Harmonize Amlipua Wolper na Kuanika Listi Nzima Ya Wapenzi Aliowahi Kuwa Nao. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Harmonize Amlipua Wolper na Kuanika Listi Nzima Ya Wapenzi Aliowahi Kuwa Nao.

Msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize ameingia tena kwenye vita ya maneno na Ex girlfriend wake staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper.

Siku ya jana kuna video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Wolper akimrushia Dongo Sarah ambaye ni mpenzi wa Harmonize kwa kumuita Mlezi wa wana baada ya taarifa kusambaa kuwa kamtosa Harmonize na kumchukua Mwarabu Fighter.

Baada ya kuona video hiyo, Harmonize alitokwa na povu zito kwani kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram alimtetea mpenzi wake Sarah na kusema yeye sio Mlezi wa wana ila Wolper ni Mlezi wa Wana na kuambatanisha na listi kamili ya wanaume wote aliokuwa nao kwenye mahusiano.

Hii sio mara ya kwanza kwa Harmonize na Wolper kuwa na sintofahamu na hata Wolper na mpenzi wa Harmonize Sarah.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.