Mke Wa P Funk Agoma Kumuacha Kajala Awe Mama Mwenye Nyumba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mke Wa P Funk Agoma Kumuacha Kajala Awe Mama Mwenye Nyumba

Mke wa Prodyuza maarufu na mkongwe kwenye mziki wa Bongo fleva P Funk majani, Samira ameibuka na kudai atapambana na Kajala na kamwe hatamuachia nyumba.

Kwa Miezi kadhaa Kumekuwa na tetesi kuwa P Funk na Ex wake ambaye pia mama watoto wake aliyezaa naye mtoto mmoja Kajala wamerudiana kitu kinachomuweka Pabaya mke wa Pfunk ambaye hivi sasa ni mjamzito.

Samira ambaye wiki iliyopita ilisemekana alikuwa tayari kumuacha Pfunk na kurudi kwa wazazi wake Arusha, inadaiwa ameamua kupambana na Kajala na kukataa kumuacha Kajala amchukue mumewe.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Samira ameongea kwa uchungu huku akidai kila siku huwa anaumizwa pale anapokutana na kashfa kumuhusu mume wake na Kajala lakini ameamua kubaaki kupambana.

"Yaani mateso ninayokutana nayo kwenye ndoa yangu ni Mungu pekee ndio anajua tena kwenye hali hii ya ujauzito niliyo nayo, awali nilipanga niondoke nimuachie nyumba lakini nimeona nikomae hadi kieleweke".

Mara nyingi Kajala alipokuwa akiulizwa kuhusiana na kuingilia ndoa hii ya mzazi mwenzie amekuwa akikana mara na kusema kuwa kuwa P Funk ni baba wa mtoto wake na si vinginevyo ingawa video mbalimbali zinavuja zikiashiria ni wapenzi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.