Hatimaye Neymar Amerudi Ufaransa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hatimaye Neymar Amerudi Ufaransa

Staa wa timu ya taifa ya Brazil anayecheza club ya Paris Stain Germain ya Ufaransa Neymar baada ya kuchukua headlines wiki kadhaa zilizopita kutokana na kutoonekana wakati wa game ya PSG na Monaco ya kutangaza Ubingwa wa Ligue One sasa amerejea.

Neymar amerejea Ufaransa baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake mwezi March nyumbani kwao Brazil na alikuwa anategemewa kuwa atarejea uwanjani wakati wa fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi lakini kuna tetesi kuwa anaweza kuichezea PSG kabla ya msimu kumalizika.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Neymar alichukua headlines wiki kadhaa zilizopita baada ya kutoonekana siku ya PSG wakitangazwa kuchukua Ubingwa na yeye akiwa kwao Brazil kitendo ambacho kilitafsiriwa na baadhi ya watu kama dharau.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.