Nyashinski Ufafanua Ujumbe Wake Mbaya wa Twitter Aliomtaja Diamond - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nyashinski Ufafanua Ujumbe Wake Mbaya wa Twitter Aliomtaja Diamond

Unaukumbuka ujumbe wa Twitter ambao ulidaiwa kuwa wa Nyashinski ambapo ulikuwa unasema kuwa Diamond hajui kutengeneza hit song? Basi msanii huyo ameamua kufunguka kuhusu ujumbe huo.

Hilo lilitokea ikiwa ni siku chache zimepite baada ya Diamond kutumia mtandao wake wa Instagram kumpigia debe kwa mashabiki na watu wote Afrika Mashariki tuungane katika kumpigia kura Nyashinski katika tuzo za MTV EMA alizochaguliwa kuwania mwaka jana.

Akiongea na Lil Ommy TV, Shinski amesema ujumbe huo haukuwa wake na wala haukutumwa kupitia akaunti yake ya Twitter. “Wacha niweke very very clear, Twitter account yangu ni Realshinski sio official au Thereal. Ukiangalia hiyo tweet ilitoka kwenye Twitter nyingine,” amesema msanii huyo.

“Unajua unaweza kuwa na watu wengi Twitter wanajiita Nyashinski. So nikaona acha niweke sawa, hiyo tweet ilikuwa inasema Diamond hajui kumake hits, wote tunajua Diamond anajua kumake hits. Hiyo kwanza haikuwa kweli , hiyo haikuwa tweet yangu,” ameongeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.