Shilole Awataka Wasanii Wenzake Waolewe Ili Waache Kuzini Mwezi Huu Mtukufu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole Awataka Wasanii Wenzake Waolewe Ili Waache Kuzini Mwezi Huu Mtukufu

Msanii wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amewataka wasanii wenzake wa kike Kuolewa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ili waache kufanya zinaa.

Shilole ambaye alifunga ndoa na mume wake Ashraf Uchebe mwaka jana mwishoni ameonekana kifurahia ndoa hasa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Shilole amekiri kuwa katika mfungo wa mwaka huu, anaona raha mno kwani ndiyo kwa mara ya kwanza umemkuta ndani ya ndoa na amekuwa akifunga na kufanya dua na mumewe tofauti na miaka mingine ambayo alikuwa hajaolewa, alikuwa akilegalega kufanya sala na kufunga.

"Huu ni mfungo wa kipekee kwangu kwani ndiyo kwanza umenikuta ndani ya ndoa, kiukweli ninajisikia raha mno ambayo sikuwahi kuipata awali".

Lakini pia Shilole aliwataka mastaa wa kike ambao hawajaolewa wajitahidi waolewe na waachane na kuzini kwa sababu dua zao ndipo zitakapopokelewa pia anawaombea ili wapate waume wema kama yeye alivyopata mume mwema anayemuongoza katika njia nzuri ya kumjua zaidi Mwenyezi Mungu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.