Mfahamu Video Queen wa Kwanza wa Diamond Katika Wimbo wa Nenda Kamwambie - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mfahamu Video Queen wa Kwanza wa Diamond Katika Wimbo wa Nenda Kamwambie

Ni miaka mingi imepita tangu mwanamuziki Diamond Platnumz atoe wimbo wa nenda kamwambie ambao ndio wimbo wake wa kwanza na uliomtambulisha katika tasnia ya muziki, Lakini inawezekana kabisa ni wachache wanaomjua yule video queen aliyewahi kutokea katika wimbo wake ule wa kwanza.

Basi siri kubwa ambayo inawezekana ni wachache wanaijua na inawezekana wengi hawakuwahi kuigundua ni kwamba mwanadada ambae ni video queen kwenye video ile ni dada yake kabisa na Diamond Platnumz anaejulikana kama Esma Platnumz kwa sasa.

Akitoa sababu ya kumtumia Esma, Diamond aliwahi kusema kuwa kipindi kile alikuwa hana pesa na wadada wengi walimringia na kukataa kufanya nae video kwa sababu alikuwa hana pesa na walikataa kufanya bure hivyo ilimlazimu kufanya na Esma kuepusha gharama.

Lakini ndio huyo Diamond ambae sasa kila mtu anatamani kufanya nae kazi, hata siku moja hupaswi kumdharau mtu usiyemjua na kujua kusudi la Mungu ndani yake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.