Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 16) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 16)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mw/Mtunzi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 16

Seid hakuitaji kuiangalia cm yenyewe, iliita mpaka mwisho bila kujua nani kapiga, ilipokuwa tayari imekata aligeuka upande ilipo cm, aliishika akaangalia nani kapiga jina likaja raya, moyo wote uliripuka, cm ikaanza kuita tena jina likiwa hilo hilo,  hakusubiri, akapokea haraka moyo wake ukiwa  una dunda, aliiweka sikioni na kusikiliza kitachoongelewa upande wa pili.

" Seid! ,, Aliitwa kwa sauti nzuri ambayo si ya mpayuko.
" Yes Raya! ,, aliitika kama mtu mwenye woga.
" Kwa nini hukunambia tokea mapema kuwa unaniitaji kimapenzi?

Alikosa la kujibu Seid, akakaa kimya zaid ya sekunde kumi akiwa anatafakari swali aliloulizwa.
" Nadhani kwa sababu nlijua sitokubaliwa, ila baada ya kuona nna mapenzi mazito juu yako imenibidi niseme tu nijue mbichi yangu na mbivu.

aliongea kwa sauti ya chini, kuhofia mama yake asije kumsikia, kiupepo cha chini chini kilichokuwa kinapiga muda huo na hali ya hewa kutulia vilimfanya Sauti izidi kuwa nzito, na ipendwe kusikika kwenye masikio ya mtu yoyote.

" Seid nadhani nimekaa na wewe muda mrefu, hukupaswa kuogopa kiasi hicho ,, kama nkikuambia niko tayari kuwa na wewe utaamini?

Moyo wote wa Seid ulipasuka kama mtu alieona kitu cha kushangaza baada ya kusikia maneno hayo, Tabasam zito lilimjia, akabakia mwenye kushangaa maneno ya Raya.

" Seid nakuuliza mbona umekaa kimya?

Aliuliza Raya baada ya kuona mtu kakaa kimya, Raya muda mrefu sana alikuwa anamkubali  seid, alimpenda tokea alipomuambia ukweli wa maisha yake yote, alijaribu kujiweka nae karibu ili itokee siku moja seid amwambie nakupenda, upo muda alitumia njia za kumuonesha kuwa anampenda lakini seid bado hakushtuka kutokana na kuwa mbali na mapenzi tokea azaliwe.

" Sijui kama ntaamini kiukweli ila nadhani ntaamini kwa sababu maneno yatakuwa yanatoka kinywani mwako.

Raya alitabasam aliposikia maneno ya Seid.
" Basi usijali, nakuruhusu uniite mpenzi wako kuanzia leo, Wanadam tumeumbwa na mambo matatu muhimu, mimi kama mwanamke sioni kinachoweza kunifanya nisikukubalie Seid wakati sina mtu na wewe ni kijana mzuri na unapendeza.

Hakuamini Seid kusikia maneno hayo kwa Raya, alihisi labla uenda yuko ndotoni au anataniwa.

" Are you Serious Raya!!? 
alimuuliza kwa mshangao, Raya hakuwa na la kumjibu zaid ya "Yah" Seid bado aliona kama ndoto ya pata potea, alijiuliza kwa nini amekubaliwa haraka namna ile, ila hakuwa na cha kuongezea zaid ya kusema ,,, " Nashkuru sana Raya kama ukisemacho ni cha kweli, Nakuahidi kukupenda maishani mwangu mwote, sitothubutu kukuumiza, naapia mbele ya Mungu wangu.

Alicheka kidogo raya ,," Seid usiseme hivyo, siku hizi sisi wanawake ngumu sana kuamini maneno ya mwanaume kutokana na kutuongopea sana mpaka mtuweke ndani, Ila nashukuru kama maneno hayo ni ya kweli, namuomba Mungu tu yasije kwenda kinyume.
" I swea naapia raya namna ulivyonitoa kijasho sikuachi maisha yangu yote, moyo wangu mweupe sasa nashkuru sana kiukweli.
" Ok my seid, ,, so niache nilale  basi kwa sababu usiku ushakuwa mkubwa then nalala na mama.
" Oooooh ,,unalala na mama yako?
"Yah ,, sasa hivi niko naangalia movi ukumbini, ila badae natoka na kuingia chumbani.
" Ok Good naa kwa nini usilale peke yako.
" Naogopaaaa mwenzio.

