Rayvanny Kumuoa Fahyma Hivi Karibuni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rayvanny Kumuoa Fahyma Hivi Karibuni

Mwanamuziki Rayvanny amefunguka na kusema kuwa anatarajia kumuoa mama wa mtoto wake mmoja wa kiume anaejulikana kama Fayhma ambae amekuwa nae kwa muda mrefu na kubahatika kupata mtoto mmoja.

Rayvanny anaongea hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Dizzim Online katika uzinduzi wa filamu ya Mama ya Aunty Ezekiel wikiend iliyopita na kusema kuwa pamoja na kwamba hivi karibuni wawili hao walienda mpak mbeya ambako ndio nyumbani kwa msanii huyo lakini bado hayuko tayari kusema ni siku gani atafunga ndoa lakini mungu akijalia siku yoyote watafunga ndoa.

"Yeah, Mungu akijalia tutafunga ndoa lakini siwezi kusema ni lini kwa sababu hivi vitu vinapangwa na Mungu lakini pia na familia,ndugu mkishapanga na ikiwa official mtajua tu."

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.