadi raha.

" Na vipi kuhusu matokeo yako, mmefanikiwa?
" Tuingie ndani kwanza mama yangu mengine yatafata.
Waliingia ndani wakafunga mlango, Waliongea mengi seid akimueleza kila kitu mama yake, walipomaliza kuongea kama kawaida ilishushwa pazia kisha kila mmoja akalala.

Asubuhi na mapema bi najma aliamka akaingia shambani, Seid nae alipoamka alifata nyayo za mama yake, walipariria baadhi ya viazi na mazao mengine yaliyokuwemo shambani, saa nne walitoka wakaandaa chai ya kunywa wakiwa na uhakika wa vitafunio hata chakula cha mchana kutokana na pesa waliopatiwa na hamad kuwa bado ipo.

Seid alipotoka shambani ilibidi aende sokoni kununua mandazi au chapati pamoja na vitu vingine, aliporudi tayari alikuta chai nzuri ya asilia imeandaliwa na mama yake, walianza kunywa wakiongea maneno ya kutaniana yaliyowafanya wacheke na kufurahi.

Walimaliza Seid akachukua maji akaenda bafuni kuoga, Baada ya kumaliza alikuta cm yake inaita, akapangusa maji maji yaliyokuwa katika kiganja akapokea haraka.

Alikuwa ni rafiki yake ambaye alimpigia kwa ajili ya kumwambia awahi mjini aone mambo mazuri kuhusu matokeo na ticha kiujumla.
Seid alijiandaa chap chap akamuaga mama yake kwa ajili ya kuondoka.
" Hivi mama, ungesikia raha gani kama ningekuwa nimepaki gari kama hili alafu la kwangu. Alimuuliza mama yake akiwa mbele ya gari.

" Ningejisikia furaha sana, ila usijali mwanangu yote ni majaliwa utapata tu lako babaangu mi nakuombea dua, nina hakika Mungu atasikia kilio changu siku moja.

Seid hakuongea chochote kuongezea kile alichokiongea bi najma, alitembea hadi kwenye mlango wa gari akiwa anatikisa kichwa chake, alibinya funguo, gari ikawaka, alifungua mlango akaingia ndani.
" Na nikiingia chuo watanikoma mimi Akyamungu, kwa sababu mambo kama haya ndio yananipa hasira za kusoma, naishi kwa tabu, shida, njaa wenzangu wanamiliki vitu vikubwa kama hivi, malaptop, ma ipad ma nini sijui dah yote maisha tu poa. Aliongea peke yake ndani ya gari, aliwasha taratibu akaanza kurudi nyuma kutafuta upenyo wa kugeuzia, Bi najma muda wote alimuangalia mwanae anavyoendesha, japo alikuwa hamuoni kutokana na vioo kuwa vyeusi. Aliachia tabasam akanyoosha mikono juu na kumuomba Mungu amuongoze mwanae ili nae siku moja afanikiwe apate vya kwakwe.

Baada ya kugeuza gari alikanyaga mafuta mpaka mjini, alifika eneo la chuo kila mmoja akishangaa kuona Seid anaendesha gari wakati haijawai kutokea, alimkumbatia rafiki yake hamad aliekuwa tayari yuko eneo hilo, alisogea ubaoni kuangalia matokeo ambapo kulikuwa na mkusanyiko wa wanafunzi wengi, Alipoyaona alijikuta akiachia meno yote mdomoni nje kwa furaha, Machozi yalianza kumlenga lenga akainua mikono juu na kumshukuru Mungu.
Hamad alimuomba waende pembeni kwa ajili ya kuzungumza, kabla ya yote seid alimpigia mama yake cm akamwambia amepata matokeo mazuri ya kuingia moja kwa moja chuo.

Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa bi najma. Hamad na seid walisogea pembeni kuongea huku wote wakionekana kufurahi sana kwa kuwa bado wataendelea kuwa darasa moja hata watakapokuwa chuoni.

" Rafiki yangu Niliwahi kukuambia siku moja haki ya mtu  Haipotei, na bora aibu kuliko fedheha waswahili wanasema, ila hawa watu wamekubali fedheha wakaogopa aibu niulize kwa nini.

