Mtoto wa Msogange Azikataa Shule - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mtoto wa Msogange Azikataa Shule

Mtoto wa video queen maarufu bongo Agnes Masogange ambaye amefariki mwishoni mwa mwezi uliopita,Sania Shaaban, amekataa kusoma shule za bweni ambazo ameahidiwa kusomeshwa na wafadhili, na kutaka kusoma shule za kutwa.

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bogno ya East Africa Radio, Sania amesema hataki kukaa mbali na shangazi zake ambao ndio wanamlea, na hajazoea shule hizo.

“Napenda kukaa nyumbani kwa sababu nitawamisi shangazi zangu, shangazi zangu wote nawapenda na sijawahi kukaa mbali nao”, amesema Sania.

Kwa upande wa shangazi zake ambo wanamlea Sada na Samia wamesema mtoto huyo hajawahi kukaa mbali na wao, hivyo suala la kwenda kusoma shule za bweni itabidi lifikiriwe kwanza kwa ajili ya usalama wake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.