Man Walter Aelezea Sababu ya Alikiba Kutofanya Collabo na NE-YO - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Man Walter Aelezea Sababu ya Alikiba Kutofanya Collabo na NE-YO

Mtayarishaji wa nyimbo nyigi za msanii Alikiba , Man Walter amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa ya msanii Alikiba kushindwa kufanya collbao na msanii mkubwa duniani NE-YO katika wimbo wake wa Seduce me kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.

Man Walter anasema kuwa pamoja na kwamba maandalizi yalikuwa yamekamilika na kila kitu lakini walikuja kugundua kuwa msanii huyo alikuwa anakuja Afrika na alikuwa na collabo na wasanii wengi sana Afrika hivyo wakaona kuwa itachukua muda sana kuwasubirisha mashabiki .

"nilipigiwa simu kuwa kiba nakuja kufanyakazi na ne-yo na kweli nikatafuta biti ikawa kidogo inafanana na ile ya miss independence , nikaitoboa kidogo na nikapata kitu nilikuwa nataka yenye maazi ya kiafrika zaidi na hata kiba alifurahi sana.

tukatuma pia kwa neyo zile biti na zote alizipokea lakini baada ya hapo sijui kwa nini kiba aliamua kubadilisha maamuzi yake , labda pengine aliona kuwa ne-yo alikuwa na collabo na wasanii wengi sana afrika , watu wasije wakaona kama vile tumedandia kolabo ya bure tukaona bora tuachane nayo."


Tetesi za Alikiba kufanya kolabo na Ne-yo zilikuwa sana kipindi cha nyuma na baada ya muda ndipo pia hata Diamond alipata kolabo na msani huyo. Hivi karibuni kulikuwa na habari kwamba msanii Alikiba anatarajia kufanya kazi na Fally Ippupa kutoka Congo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.