Mayweather Amzawadia Mwanaye Pete ya Tsh Bilioni 11 Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mayweather Amzawadia Mwanaye Pete ya Tsh Bilioni 11 Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa

BONDIA maarufu duniani, Floyd Mayweather amemfanyia kufuru mtoto wake, Iyanna ‘Yaya’ baada ya kumnunulia pete ya almasi yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 5 (zaidi ya shilingi bilioni 11 za Kibongo) katika siku yake ya kuzaliwa ‘bethidei’.

Kwa mujibu wa Mtandao wa TMZ, Mayweather amekuwa akimpenda Yaya kuliko pesa na marafiki. Mayweather alimkabidhi Yaya pete hiyo katika bethidei ambapo alikuwa akitimiza miaka 18. Hata hivyo, baada ya kutupia mtandaoni aliandika kuwa amekuwa akipenda kuiangalia mara kwa mara na wala hachoki.

Hii si mara ya kwanza kwa Mayweather ‘kumsapraizi’ Yaya katika siku yake ya kuzaliwa kwani alipotimiza umri wa miaka 16, aliwaalika wakali wa Hip Hop, Drake na Future kwa ajili ya kumuimbia huku pia Justin Bieber naye akialikwa kumtungia Yaya wimbo maalum.

Inakumbukwa kwamba, Yaya alipotimiza umri wa miaka 14, Mayweather alimzawadia gari aina ya Mercedes 550 S-Class.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.