Hamad  aliongea kwa kutumia mdomo na vitendo vya mkono.
"Kwa nini ,, Seid alisema kama alivyoambiwa aseme.
"Vizuri, Michael Jamseh anasema katika kitabu chake kizuri cha kifaransa ambacho mpaka kesho hakupatikana mwingereza wa kutia neno lake hata moja.
" Mtu anathamini chake kuliko cha mwenzake, waliowengi wanafurahi kuona vya kwao vinafanikiwa ila vya wengine vinafeli, mtu wa aina hii yuko tayari akuone unachomwa mshale yeye akacheka akijua hupati uchungu, ila endapo ule mshale utamgeukia uso wake hubadilika na kuwa kama uso wa chatu mwenye njaa kali, ambae hana huruma na mwanadam pindi anapotaka  kummeza. Huyu jamaa rafiki yangu alikuwa na akili sana kuyaongea haya maneno, Mr Zubeir aliitaji kutumia pesa ili mwanae apite, akasahau msemo wa wahindi usemao my Opena, Mungu alivyo mkubwa, akamuonesha kuwa haki ya mnyonge miaka yote hailiki hivi hivi, aibu aliyoipata sasa hivi katimkia marekani, kijana wake kampeleka wapi sijui huko ndio maana humuoni hapa, Watu baada ya kutumia akili zao za kuzaliwa kupata matokeo mazuri anategemea kuhonga, si upuuzi uliopindukia huo?, Kizuri  zaid soma hili gazeti ukurasa wa nne uone mambo. Alisema hamad.

Seid alipatiwa gazeti la Zanzibar Leo, lililokuwa lina habari za kijakazi wa Waziri wa Elimu profesa Sharif kujiuzulu kazi asubuhi ya saa mbili, pamoja na ukweli wote kubainika kuhusu kupigwa risasi kwa ticha, Pia kutangazwa kiongozi huyo kuwa miongoni mwa watu wajuu walioshiriki kuuza matokeo ambao wengine hawakujulikana. Seid alishangaa zaid baada ya kuiona picha yake kwenye gazeti na maelezo yasemayo. "Huyu ndio kijana aliewaburuza watoto wa vigogo katika matokeo, matokeo yake ndio yaliyokuwa yameuzwa.

Alifunika gazeti akamuangalia Hamad.
" Hiyo ndio habari nzima iliyopo.

Furaha aliyokuwa nayo Seid hakuweza kuijua mtu yoyote zaid yake na Mungu wake, alimshukuru sana Hamad aliefanya juu chini mpaka kueneza habari za kuuzwa matokeo ya mitihani yake, walitoka eneo walilokuwa wamesimama, wakaenda kwenye ofisi ya waziri baada ya hamad kupigiwa cm na waziri wa Elimu akiwaitaji waende.

Walipofika kwa waziri, waziri alimpongeza seid na kumpa pole pia juu ya usumbufu uliojitokeza, waliongea mambo kadhaa yaliyohusu matokeo na mipangilio mipya ya chuo. Waziri alimuahidi seid kumpatia Laptop na vitabu vyote vitavyoitajika akiwa chuo ili asije kusumbuka tena, Alishukuru sana Seid juu ya msaada huo wa Waziri, japo matokeo yake ya kuingia chuo yalipatikana lakini bado hakujua vifaa vyote vya kusomea atavipata wapi.

Cm yake ilianza kuita, Baada ya kuiangalia jina lilikuwa Ticha, Alipokea na kuanza kuongea nae, alifurahi sana baada ya kusikia sauti ya Ticha wake ikiwa katika hali ya furaha, mwisho Seid aliomba wakutane kwa ajili ya maongezi kabla hajarudi shamba.
Hawakuwa na cha zaid cha kuongea na waziri kwa muda huo, Waliitaji kumuaga wamuache aendelee na kazi za kiofisi zilizoko mbele yake, na wao warudi makwao kupumzisha akili kwani hakukuwa na chengine cha kuwafanya wazunguke mjini.
" Kijana kabla hamjaondoka, Naomba siku moja kabla ya kuingia chuo, uje ofisini kwangu, tutaongozana hadi wizarani nikakupatie vitabu, na kuhusu Laptop tufanye hivi. Alisema waziri. Alifungua droo akatoa kiasi cha pesa laki tano na nusu Akampatia Seid, Seid alipokea kwa mikono miwili

" Asante sana Waziri wangu asante sana kiukweli sina la kukulipa zaid ya kukuombea dua Ili mungu akuzidishie.
" Usijali kijana, Hiyo ni kazi yangu kiongozi wa vijana kama nyie wenye hali za chini na kuonesha nia ya kufika mbali, maana najua miaka mitatu au minne mbele utakuja kuwa mtu mkubwa serikalini au Tanzania, pita mjini ununue laptop ikusaidie katika masomo yako.
" Mimi ndio maana huwa nasema, kama wakipatikana viongozi kumi tu wakawa kama wewe, hii Tanzania yetu inanyooka.

