Nandy: Nilitaka Kuacha Muziki Kisa Video Chafu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nandy: Nilitaka Kuacha Muziki Kisa Video Chafu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy amefunguka na kudai alikuwa tayari kuacha muziki baada ya ile video yake chafu kuvuja kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki chache zilizopita Nandy aliwaacha watu midomo wazi baada ya video yake iliyomuonyesha akiwa kitandani na aliyekuwa mpenzi wake Billnas kivujishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Nandy amekiri kutaka kuacha muziki kwenye mahojiano na Kipindi cha leo Tena cha Clouds Fm ambapo amezidi kufunguka haya:

"Nilihisi kukata tamaa kuachana na muziki kabisa sikuona maana ya maisha. Lakini nilipofika BASATA walinipa ushauri na kunihoji binafsi sikuwa na picha mbaya nyuma katika maisha yangu kama kweli nilivujisha picha zile kwa ajili ya Kiki.

Hali yangu ilikuwa mbaya sana nilipoona ile video sikuamini kabisa macho yangu. Nilizidiwa na Pumu nikakimbizwa hospitali kifupi nilipata Brain Attack niliwaza kuhusu familia yangu nItamtazamaje mama na baba yangu?".


Nandy jana aliachia wimbo wake mpya ulioandikwa na msanii mwenzake Aslay unaoitwa Ninogeshe.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.