Raya alimkiss seid na kukata cm, Seid hakuamini kilichotokea, alifumba macho kisha akayafumbua huku mdomo ukitabasam.
" Yes!! hapa hata usingizi utakuja.

alijigeuza akalalia ubavu huku akitafakari kilichotokea, Raya maisha yake yalikuwa ya kizungu zungu hakuitaji kumwambia mara subiri nifikirie kama ilivyo kawaida ya madada wengi wa kitanzania.

" Kweli mapenzi ni upofu ambao unakuwa unaona unakoenda lakini unapamia vichakani, yani kijasho kimenitoka, moyo umenienda mbio buuuure kumbe mambo yalikuwa rahisi tu, Ah! Rayaaaaaaa!!!!.

akiwa anaendelea kuwaza message iliingia katika cm yake, aliifungua na kuiangalia , ulikuwa ni ujumbe mzuri toka kwa raya, moyo wake ulijawa na furaha baada ya kuisoma, meno yote mdomoni yalitoka nje, alikuwa kama chizi muda huo, aliiangalia tena na tena message mwisho akachumu screen ya cm mmwwwaaaaa Rayaaaa! sitaki hata kukujibu nkaja kuaribu ,, aliweka cm pembeni na kuanza kutafuta usingizi huku akijikuta anatabasam akiwa amefumba macho kila akikumbuka kilichotokea muda si mrefu mpaka alipopata usingizi.

********
Ticha alipiga usingizi kwenye kibaraza cha nyumba yake, mbuu walimshambulia sana, hakuweza kuwasikia kwa sababu ya kujawa usingizi.
Usiku wa Saa nane na nusu, Rahma aliamka akamfata Ticha mmewe alipokuwa amelala, alifika akasimama kichwani kwake, akaanza kumpiga kwa mguu huku akisema "Wewe, Wewe.

Ticha alishtuka akiwa kwenye usingizi mzito, aliangalia huku na kule akamuona mkewe, moja kwa moja alijua balaa linataka kuanza, alijifanya hajamuona akalala tena.

" Hujaniona au?
aliuliza rahma, Ticha hakujibu, ndipo Rahma alisogea upande wa pili nae akalala.
Ticha ilibidi aamke baada ya kumsikia mkewe akiwa amelala nyuma yake.

" Hivi mke wangu unataka nini lakini!, umenitoa ndani nkakubali na huku pia jamani! Mbona huna hata uruma!. ,, Ticha aliongea akionekana kuchukia.
" Nataka kulala na wewe mme wangu nna hamu mwenzako.
Aliongea rahma kwa sauti ya chini, Ticha alimuangalia akaachia msonyo, Rahma alionekana mwenye hisia kali za mapenzi muda huo, alimsogelea Ticha akaanza kumpapasa.
" Naomba uvue nguo unipatie nnachokiitaji pliiz beiby ,, alisema rahma.

' Dah ningejua mambo yenyewe haya nisingearakia kuoa mimi akyamungu yani mtu mzima hadi nataka kulia, manyanyaso gani haya nayapata mimi saa tisa yote hii mtu anakuamsha Aaah...
Ticha aliongea peke yake moyoni, alikumbuka maneno ya docta ,,,,,  mheshimiwa mkeo kwa hali hii aliyonayo akiitaji hata game saa tisa usiku inabidi ukubali laa sivyo utazua balaa.

" Naomba twende ndani basi.

baada ya kukumbuka maneno ya docta ilibidi akubali tu, akamuomba waende ndani ampatie kile anachokitaka.
" Eeee ndani? ,,Rahma aliuliza kwa mshangao.
" Sasa unataka tufanyie hapa!?
" Ndio. 
" Ebu mke wangu mlaani shetani usiwe hivyo basi naomba tuingie ndani tafadhali.
" Sitaki nataka hapa kwani lazima? ,, aliongea akionekana kukasirika tayari.

DAH! MATESO GANI NAYAPATA MIMI HAYA JAMANI!? KWELI HILI ENEO LA KUFANYIA NGONO HILI SI KUONDOA BARAKA NDANI YA NYUMBA HUKU?

aliwaza ticha akiwa amemuangalia mkewe, Rahma nae alikuwa amemlegezea jicho muda huo.
" Ebu naomba twende ndani mke wangu pliz.
" Rajab naomba usinitibue, kama hutaki sema.

Alichange ghafla Rahma baada ya kutumia upole aliamua kutumia nguvu, Ticha hakuwa na namna alivua surual yake na boxa akabaki mtupu, Rahma alitoa khanga yake akalala chali, akiachia mapaja ili mmewe apite.

" Tena uniniu vizuri hapo, si ufanye kiusingizi singizi, umshike na mtoto wako ,, aliongea akiachia tabasam la utani kwa mmewe.

