Penzi la Aslay na Mama Mtoto Wake Ladaiwa Kuvunjika - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Penzi la Aslay na Mama Mtoto Wake Ladaiwa Kuvunjika

Kumekuwa na tetesi huko instagram kuwa msanii Aslay na mke wake ambae amebahatika nae kupata mtoto mmoja kuwa kwa sasa hawapo tena pamoja na kwamba wawili hao kila mmoja anafata ustaarabu wake kwa sasa na inawezekana hata kukaa pamoja hawakai tena.

Wikiendi hii ilikuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa wawili hao huku siku zao zikiwa zimefatana lakini kitu cha ajabu ni kwamba hakukuwa na shamrashamra za sherehe hiyo kwa wote wawili huku Aslay hakutaka hata kuweka picha ya mzazi mwenzake huyo katika ukurasa wake wa instagram.

Habari ziliozpo chini ya kapeti ni kwamba Aslay na Tessy hawako pamoja tena na kwamba mwanamke huyo alishaondoka nyumbani kwa Aslay na sasa wapo katika mahusiano kama ya wazazi tu na sio vinginevyo.

Wasanii wengi wamekuwa na skendo za kuwa na mapenzi ya muda mfupi na pengine hata kushindwa kufikia muafaka wa ndoa kwa wapenzi wao huku swala kubwa likihusishwa na wivu wa mapenzi na kulewa umaarufu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.