Nandy Apoteza Kilo 5 Kisa Video ya Utupu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nandy Apoteza Kilo 5 Kisa Video ya Utupu

Ukitaja wanamuziki wanaokuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva, huwezi kuacha kutaja jina la mwanadada Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’. Mrembo huyu anaonekana kuwa tishio kwa sasa.

Nandy ana sauti tamu ya kumtoa nyoka pangoni.

Pamoja na misukosuko aliyokutana nayo juzikati baada ya kuvuja kwa picha zake za chumbani, lakini bado ameweza kuangusha bonge la ngoma inayokwenda kwa jina la ‘Ninogeshe’.
Baada ya kupitia kwenye misukosuko hiyo na kuachia ngoma hiyo, Nandy amepata chansi ya kufanya mahojiano ya Over Ze Weekend na kufunguka mambo kibao kama ifuatavyo;
Over Ze Weekend: Pole sana kwa misukosuko ya hapa na pale ambayo yamekufanya utulie kidogo.
Nandy: Nimeshapoa na maisha yanaendelea sasa.
Over Ze Weekend: Skendo iliyokupata imekuathiri vipi?
Nandy: Iliniathiri kwa kiasi kikubwa sana, lakini ninashukuru kuwa na watu sahihi nyuma yangu ambao wamenifanya niwe na amani tena.
Over Ze Weekend: Ni kitu gani ulikipoteza kwa kipindi hicho?
Nandy: Kilo zangu, maana nilikuwa na kilo 47, tano zote zikaondoka kwa ajili ya mawazo.
Over Ze Weekend: Kipindi kidogo cha nyuma ulikuwa huwezi kutoka bila kuvaa dela kubwa na miwani vipi sasa hivi?
Nandy: Sasa hivi ninavaa kawaida tu. Siwezi kuvaa tena kama wakati ule.
Over Ze Weekend: Vipi mchumba wako alilichukuliaje suala hilo? Maana ndiyo ninasikia anatarajia kukuoa soon?
Nandy: Unajua yeye ananifahamu mimi vizuri sana na anajua vyema zile picha ni za lini na kwa vile ni muelewa sana, aliona ni jambo ambalo litapita tu kama mengine.
Over Ze Weekend: Vipi kwa upande wa ndugu zake sasa?
Nandy: Hawana shida, kila kitu kipo sawa tu.
Over Ze Weekend: Ngoma yako mpya ya Ninogeshe ni bonge moja la ngoma, je, umeandika mwenyewe?
Nandy: Hapana, hiyo ngoma ameniandikia Aslay.
Over Ze Weekend: Umekuwa na ukaribu mkubwa sana na Aslay kiasi ambacho watu wameanza maneno, unaliongeleaje jambo hilo?
Nandy: Hakuna chochote kwa sababu tumefanya kazi nyingi pamoja na tumezoeana sana. Hakuna chochote kianachoendelea kati yetu.
Over Ze Weekend: Hivi karibuni tuliona umevuta ndinga jipya, je, ni la kwako? Isije ikawa kadi ipo kwa mwenyewe?
Nandy: Hapana, ni la kwangu, kwani siyo gari langu la kwanza ila tu zimezidiana uzuri.
Over Ze Weekend: Kama umeweza kununua
 gari zuri na la tha-mani hivi, vipi kuh-usu nyu-mba?
Nandy: Nyumba ninayo tayari, soon watu wataiona.
Over Ze Weekend: Najua una kipaji kingine cha ushonaji, vipi unaendelea nacho au muziki ndiyo umechukua nafasi kubwa?
Nandy: Hapana, vyovyote niko navyo maana ukiangalia hata Wimbo wa Ninogeshe, nguo zote ni mimi ndiye nimeshona na kudizaini.
Over Ze Weekend: Mchumba wako anayetarajia kukuoa ni mtu maarufu au?
Nandy: Sitaki kuzungumzia ni mtu wa aina gani, lakini ananifahamu sana tu.
Over Ze Weekend: Vipi ishu ya kuzaa hivi karibuni?
Nandy: Mtoto sasa hivi bado, ila ndoa ndiyo itaanza kwanza.
Over Ze Weekend: Ni kitu gani unacho-kitamani umeki-misi?
Nandy: Kupanda daladala.
Over Ze Weekend: Asante, nakush-ukuru sana.
Nandy: Asante sana, nawap-enda waso-maji wa Gazeti la Ijumaa Wikie-nda.

IMELDA MTEMA

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.