Safari ya ghafla ndani ya usiku mnene Ilianza, Rahma alikuwa ana hisia kali sana muda huo, zilimfanya afike haraka alipokuwa anataka kufika kabla ya Ticha ndani ya muda mfupi.

" Hujamaliza tu?

Rahma aliuliza, hisia zake tayari zilishakata baada ya kukipata alichokuwa anakitaka.
Ticha nae muda huo alikuwa yuko hoi, alishachizika kwa tendo analolifanya, hasa sehemu aliyokuwa anaelekea kuwa si nzuri kimazingira.

" Jamani bado!, Ah?

Aliuliza tena Rahma, Ticha alishindwa kujibu kutokana kuwa kama chizi kwa raha anazopata muda huo, Mwisho Rahma alishindwa kuvumilia baada ya kuona mtu anaenda tu, alimshika kwa nguvu na kumchomoa, akainuka alipokuwa amelala akiachia msonyo na kuingia zake ndani. ,," Na hunipati tena ng'oo! we mtu nimekuachia kidogo tu unafanya misaa kibao lione!.

Ticha alibaki chini katika hali ya mshangao, namna alivyojisikia alitamani kuua mtu, machozi taratibu yalianza kumtiririka, alisononeka sana jamaa kwa kukatishwa safari yake iliyokuwa ikielekea mwisho, aliumia zaid ya sana, ni kama alizichezea hisia zake, alianza kuangua kilio kama mtoto kwa uchungu aliokuwa nao, ni zaid ya unyama aliokuwa amefanyiwa na mkewe, ila alibaki na jibu la ntafanyaje.

HIVI NINI HIKI KINANIKUTA MIMI!?, HUU SI UUAJI JAMANI HUU!, YANI MTU KWELI UNAMKATISHA HISIA ZAKE BILA HATA HURUMA!, KWA NINI LAKINI? BORA SASA NINGEKUWA MWANZO ,, NDO NAKARIBIA KUMALIZA NASIKIA KABISA ZINAKUJA MTU ANANITOA KWA NINI LAKINI JAMANII! AH, Eh Mungu nihurumie basi mimi nateseka mja wako.

Aliongea peke yake kwa kunung'unika, akainuka akazunguka nyuma ya nyumba kulikokuwa na bomba, akafungua maji na kujisafisha uume wake, kisha akarudi kwenye mkeka. alivaa nguo zake akalala, usingizi ulimchukua mpaka saa mbili asubuhi ambapo alishtuka akamkuta mkewe akiwa anachambua maharage pembeni yake.

" Morning my Husband.

Rahma alimsalimia baada ya kumuona mmewe ameshtuka.
" Morning too how are you
" Am fine and you?
" am okey too mbona hujanishtua sasa kumbe kushakucha?
" Mi nliona bado una usingizi, nkaona nikae pembeni ya my hasband nimlinde asije kuibiwa.

Ticha alivyomuangalia akajua mashetani ya mimba yake yatakuwa yametulia muda huo.
" vipi niingie ndani nkaswaki? 
" Hee Mme wangu!, hii si nyumba yako jamani, unaniomba mimi kuingia ndani tena.

Hakuwa na la kuongeza aliingia ndani kwa ajili ya kuswaki.

" Kiukweli kwa hali hii ukizaa huyu mke wangu inatosha, maana! hii ni too mach sasa, na angekuwa mwanaume mwengine angeshakutia makofi kwa jinsi unavyouzi, kwanza kwa kitendo ulicho nifanyia usiku, niko nakaribia kufika unanikatisha, aaaaaaah angekuwa mwengine hakubali, hajali cha mimba wala nini tia makofi endelea na kazi.

Aliongea na moyo wake ticha akiwa anaingia ndani.

********
Seid alikuwa bado amelala kutokana na uchovu aliokuwa nao, Bi najma baada ya kuandaa chai alimuamsha ili wapate chai kwa pamoja. 
aliamka akatoka nje kupiga mswaki kisha akarudi wakaanza kupata chai huku wakiongea.

Baada ya kumaliza seid alichukua vitabu na kuanza kusoma, akipendelea kusoma sana vitabu vya waandishi wa mashairi au wa misemo, methali, mafumbo pamoja na misamiati mara kwa mara.
Akiwa yuko anasoma vitabu vyake cm iliita, kuangalia kwenye screen jina lilikuwa ni raya, aliachia tabasam akashika cm na kupokea.
Walisalimiana, wakajuliana hali, waliambiana baadhi ya maneno mazuri ya mapenzi, walichukua zaid ya dakika sita  kuongea, kisha Raya alikata cm akimalizia na maneno I Love You Seid.

