Nyanshinski Kuja na Kolabo Yake na Jux - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nyanshinski Kuja na Kolabo Yake na Jux

Staa wa Muziki kutoka 254 Kenya Maarufu kama Nyanshinski aliyewahi kutamba na kibao chake cha ‘Malaika’ ametangaza ujio wa Kolabo Yake na msanii wa Bongo fleva Juma Jux.

Nyanshinski alifunguka hayo Kwenye mahojiano na BBC alipokuwa anaongelea ujio wake wa Kolabo mbali mbali alizofanya na wasanii mbali mbali kutoka Africa Mashariki.

"Lakini nimefanya kolabo na Jux tunangoja tu itoke”.

Lakini pia Nyanshinski aliwataja baadhi ya wasanii ambao amesha fanya nao kazi kutokea Tanzania ni kama msanii mkongwe Ay ambaye ameweka wazi kuwa ngoma yao ipo Kwenye Mtandao wa Youtube tayari.

"Nilifanya kolabo moja na AY ilikuwa inaitwa ‘More in More’ ukiitafuta YouTube utaiona”.

Nyanshinski ameweka wazi kuwa kwa hivi sasa anaangalia zaidi kufanya kazi na wasanii kutoka Rwanda na Uganda kwani hajawahi kabisa kushirikiana nao.

Lakini pia Nyanshinski Aliweka wazi kuwa yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa label ya WCB ili aweze kufanya nao kazi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.