Nay wa Mitego: Kwa Sasa Mimi Sina Mpango wa Kuoa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego: Kwa Sasa Mimi Sina Mpango wa Kuoa

Kumekuwa na tetesi zinazo sambaa katika mitandao kwamba msanii Nay wa Mitego kwa sasa ana mpenzi mpya ambae ni mzuri na mkali zaidi ya yule mama wa watoto wake aliyewahi kuwa nae mara ya kwanza aliyejulikana kama Siwema.

Akiongea huku akikataa jina lake kutowekwa wazi, moja ya mapaparazi alisema kuwa kwa sasa Nay ana chombo kipya kizuri kuliko hata Siwema aliyekuwa nae mwanzo,’hivi mna habari kuwa Nay sasa hivi ana chombo kipya kisu kuliko Siwema, ni mjasiriamali na anakaribia kumuoa na mara nyingi anakuwa nae pale Kimara nyumbani kwake.’

Mimi nakuibia siri ya familia kwa sababu huyo dada amechukua sehemu kubwa ya Siwema kwa hio wamemwambia kuwa lazima amuoe huyo dada.

Baada ya hapo Nay alitafutwa ili kuweka ukweli juu ya jambo hilo na kutuweka wazi kuhusu kila kitu kuhusu mahusiano yake, ndipo Nay alipojibu kuwa kwa sasa hana mpango wa kuoa.

Sina mpango wa kuoa mimi, na mmepata wapi picha,sema kwanza picha umezitoa wapi na nani kakutumia ndipo nitakujibu kama ni mpenzi, mchumba au vipi.

Mimi huyu sio mwanamke wangu aisee, mimi nina mahusiano yangu mengine kabisa.

Hata baada ya kuulizwa hivyo Nay wa Mitego hakutaka kujibu tena swali lingine lolote zaidi ya hilo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.