Sijutii Chelsea Kumuuza Mohamed Salah – Antonio Conte - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sijutii Chelsea Kumuuza Mohamed Salah – Antonio Conte

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amejitapa kuwa kamwe hajutii kitendo kilichofanywa na uongozi wa timu hiyo kumuuza mshambuliaji wao, Mohamed Salah mwaka 2014.

Salah mwenye umri wa miaka 25, ameondoka kwa mkopo Stamford Bridge Januari mwaka 2014 kisha rasmi mwaka 2016 wakati huo huo ambao Conte anajiunga na klabu hiyo na kusema kuwa halikuwa chaguo lake.

Hakuna mtu aliyeniuliza kuhusu yeye kwahiyo sihitaji kuhusishwa katika hili maana ningelikuwa kwenyematatizo.

Nadhani msimu huu ni bora mno kwa Salah, hapa tunazungumzia mchezaji bora. Nilimjulia Italia lakini msimu huu ulikuwa mgumu kutabiri.

Salah kwa sasa anaichezea klabu ya Liverpool ambayo Jumapili hii itasafiri hadi Stanford Bridge kuikabili Chelsea huku, Conte akiamini kuwa ushindi kwao ndiyo nafasi pekee ya kuwahakikishia wanatinga ‘top four’ kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza ili kuwa na uhakika wa kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.