Seid alijihisi yuko katika dunia yenye salama na Amani, Huku akihisi kunenepa kabisa ghafla kwa kuingia kwenye mausiano na msichana aliehisi ndie chaguo lake.

Ilipofika jioni jioni alifunga safari akaenda kwa bibi yake, alipokelewa vizuri baada ya kufika kwa sababu hakuonekana muda mrefu, bibi alifurahi zaid baada ya kupokea zawadi ya mawasiliano kutoka kwa mjukuu wake, walitaniana kama bibi na mjukuu, wakaongea mengi na kuombeana dua, ilipoingia saa moja moja Seid alimuaga bibi na kuanza safari ya kurudi nyumbani.

********
Siku zilisonga mbele, muda wa kurudi chuo ulikaribia, mawasiliano yalizidi kuwepo kati ya Seid na Raya, huku wakifanya juu chini kuhakikisha wanauweka karibu uhusiano wao kwa kutumia njia ya cm,  wakipeana maneno mazuri kila kukicha na kuhadisiana hisia zao zilivyo, kuhadiana mengi pindi watapoonana kutokana na kila mmoja kuwa na hamu na mwenzake....

Matatizo kwa upande wa Ticha yaliendelea kila kukicha, ulifika muda alihisi uenda kuna kosa amelifanya ndo maana anaadhibiwa kiasi kile, haiwezekani mkewe akawa mtu wa kumnyanyasa kila leo kisa mimba, Tena katika nyumba yake mwenyewe.
Alivumilia lakini ilifika muda akahisi amechoka, kila alipopiga hesabu na kuona mimba ndo kwanza ina miezi saba alijikuta Anadata, miezi miwili iliyobaki aliiona kama mwaka.

" Naamini hii ni adhabu tosha kwangu, haiwezekani kwenye nyumba yangu mwenyewe mara naambiwa lala nje, Mara pika, mara kalale seblen, mara hivi, yani hii mimba nahisi nimeibeba mimi akyamungu, Bora ingebandikwa tumboni kwangu nkatembea nayo kila sehemu nkajulikana nna kitambi kuliko mateso haya nnayopata.

Ni maneno aliyokuwa akiyawaza mara kwa mara kutokana na mateso aliyokuwa akiyapata, Huku akisema mtu unaweza kukonda ghafla  hali ya kuwa unaishi vizuri na kulala katika nyumba nzuri.....

********
Siku zilizidi kuporomoka hatimae siku ya chuo ilifika, Msimu huu hakuwa Hamad tena aliemfata seid shamba, bali alikuwa ni Raya ambae aliitaji kumfata ili waende wote chuo.

Jumaa tatu asubuhi na mapema hamad alimpigia cm Seid kumuuliza kuhusu usafiri kama unasumbua au laa ili amfate, Seid alimuambia Asante na kumuomba aende tu chuo tayari amepata usafiri.

Kwa mara ya kwanza Raya tokea azaliwe anafika shamba kwa ajili ya kumfata Seid, japo hakuwai kufika lakini hakupotea kutokana na maelekezo ya bara bara.

Baada ya kufika alimkuta seid akiwa amesimama bara barani akimsubiria yeye, alipaki gari pembeni akashuka na kwenda kumkumbatia seid kwa nguvu, kwa furaha, kwa mapenzi ya hali ya juu.

Tokea azaliwe Seid hakuwai kukumbatiwa na mwanamke kimapenzi, alijikuta anaharibu mzunguko wote wa kiafya, Raya alimuangalia Seid na kuachia tabasam zito.

" I love you my beib boy ,,
" I love you too, tafadhali tuanze safari, tuna dakika chache tu za kuwa chuoni ,, alisema seid
" mbona unakaa mbali sana kiasi hiki na nyumba yenu iko wapi!!?
" Tutaongea tukiwa kwenye gari kwa sababu Chorz Dray anasema katika kitabu chake cha utakatifu you dont waste time when there is no time to lose again. 
" Umeanza mafumbo yako ebu Shika funguo.
" uuum
" Shika funguo!!!

Alishangaa sana kuona mtoto wa kike anampatia funguo akimanisha aendeshe yeye, aliichukua akaingia kwenye gari huku raya nae akizunguka upande wa pili, aliwasha gari akageuza na kuanza kuelekea chuoni huku wakipiga stori za hapa na pale.

TUKUTANE SEHEMU YA 17 Kesho Mahali Hapa Hapa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.