Sad News: Nyumba ya Joti Kubomolewa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sad News: Nyumba ya Joti Kubomolewa

Habari zilizosambaa leo asubuhi katika mitandao ya kijamii na katika magazeti ni kuhusu nyumba kubwa ya Joti, msanii wa vichekesho na msanii anaetumika katika matangazo mengi ya kijamii hasa kutokana na ukubwa wa kazi zake na umbo lake linalomfanya kuwa na uhuru wa kufanya kitu chochote.

Nyumba hiyo ambayo bado ni mpya , inasemekana kubomolewa huku picha zikiwa zimesambaa msanii huyo akiwa na baadhi ya maafisa wa polisi akiwa anazungumza nao huku nyumba hiyo ikionekana kuwa na michoro ya x ikimaanisha kubomolewa.

Hata hivyo, wadau na watu mbalimbali wameshauri kuwa pale watu wanapotaka kununua kiwanja au nyumba ni bora kuuliza kwa undani eneo hilo unalonunua linakuwa na matumizi gani ya kijamii isije kuwa kama haya yaliyomkuta Joti kuwa hakuwa anajua kama ni eneo la barabara.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.