Joyce Kiria: Siwezi Kuvumilia Ukatili na Machungu ya Ndoa Yangu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Joyce Kiria: Siwezi Kuvumilia Ukatili na Machungu ya Ndoa Yangu

Joyce Kiria: Siwezi Kuvumilia Ukatili na Machungu ya Ndoa Yangu
Mwanaharakati na mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amedai kuwa anapokea matusi na lugha za kebehi kutoka kwa watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutamka wazi miezi mitatu iliyopita kuwa ananyanyaswa na mumewe kwenye ndoa yake.

Joyce amesema kuwa matusi hayo na lugha za kebehi kwake anaona ni jambo la kawaida na ni afadhali kwake lakini sio kuvumilia maumivu aliyokuwa akiyapata kwenye ndoa yake na mumewe Henry Kilewo.

“Nachotaka kusema ni kwamba kwa vile nilichangua hii kazi  ya kuwa sauti za wanawake najua gharama zipo, na gharama kubwa kabisa ni kutukanwa lakini sio kwamba mimi sioni hayo matusi nayaona lakini navumilia. Kwahiyo sio kwamba siumii naumia!! na kuna wengine wananikosesha dili za matangazo kwenye kipindi changu kwa kuona nimejiharibia na mambo ya kisiasa.“ amesema Joyce Kiria kwenye kipindi chake cha Wanawake Live na kufafanua.

“Pamoja na machungu yote ninayoyapitia ya kutukanwa na kukosa wadhamini kwenye kipindi changu nikilinganisha na maumivu ya kwenye ndoa ni bora nitukanwe na jamii  lakini sio kuvumilia ukatili na machungu ya ndoa yangu.“ amesema Joyce Kiria.

Mwezi Januari, Joyce Kiria aliutangazia umma kuwa yeye na mumewe hawapo sawa kwenye ndoa yao kwani amekuwa akipigwa na kuachiwa majukumu yote ya kifamilia.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.