Shamsa Akiri Kuumizwa na Harmonize - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shamsa Akiri Kuumizwa na Harmonize

Muigizaji wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amekiri kuumizwa na kitendo cha Harmonize kumuhusisha mume wake katika ugomvi wake na ex-girl friend wake, Wolper.

Utakumbuka wiki iliyopitia katika kurushiana maneno kati ya Harmonize na Wolper, mume wa Shamsa Ford, Chid Mapenzi alitajwa na Harmonize katika orodha ya wanaume 12 aliodai wametoka kimapenzi na Wolper.

Sasa Shamsa amesema si kwa mume wake pekee bali hata mtu wake wa karibu anapozungumzwa kwa ubaya huwa anaumia.

“Lazima uumie ukiwa kama binadamu hasa kwa mtu ambaye unampenda sio lazima kwa mume kwa mtu yeyote ambaye unampenda, yupo katika sehemu ya maisha yako lazima ujisikie vibaya,” amesema Shamsa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.