Hamad aliongea akimuangalia waziri, Waziri hakuwa na la kuongea zaid ya kucheka, walimuaga wakatoka nje, waliingia kwenye gari na kuanza safari ya kwenda mjini wakipiga stori za hapa na pale kuondoa hali ya kusababisha ukimya.

" Seid hiyo pesa usinunulie laptop, iweke itakusaidia kwenye mambo mengine, kwa sababu nadhani tukishaingia chuo kuna vitu vingi sana itabidi ukabiliane navyo na vinaitaji pesa. Mimi nina laptop mbili, nitakupatia moja utumie mpaka pale utapo maliza. Wakiwa kati kati ya maongezi Hamad aliongea maneno hayo yaliyokuwa kama lulu kwa seid..

" Dah, kiukweli wewe ni zaid ya rafiki kwangu, huwa unapenda kumwambia waziri kuwa kama wangepatikana kumi kama yeye, lakini hata kwako kaka, wakipatikana marafiki kumi kama wewe lazima mtu uendelee.

Walipofika mjini waliongea kidogo, Wakafanikiwa kukutana na Ticha wakaongea nae ndani ya muda mfupi,  kisha Seid akapata dala dala na kurudi shamba.

Hamad alienda moja kwa moja hadi nyumbani anakoishi, akamkuta baba yake na mama yake bi Suria wakiwa wamekaa sebleni wanapata Tangawizi.
" Assalam alaykum. Alisalimia alipoingia ndani na kukaa kwenye sofa, Wazee wake walimuitikia kwa furaha, kisha kumuuliza kuhusu matokeo mapya na hali ya hewa ilivyo huko mjini mjini.

" Kiukweli namshukuru Mungu, hali ya hewa imetulia inaridhisha.
" Na vipi kuhusu Ticha? ,,Mzee shaibu aliuliza.
" Ticha ashapona, tumetoka kuonana nae muda si mrefu bado amelazwa lakini, hakuumia mno ilikuwa ni mshtuko tu.
" Mpigie cm niweze kuongea naye kama tayari anaweza kuongea, Na vipi kuhusu yule mwenzako?.
" Seid?.
" Ndio.
" Karudi kwao sasa hivi.
" Na matokeo alikuwa amepata vipi.
" Aaaah baba yule mtu si mtu mzuri, katuburuza wote kidato cha sits achana nae kabisa.
"Aisseeee.

Hamad alimpigia cm ticha na kumuambia mzee wake anamsalimia anataka kuongea na yeye, kwa bahati mbaya salio halikuwepo la kutosha, kabla ya kumpatia mzee shaibu cm ilikatika..

Baada ya kukata ukimya kidogo ulipita, Mzee shaibu ndo alianzisha mazungumzo upya alipouliza tarehe ya kuingilia chuo,  Alijibu hamad na kuendelea kuongea na wazazi wake, huku akiwaelezea namna ambavyo hatoweza kulisahau tukio hilo lililotokea la Ticha kutandikwa risasi na kamanda wa jeshi la police mr Richad, ambaye kesi yake imeishia juu juu na haikusikika tena mara tu alipofika dar kutokana na mkono wa pesa uliokuwa umemzunguka.

Seid alifika nyumbani kwao akakuta mlango umefungwa, Aliushika akautikisa na kushangaa sana baada ya kugundua umefungwa kwa ndani, alimuita mama yake bila kufanikiwa kuitikiwa, aliita tena na tena kwa nguvu bila mtu kuitika, ikabidi azunguke mpaka nyuma kuliko kuwa na dirisha, akaita mama! mama, mama Seid lakini wapi!, alirudi mbele akauangalia vizuri na kuhakikisha haujafungwa kwa nje.

" Um mbona mlango haujafungwa kwa nje huu na mama haitiki?, Mama!, Mamaa! 
Alimuita tena bila kuitikia 
" jamani ina maana mama hayumo ndani au  vipi ?


Tukutane Sehemu ya Kumi na Tatu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.