Q Chillah Afunguka Mazito Kuhusu Kuacha Muziki “Sijaja Kwenye Muziki Kwa Kiki” - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Q Chillah Afunguka Mazito Kuhusu Kuacha Muziki “Sijaja Kwenye Muziki Kwa Kiki”

May 22, 2018 Muimbaji Q chillah amefanya mahojiano Clouds FM kupitia kipindi cha XXL kinachoruka kwa masaa matatu kuanzia saa 7 kamili mchana mpaka saa 10 jioni na kwenye mahojiano hayo Q chillah amezungumza mambo mbalimbali kuhusu kuacha mziki na haya hapa ni baadhi ya mambo hayo.

Nakupa nafasi ya kuyapata mambo haya aliyoyazungumza msanii Q chillah kama hukupata bahati ya kusikiliza Radio ni time yako kuyajua hapa.

“Asante kwa CMG, Ruge, Joseph Kussaga na Mkewe, maamuzi haya hayakuwa rahisi nimechukua muda mrefu kufikiria mpaka kuamua lakini naamini sasa ni wakati sahihi kuachana na muziki nimemshuhudia Ruge akiwanyanyua watu waliochini kabisa, waliokata tamaa ya maisha, mfano Mama Saida Kalori alikuwa ameanguka, Ruge alimchukua na kumuinua na akafanikiwa kurudi tena na sasa amesimama imara.”
“Kinachoniuma naacha muziki nikiwa naona bado naona nafasi yangu kwenye muziki, nasikiliza nyimbo zinazopigwa bado naona ningeweza kupita katikati yao na kutengeneza barabara yangu.”

“Kinachonitafuna mimi ni mimi mwenyewe, maisha yangu ya nyuma yananihukumu. Lakini I don’t want to be a prisoner of my past, Sio mara ya kwanza kutangaza kuacha muziki lakin kipindi kile bado nilikuwa natumia drugs Sikuwa sawa lakini sasa nimepona, nipo sawa naongea haya nikiwa na utimamu wa akili na mawazo niliyoyapitia ni magumu, makosa niliyoyafanya yanaathiri ndoto zangu hayawezi kukatisha ndoto”

“Tangu nimetangaza kuacha muziki, nimeona mapenzi ya watanzania nimeona mahaba yao, mpaka nimejiuliza tatizo sio support ya watanzania, labda ni mimi, au sikupata msaada niliohitaji ili kufanikisha maendeleo ya kazi yangu.”

Lakini pamoja na hayo amejitokeza mtu ambaye amefanya mazungumzo na Q chillah na kisha kukubaliana asiache muziki na watafanya naye biashara kuhakikisha muziki wake unamlipa na leo ameachia wimbo mpya unaoitwa Saratani.

”Ninawimbo mpya unaitwa SARATANI asante sana Tanzania Nimeguswa sana na sijaja kwenye mziki huu kwa njia ya kiki kwanza hata Smart Phone sina ila nawapenda sana” – Qchila

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.